Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,412
2,000
Sometime is better to blame the system, na sio kiongozi, maana inaonesha kiongoz akishika madaraka, zile siku za mwanzo anakuwa na nia njema ya kuwatumikia wananchi, lkn baada ya muda mfupi anarudishwa ktk factory reset ya system iliyomuweka madarakan kwa kufanya na kufuata agenda nzma za system bila kuvunja mashart, ndio kama muonavyo kwa samia, mwanzo inawezekana hakujua hali ikoje ktk utawala.lkn baada ya kuingia ndyo anaanza kuwekwa sawa na wenyenchi yao...ccm ni ilee ilee
Uko right. Kwa mfumo huu hata aingie nani hawezi ku-perform vizuri. Kitu cha kwanza ni kuwa mfumo unamfanya rais achanganyikiwe kwa sababu anakutana na vitu vingi sana vya kufanya. Akishachanganyikiwa ndiyo anaanza kulainika na wapambe ndiyo wanaingia kufanya yao. Kumbuka kuna watu huu mfumo ndiyo kula yao na hawatakubali hata siku moja ubadilike.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,916
2,000
Kwani ukiwa usalama wa taifa ukiwa mwizi haushugulikiwi?

Acha upumbavu basi

Hakuna usalama yeyote anawezafanya kosa la jinai na akaachwa labda kwenye mfumo kama wetu uliasisiwa na ccm na magenge yake.

Acha ushamba.
 

mazagazagatza

Senior Member
Jul 15, 2021
106
225
Naona umeoverrate mfumo wa usalama wa Tanzania. Hakuna chochote cha maana kuhusu hiyo intelligent system bali kuna kamati kuu ya CCM. Hiyo ndio kila kitu, mifumo mingine yote ni mbwa tu hapa Tanzania. Kila kitu ni siasa, tena siasa chafu chafu. Wewe ujiulizi inakuwaje baadhi ya viongozi wa upinzani wananunuliwa na kuhamia CCM halafu huko wanakwenda kupewa vyeo vya juu vya serikali. Ni lini waliandaliwa na kuaminiwa na mtawala wa CCM?

Watu wengi wanaaminishwa kuwa hapa Tanzania viongozi ni watu smart na kuna mfumo smart wa kuratibu mambo ya kiungozi na usalama hapa Tanzania, lakini kiuhalisia viongozi wengi ni mazezeta na mfumo ni mbovu kupita maelezo.
 

mazagazagatza

Senior Member
Jul 15, 2021
106
225
Kwamba Sabaya anaenda kuiba simu aina ya Techno kwa kutumia silaha! Nchi hii kuna sanaa na maigizo ya aina yake!
Hilo gazeti refuuu uliooandika hapo juu kumbe lengo ilikuwa kumtetea jambazi mwenzio Sabaya?

Sijui classified intelligence briefing,sijui kitu gani..... Usalama wa taifa wanaruhusiwa kuwa wahalifu...unajaribu kutuaminisha nini?

Kama ni kweli unayosema basi nchi hii inatawaliwa na genge la wahuni. Bahati nzuri unayosema siyo ya kweli!
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,432
2,000
..kwamba upo uwezekano Sabaya alitumwa na "system" kuvamia hoteli ya Mbowe?

..pia upo uwezekano "system" ilimuelekeza atumie gari yenye namba feki za UN?

..Na "system" haikuhakikisha kwamba Sabaya hataonekana ktk CCTV camera?

..nadhani umeidharau sana "system" kiasi cha kufikiria inaweza kushiriki jambo la kipumbavu namna ile.

