Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Kifo cha Rais Magufuli kimefunua siri ambayo nadhani wengi hawakuwahi kuijua. Kifo cha Rais Magufuli kimeonyesha jinsi ambavyo Rais Samia alikuwa hajui siri za nchi ambazo kwa wadhifa wake kama Makamu wa Rais alitakiwa awe anajua!

Nakumbuka hata Rais Magufuli alipoingia madarakani alikuwa hajui siri nyingi za nchi lakini hili halikunishangaza sana kwa sababu alikuwa waziri tu kabla ya kuwa Rais wa Tanzania. Waziri hawezi kujua siri za ulinzi na usalama ambazo kwanza zinamfikia Rais kama Amiri Jeshi Mkuu.

Kwa wanaokumbuka vizuri, baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani aliwaondoa wafanyakazi wengi hasa wa vyeo vya juu katika nafasi zao bila kujua baadhi yao ni sehemu ya watu wa usalama wa taifa(TISS). Mmoja wa wale waliondolewa ni Diwani Athumani Msuya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai(DCI) na kupelekwa kuwa Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera.

Baada ya Rais Magufuli kuanza kupata classified intelligence briefings kutoka kwenye taasisi za ulinzi na usalama nchini ndio akajua alichokifanya pia kwa Diwani Athumani Msuya ni makosa ya bila kujua kwa sababu Diwani ni sehemu ya Usalama wa Taifa ndio maana akamrudisha na kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Kwa wenye kumbukumbu, Rais Magufuli baada ya kuingia madarakani alianzisha mahusiano ya karibu na Rais Kagame lakini yalipungua sana baada ya kupata classified intelligence briefings kuhusu faida na athari zake kwa taifa.

Kilichonishangaza zaidi ni kuona kuwa Makamu wa Rais kwa zaidi ya miaka mitano ambaye kwa sasa amekuwa Rais wa Tanzania hana uelewa mkubwa wa mambo yanayoendelea hasa ya ulinzi na usalama nchini.

Rais Samia baada ya kuapishwa kuwa Rais alianza naye kusikiliza kelele za kwenye mitandao na kuanza kuondoa watu mbalimbali katika nafasi zao za kazi huku pia akiagiza wafanyiwe uchunguzi bila kujua kuwa baadhi ya watu hao ni sehemu ya usalama wa Taifa. Hii inaonyesha pamoja na kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa zaidi ya miaka mitano lakini hajui kinachoendelea nchini hasa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

Kwa sasa nadhani baada ya kuanza kupata classified intelligence briefings kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama ameanza kuujua ukweli na kujikuta hata baadhi ya chunguzi ambazo alielekeza zifanyike zinakuwa ''redundant''.

Yanayoanza kutokea kwa sasa yanadhihirisha Rais Samia hakupata classified intelligence briefings wakati akiwa Makamu wa Rais. Kwa sasa baada ya kuanza kupewa hata aina tabia za kiuongozi zimeanza kubadilika. waliokuwa wanalia wameanza kucheka na waliokuwa wanacheka wameanza kulia!

Wanaoijua ''system ya utawala'' nchini hawawezi kushangaa kuona uchunguzi wa BOT na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini(TPA) Deusdedit Kakoko ukiishia kwenye makabati ya Ikulu!

Hata kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai inaweza kufia njiani, fikria eti kwa sasa mashitaka yamebadilishwa na anashitakiwa kwa kosa la kuiba kiasi cha Tsh 3,125,000 na simu aina ya Techno. Haya makosa yamefanyika siku moja katika duka moja! Yaani Sabaya huyu ambaye tuliaminishwa kwenye magazeti na mitandao anabaka, anachukua mamilioni ya shilingi kwa nguvu na kufisadi eti ameiba simu ya Techno!

Hii imenifanya nijiulize; Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndio mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo nchini?

Kama Rais Samia akiwa Makamu wa Rais hakupewa classified intelligence briefings ni kutokana na mfumo wa ulinzi na usalama basi kanuni zake inabidi zibadilishwe! Kama hakupewa kwa sababu alikuwa haaminiki, kwa nini hakuaminika wakati ni Makamu wa Rais?

Nchini Marekani tatizo hili la Makamu wa Rais kutojua kinachoendelea katika nchi hasa kwenye suala la ulinzi na usalama walilifanyia kazi mwaka 1945 baada ya Harry Truman ambaye alikuwa Makamu wa Rais kwa siku 82 tu na kujikuta anakuwa Rais wa nchi baada ya Rais Franklin Roosevelt kufariki. Wakati akiwa Makamu wa Rais hakujua kama kuna mradi uliojulikama kama ''Manhattan project'' ambao ulikuwa mahsusi kutengeneza bomu la atomiki.

Baada ya Harry Truman kuapishwa na kuwa Rais na kugundua udhaifu huo alijiapisha kuwa huo udhaifu hauwezi kutokea tena kwa Rais mwingine kuingia madarakani bila kuandaliwa kwanza kwa kupewa intelligence briefings. Utaratibu wa kupewa intelligence briefings umeendelea mpaka leo hasa pale vyama vikuu viwili vinapoteua wagombea Urais ambapo huanza kupewa intelligence briefings ili wakati wa kampeni wajue ni mambo gani wanatakiwa wayaseme kwenye mikutano ya hadhara ili kulinda maslahi ya taifa.

Watu au taasisi hujifunza kutokana na makosa, Kwa msingi huu yaliyotokea inabidi liwe ni funzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa faida ya Taifa!
 
20210721_193345.jpg


Mama kwa sasa ameiva....
 
Naona umeoverrate mfumo wa usalama wa Tanzania. Hakuna chochote cha maana kuhusu hiyo intelligent system bali kuna kamati kuu ya CCM. Hiyo ndio kila kitu, mifumo mingine yote ni mbwa tu hapa Tanzania.

Kila kitu ni siasa, tena siasa chafu chafu. Wewe ujiulizi inakuwaje baadhi ya viongozi wa upinzani wananunuliwa na kuhamia CCM halafu huko wanakwenda kupewa vyeo vya juu vya serikali. Ni lini waliandaliwa na kuaminiwa na mtawala wa CCM?

Watu wengi wanaaminishwa kuwa hapa Tanzania viongozi ni watu smart na kuna mfumo smart wa kuratibu mambo ya kiungozi na usalama hapa Tanzania, lakini kiuhalisia viongozi wengi ni mazezeta na mfumo ni mbovu kupita maelezo.
 
Back
Top Bottom