Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

Kifo cha Rais Magufuli kimefunua siri ambayo nadhani wengi hawakuwahi kuijua. Kifo cha Rais Magufuli kimeonyesha jinsi ambavyo Rais Samia alikuwa hajui siri za nchi ambazo kwa wadhifa wake kama Makamu wa Rais alitakiwa awe anajua!

Nakumbuka hata Rais Magufuli alipoingia madarakani alikuwa hajui siri nyingi za nchi lakini hili halikunishangaza sana kwa sababu alikuwa waziri tu kabla ya kuwa Rais wa Tanzania. Waziri hawezi kujua siri za ulinzi na usalama ambazo kwanza zinamfikia Rais kama Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa wanaokumbuka vizuri, baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani aliwaondoa wafanyakazi wengi hasa wa vyeo vya juu katika nafasi zao bila kujua baadhi yao ni sehemu ya watu wa usalama wa taifa(TISS). Mmoja wa wale waliondolewa ni Diwani Athumani Msuya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai(DCI) na kupelekwa kuwa Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera.

Baada ya Rais Magufuli kuanza kupata classified intelligence briefings kutoka kwenye taasisi za ulinzi na usalama nchini ndio akajua alichokifanya pia kwa Diwani Athumani Msuya ni makosa ya bila kujua kwa sababu Diwani ni sehemu ya Usalama wa Taifa ndio maana akamrudisha na kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Kwa wenye kumbukumbu, Rais Magufuli baada ya kuingia madarakani alianzisha mahusiano ya karibu na Rais Kagame lakini yalipungua sana baada ya kupata classified intelligence briefings kuhusu faida na athari zake kwa taifa.

Kilichonishangaza zaidi ni kuona kuwa Makamu wa Rais kwa zaidi ya miaka mitano ambaye kwa sasa amekuwa Rais wa Tanzania hana uelewa mkubwa wa mambo yanayoendelea hasa ya ulinzi na usalama nchini.

Rais Samia baada ya kuapishwa kuwa Rais alianza naye kusikiliza kelele za kwenye mitandao na kuanza kuondoa watu mbalimbali katika nafasi zao za kazi huku pia akiagiza wafanyiwe uchunguzi bila kujua kuwa baadhi ya watu hao ni sehemu ya usalama wa Taifa. Hii inaonyesha pamoja na kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa zaidi ya miaka mitano lakini hajui kinachoendelea nchini hasa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

Kwa sasa nadhani baada ya kuanza kupata classified intelligence briefings kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama ameanza kuujua ukweli na kujikuta hata baadhi ya chunguzi ambazo alielekeza zifanyike zinakuwa ''redundant''.

Yanayoanza kutokea kwa sasa yanadhihirisha Rais Samia hakupata classified intelligence briefings wakati akiwa Makamu wa Rais. Kwa sasa baada ya kuanza kupewa hata aina tabia za kiuongozi zimeanza kubadilika. waliokuwa wanalia wameanza kucheka na waliokuwa wanacheka wameanza kulia!

Wanaoijua ''system ya utawala'' nchini hawawezi kushangaa kuona uchunguzi wa BOT na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini(TPA) Deusdedit Kakoko ukiishia kwenye makabati ya Ikulu!

Hata kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai inaweza kufia njiani, fikria eti kwa sasa mashitaka yamebadilishwa na anashitakiwa kwa kosa la kuiba kiasi cha Tsh 3,125,000 na simu aina ya Techno. Haya makosa yamefanyika siku moja katika duka moja! Yaani Sabaya huyu ambaye tuliaminishwa kwenye magazeti na mitandao anabaka, anachukua mamilioni ya shilingi kwa nguvu na kufisadi eti ameiba simu ya Techno!

Hii imenifanya nijiulize; Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndio mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo nchini?

Kama Rais Samia akiwa Makamu wa Rais hakupewa classified intelligence briefings ni kutokana na mfumo wa ulinzi na usalama basi kanuni zake inabidi zibadilishwe! Kama hakupewa kwa sababu alikuwa haaminiki, kwa nini hakuaminika wakati ni Makamu wa Rais?

Nchini Marekani tatizo hili la Makamu wa Rais kutojua kinachoendelea katika nchi hasa kwenye suala la ulinzi na usalama walilifanyia kazi mwaka 1945 baada ya Harry Truman ambaye alikuwa Makamu wa Rais kwa siku 82 tu na kujikuta anakuwa Rais wa nchi baada ya Rais Franklin Roosevelt kufariki. Wakati akiwa Makamu wa Rais hakujua kama kuna mradi uliojulikama kama ''Manhattan project'' ambao ulikuwa mahsusi kutengeneza bomu la atomiki.

Baada ya Harry Truman kuapishwa na kuwa Rais na kugundua udhaifu huo alijiapisha kuwa huo udhaifu hauwezi kutokea tena kwa Rais mwingine kuingia madarakani bila kuandaliwa kwanza kwa kupewa intelligence briefings. Utaratibu wa kupewa intelligence briefings umeendelea mpaka leo hasa pale vyama vikuu viwili vinapoteua wagombea Urais ambapo huanza kupewa intelligence briefings ili wakati wa kampeni wajue ni mambo gani wanatakiwa wayaseme kwenye mikutano ya hadhara ili kulinda maslahi ya taifa.

Watu au taasisi hujifunza kutokana na makosa, Kwa msingi huu yaliyotokea inabidi liwe ni funzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa faida ya Taifa!
Katiba mpya ndoa jibu la hayo
 
Kwamba mtu akiwa usalama wa Taifa amepewa kibali chakuwa jizi? Hawezi kuchunguzwa? Akiwa mzembe hawezi kuwajibishwa?

Jinga kabisa.
 
Hivi kwa yule boss wa Madawa ya kulevya Mh. KJ imekuaje kasitishiwa utumishi ilihali amehudumu katika idara ya usalama kwa takribani miaka 30 sasa. Isije kuwa Mama analishwa sumu ni bora kwa mtu kama yule kupelekwa ubalozini na si kuachwa tu, Ombi kwake Mh. Raisi alifikirie hili suala kwa mapana zaidi maana bwana yule kashika sehemu nyeti sana za idara katika utumishi wake.
Kaji hana lolote, ni Sukuma gang tu, msimtishe mama tunamlinda hakuna kima yoyote wa kusumbuwa utawala huu.
 
boss wa Madawa ya kulevya Mh. KJ

Gerald au?

Unasema ni Teeth TOKA lini?
Kaji ni Tiss kitambo tu. Tatizo wajinga wengi wamo kwenye hiyo idara akiwemo huyo Kaji.

Na ameshafukuzwa kazi rasmi humo idarani, ni raia kama wewe tu na hana lolote jinga fulani tu.
 
Umewahi kujiuliza kama hao unaodai ni wapinzani wananunuliwa wakati kumbe hao pia ni sehemu ya ''system''!

Kama tunamjadili Makamu wa Rais asiyejua kinachoendelea nchini utawezaje wewe kujua wakati hata mlango wa Ikulu hujui umekaa upande gani?
Binadamu wengi wa kitanzania wana tabia ya kushabikia mambo mengi wasiyokuwa na uelewa juu yake. Leo anakwambia flani kanunuliwa kumbe hajui mwezie alikuwa akitimiza majukumu huko alikokuwa na wafuata upepo wakiwa nyuma yake kwa kishindo kikubwa.
 
Usilete dharau, tunawajuwa hata Kadinali Pengo na Sheikh mkuu wa Dar ni watu wao, hawa huwa wanaitwa Agents, huitaji kwenda depo ya kijeshi ili kuwa Agent.
 
Unawajua wewe na nani mkuu, usipende kutumia wingi. Ni ushauri tu.
 
Sukuma gang endeleeni kudanganyana na kufarijiana, Sabaya yupo jela na ataendelea kuwa jela mpaka amalize kutumikia kifungo na atakuwa amepata fundisho.

Walidhani yule kichaa ataishi milele.
Hakuna cha sukuma genge wala nini linapokuja suala la kitaifa na sura halisi ya taasisi za umma zilivyonajisiwa.

Mzee Matola, mimi si kibendera fuata upepo kama unavyodhania wewe.

Kusema hivyo niliandika huku nikitafakari namna gani waliopewa mamlaka ya mashitaka wasivyojali matokeo ya uandaaji wa kesi zenye mvuto kwa umma.

Bila kujali athari za matokeo kwa umma, wao hutumia hila zao kwa makusudi kupotosha mashitaka na mwisho wa sakata waliyemshitaki huibuka mshindi.

Siangalii mtu atakaa rumande muda gani, bali naangalia mwisho wa kesi utakuwaje, maana mwanzoni kabisa inaonesha walioandaa kesi hiyo ni kama walifanya kwa kukurupuka kwa shinikizo ama bila weledi kitaaluma.

Nikatolea mfano wa kesi ya kina Zombe na genge lake.
 
Kaji ni Tiss kitambo tu. Tatizo wajinga wengi wamo kwenye hiyo idara akiwemo huyo Kaji.

Na ameshafukuzwa kazi rasmi humo idarani, ni raia kama wewe tu na hana lolote jinga fulani tu.
Mkuu idara ya usalama wa taifa ukiwa mwajiliwa kwa level yoyot ile huwezi kuacha kazi mpka unaingia kabulini, ila ajira inaweza kukoma kwa maana ya majukum ya kila siku ila kazi haitaisha mpka wanakuzika, na siku ya kuzika lazima watume wat Zaid ya 1 kuja kujilidhisha Kama kwel umekufa na umezikwa, hii ndo idara ambayo watu hawajuani ila wanafanya kazi Kama wanajuana..

Humo ndn,kunaviongoz wema, waovu, majambaz, wafanyabiashara wahuni, wavuta bangi, wanasiasa, wachungaji, waumini, wanamitindo, Malaya n.k..
Mkuu hakuna uelwa sahihi wa taasis hii kwa sisi raia tu wa kawaida, mambo mengine mkuu Ni aheri kutokuyajua maana ukiyajua yatakusumbua na hutaweza kuyatatua....
 
Hii ni overrated tu, Idara hii ya usalama wa Taifa ni moja ya idara za Hovyo hapa nchini. Msingi wa idara hii na ukakasi wa kuhariri sheria inayoipa nguvu ya kimamlaka kwa pamoja vinaendelea kuifanya Idara hii kuishi kwa nadharia katika mitazamo ya kiujamaa ya kukihami chama tawala zaid kuliko maslahi mapana ya nchi.

Kuna vilaza na watu wengi sana wasio na uwezo wanaofanya kazi katka Idara hii nyeti. Kuna mifano mingi ya maafisa Usalama wa Taifa kufanya fyongo, Blunders na hata incompetence wanapokuwa field. Upo mfano wa Afisa usalama kumkimbia Accused Gaidi fulan ambaye alitumwa kumfuatilia na kuchora life pattern yake.

Kwa madhila ya mikataba mibovu, wizi uliokithiri, ubadhirifu wa mali za umma unaofanywa na baadhi ya watumishi. Ujambazi wa viongozi, teuzi mbovu na kulindan kwa maslah ya tumbo, kote huku kunaiganya idara hii kuwa incompetence kwa kushindwa kusimamia Taaluma ya ushushu na utekelezaji wa mipango kazi katka kuyahami maslah mapana ya nchi hata kwa maadui wa ndani waliojipenyeza katika System.

Idara hii n idara ya chama Tawala kiutendaji. Idara hii ni moja ya Idara mbovu na kipuuzi zinazofifisha ustawi wa taifa hili. Idara hii n moja ya taasisi zinazochagiza mpasuko wa kitaifa kwa kuwa brutal na wote wenye fikra kinzani na viongozi mburula wa Chama Tawala.

Huo umakini wa ufuatiliaji na ujiridhishaji na sifa kedekede zinazoelekezwa katika Idara hii n Hoax stories tu. Hii ni moja ya Idara mbovu kuwepo ndani ya nchii hii. Huenda n mbovu zaid kuliko hata Jeshi la Polisi.

Kama circle system ya nchi hii ndo ina watu kama akina Lengai, kuna nini tena?
 
Idara hii ilikuwa ni branch ndani ya jeshi la Polisi kabla ya kutengwa na kupelekwa ofisi ya Rais.

Kwahiyo ule ujingaujinga na ubabaishaji ni uleule.
 
Back
Top Bottom