..kwa upande mwingine "system" inaundwa na binadamu kama mimi na wewe, na kila binadamu ana mapungufu.
Bandiko lako hili limenifikirisha tukio la intel wa UK kuacha nyaraka za siri stendi kuhusu ile meli ya kupita karibu na Crimea!!! Je. Press ilikuwa inatudharau sisi wasomaji ama UK intel iliteleza kweli!?
 

lwiva

JF-Expert Member
Apr 17, 2015
5,209
2,000
Kwa hiyo viongozi/wafanyakazi wa usalama wana haki ya kuiba ama kufanya uhalifu wowote kwa kadiri wanavyojisikia?
Huyo ni boya ajui uchunguzi na ukaguzi anao fanya mama ni bosheni tu kwa sababu ya kivuli cha magufuli
 

mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,435
2,000
Kifo cha Rais Magufuli kimefunua siri ambayo nadhani wengi hawakuwahi kuijua. Kifo cha Rais Magufuli kimeonyesha jinsi ambavyo Rais Samia alikuwa hajui siri za nchi ambazo kwa wadhifa wake kama Makamu wa Rais alitakiwa awe anajua!

Nakumbuka hata Rais Magufuli alipoingia madarakani alikuwa hajui siri nyingi za nchi lakini hili halikunishangaza sana kwa sababu alikuwa waziri tu kabla ya kuwa Rais wa Tanzania. Waziri hawezi kujua siri za ulinzi na usalama ambazo kwanza zinamfikia Rais kama Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa wanaokumbuka vizuri, baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani aliwaondoa wafanyakazi wengi hasa wa vyeo vya juu katika nafasi zao bila kujua baadhi yao ni sehemu ya watu wa usalama wa taifa(TISS). Mmoja wa wale waliondolewa ni Diwani Athumani Msuya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai(DCI) na kupelekwa kuwa Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera.

Baada ya Rais Magufuli kuanza kupata classified intelligence briefings kutoka kwenye taasisi za ulinzi na usalama nchini ndio akajua alichokifanya pia kwa Diwani Athumani Msuya ni makosa ya bila kujua kwa sababu Diwani ni sehemu ya Usalama wa Taifa ndio maana akamrudisha na kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Kwa wenye kumbukumbu, Rais Magufuli baada ya kuingia madarakani alianzisha mahusiano ya karibu na Rais Kagame lakini yalipungua sana baada ya kupata classified intelligence briefings kuhusu faida na athari zake kwa taifa.

Kilichonishangaza zaidi ni kuona kuwa Makamu wa Rais kwa zaidi ya miaka mitano ambaye kwa sasa amekuwa Rais wa Tanzania hana uelewa mkubwa wa mambo yanayoendelea hasa ya ulinzi na usalama nchini.

Rais Samia baada ya kuapishwa kuwa Rais alianza naye kusikiliza kelele za kwenye mitandao na kuanza kuondoa watu mbalimbali katika nafasi zao za kazi huku pia akiagiza wafanyiwe uchunguzi bila kujua kuwa baadhi ya watu hao ni sehemu ya usalama wa Taifa. Hii inaonyesha pamoja na kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa zaidi ya miaka mitano lakini hajui kinachoendelea nchini hasa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

Kwa sasa nadhani baada ya kuanza kupata classified intelligence briefings kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama ameanza kuujua ukweli na kujikuta hata baadhi ya chunguzi ambazo alielekeza zifanyike zinakuwa ''redundant''.

Yanayoanza kutokea kwa sasa yanadhihirisha Rais Samia hakupata classified intelligence briefings wakati akiwa Makamu wa Rais. Kwa sasa baada ya kuanza kupewa hata aina tabia za kiuongozi zimeanza kubadilika. waliokuwa wanalia wameanza kucheka na waliokuwa wanacheka wameanza kulia!

Wanaoijua ''system ya utawala'' nchini hawawezi kushangaa kuona uchunguzi wa BOT na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini(TPA) Deusdedit Kakoko ukiishia kwenye makabati ya Ikulu!

Hata kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai inaweza kufia njiani, fikria eti kwa sasa mashitaka yamebadilishwa na anashitakiwa kwa kosa la kuiba kiasi cha Tsh 3,125,000 na simu aina ya Techno. Haya makosa yamefanyika siku moja katika duka moja! Yaani Sabaya huyu ambaye tuliaminishwa kwenye magazeti na mitandao anabaka, anachukua mamilioni ya shilingi kwa nguvu na kufisadi eti ameiba simu ya Techno!

Hii imenifanya nijiulize; Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndio mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo nchini?

Kama Rais Samia akiwa Makamu wa Rais hakupewa classified intelligence briefings ni kutokana na mfumo wa ulinzi na usalama basi kanuni zake inabidi zibadilishwe! Kama hakupewa kwa sababu alikuwa haaminiki, kwa nini hakuaminika wakati ni Makamu wa Rais?

Nchini Marekani tatizo hili la Makamu wa Rais kutojua kinachoendelea katika nchi hasa kwenye suala la ulinzi na usalama walilifanyia kazi mwaka 1945 baada ya Harry Truman ambaye alikuwa Makamu wa Rais kwa siku 82 tu na kujikuta anakuwa Rais wa nchi baada ya Rais Franklin Roosevelt kufariki. Wakati akiwa Makamu wa Rais hakujua kama kuna mradi uliojulikama kama ''Manhattan project'' ambao ulikuwa mahsusi kutengeneza bomu la atomiki.

Baada ya Harry Truman kuapishwa na kuwa Rais na kugundua udhaifu huo alijiapisha kuwa huo udhaifu hauwezi kutokea tena kwa Rais mwingine kuingia madarakani bila kuandaliwa kwanza kwa kupewa intelligence briefings. Utaratibu wa kupewa intelligence briefings umeendelea mpaka leo hasa pale vyama vikuu viwili vinapoteua wagombea Urais ambapo huanza kupewa intelligence briefings ili wakati wa kampeni wajue ni mambo gani wanatakiwa wayaseme kwenye mikutano ya hadhara ili kulinda maslahi ya taifa.

Watu au taasisi hujifunza kutokana na makosa, Kwa msingi huu yaliyotokea inabidi liwe ni funzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa faida ya Taifa!
Kuwa usalama wa taifa sio kinga ya kufanya uhalifu.
 

diranqhe

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
1,213
2,000
Hata hilo unalosema alivamia hotel ya Mbowe, Kama kweli alivamia tutajuaje kama hakutumwa na ''system'' kufanya hivyo?

Kama nilivyosema kwenye mada yangu, inaonyesha Rais Samia hakujua yanayoendelea nchini na kwa mantiki hii hata kutaka kufanya uchunguzi alisema wakati hajapata picha halisi ya ulinzi na usalama nchini!
Umeandika utumbo mtupu. Usalama wa taifa sio tiketi ya kufanya maovu. Huyo mumeo Sabaya unayemtetea kafanya maovu yasiyohitaji maelezo mengi zaidi ya kumfikisha mahakamani. Kamati ya maadili ya CCM ndo kila kitu nchi hii. Muulize Lowassa atakupa jibu sahihi kuhusu hiyo kamati.
 

MORIA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
623
250
Nini unataka kusema?
Kwamba Sabaya ni afisa wa usalama wa taifa? Kama ni ndio kuna kipindi alishawahi kushtakiwa kwa kujifanya usalama wa taifa?
Taifa hili usalama wa taifa ni watu wa hovyo tu isipokuwa wachache sana wanaoijua vyema kazi yao.
Jamaa ni bora ndo maana tuko salama hata leo...tusifie vyetu, tutasifia cia mpaka lini !? Ajionavyo mtu ....
 

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
994
1,000
Neno ''wanavyojisia'' halipo kwenye majukumu ya ofisa wa Usalama wa Taifa!

Hoja ya msingi ni kuwa utajuaje kama alichofanya amekifanya kama ''anavyojisikia'' na sio kama ''alivyotumwa''.

Wenye historia ya nchi hii tunajua kuwa wakati wa vita vya uhujumu uchumi vilivyoongozwa na Marehemu Sokoine wakati wa utawala wa Nyerere, kuna watu wa usalama wa taifa ilibidi waonekane kama wamekamatwa na kupelekwa gerezani kama wahujumu uchumi lakini kiuhalisia walikuwa kazini kwenda kuwapeleleza mahabusu wengine waliokamatwa kwa kesi hizo.
Na wengine walipotoka huko wakaoata na U DC U RDD na ukadhalika
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom