Je, Rais Magufuli ni jibu la sala na maombi ya watanzania?

broken ages

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
235
84
Ikiwa unamwamini MUNGU utapaswa pia umwamini katika maombi unayoyafanya,

Ninakumbuka kwamba kipindi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 watanzania tulimwomba MUNGU sana kwa habari ya uchaguzi wa rais na kwamba tulikuwa tukimwomba MUNGU atupe rais ambaye atatufaa watanzania na ambaye angetuvusha na kama kumbukumbu zangu zitakuwa sawa hatukumwomba MUNGU pengine tukilenga kwa kuwataja majina wale waliokuwa wagombe kwa wakati ule, bali tuliomba mungu kwamba atuchagulie rais ambaye atawafaa watanzania.

Mwisho wa siku MUNGU yule yule tuliyekuwa tukimwomba alitupatia rais tuliye naye sasa ambaye ni MAGUFULI.
Ajabu ni kwamba hata baada ya kumpata rais hatukupiga tena magoti kumshukuru MJNGU kwamba asante kwa kuyajibu maombi yetu bali tulimfanyia dhihaka MUNGU ya kwamba kwa nini umetupa huyu? Je hii siyo laana kwa watanzania? na je MUNGU wetu si mwaminifu?

Je, watanzania tulimtaka rais yupi na wa namna gani? je sisi watanzania mbona ni watu tusioridhika?. Mlimtaka rais ambaye angeiuza nchi hii vipandevipande?na mbona utawala uliokuwepo kabla ya magufuli mliupigia kelele nyingi sana kwamba haukufanya vizuri kwa maendeleo ya watanzania?,

Kwa sababu hatujachelewa bado tunayo nafasi na tunapaswa hata sasa kumshukuru MUNGU kwa maana alitupa rais aliyetawala kwa amani na tena ameyafanya mapenzi yake MUNGU kwani ametutawala na kutuongoza ktk haki na kweli bila kusahau kuwa hata kipindi chake cha uongozi limekuwepo janga la corona alitutia moyo na ujasiri mkubwa sana watanzania kiasi cha kutuondolea hofu iliyoitawaka dunia nzima na badala yake akatuongoza kumtegemea MUNGU zaidi huku yukichapa kazi na hatimaye MUNGU ametushindia.

Kimefika kipindi kingine cha uchaguzi watanzania msiache na wala msichoke kumwomba MUNGU kutuchagulia tena rais kwa mara nyingine ili tutakapokuwa tumemaliza uchaguzi na tukampata rais tutakayempata tumshukuru MUNGU na tumpe ushirikiano kwa sababu tutakuwa tumepewa na MUNGU na hii ni bila kujali ikiwa rais huyo ajaye ni yule umpendaye ama usiyempenda.

Mwamini MUNGU naye atakuchagulia mtawala mfalme,ikitokea akawa rais ni MAGUFULI kwa kipindi kingine tufanye furaha na vigelegele maana ni MUNGU atakuwa amefanya ili taifa la TANZANIA likapate kumtukuza kwa sababu hiyo,
 
Watanzania msiache na wala msichoke kumwomba MUNGU kutuchagulia tena rais kwa mara nyingine ili tutakapokuwa tumemaliza uchaguzi na tukampata rais tutakayempata tumshukuru MUNGU na tumpe ushirikiano kwa sababu tutakuwa tumepewa na MUNGU.
AMEN.
Rais Magufuli azidi Kuthibitisha kuwa ni Rais wa watu, anawasikiliza watu Hakuna cha 'Mswalie Mtume' big Up Rais Magufuli
Wanabodi,
Rais Magufuli ndiye chaguo la Mungu kwa Tanzania, kuiondoa hii nchi kwenye lindi la umasikini uliotopea na kuifikisha kule Tanzania ilikopaswa kuwepo, kuwa nchi ya ahadi.
Paskali
Bariadi Simiyu (Jirani na Gambosh)

P
 
Ikiwa unamwamini MUNGU utapaswa pia umwamini katika maombi unayoyafanya,

Ninakumbuka kwamba kipindi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 watanzania tulimwomba MUNGU sana kwa habari ya uchaguzi wa rais na kwamba tulikuwa tukimwomba MUNGU atupe rais ambaye atatufaa watanzania na ambaye angetuvusha na kama kumbukumbu zangu zitakuwa sawa hatukumwomba MUNGU pengine tukilenga kwa kuwataja majina wale waliokuwa wagombe kwa wakati ule, bali tuliomba mungu kwamba atuchagulie rais ambaye atawafaa watanzania.

Mwisho wa siku MUNGU yule yule tuliyekuwa tukimwomba alitupatia rais tuliye naye sasa ambaye ni MAGUFULI.
Ajabu ni kwamba hata baada ya kumpata rais hatukupiga tena magoti kumshukuru MJNGU kwamba asante kwa kuyajibu maombi yetu bali tulimfanyia dhihaka MUNGU ya kwamba kwa nini umetupa huyu? Je hii siyo laana kwa watanzania? na je MUNGU wetu si mwaminifu?

Je, watanzania tulimtaka rais yupi na wa namna gani? je sisi watanzania mbona ni watu tusioridhika?. Mlimtaka rais ambaye angeiuza nchi hii vipandevipande?na mbona utawala uliokuwepo kabla ya magufuli mliupigia kelele nyingi sana kwamba haukufanya vizuri kwa maendeleo ya watanzania?,

Kwa sababu hatujachelewa bado tunayo nafasi na tunapaswa hata sasa kumshukuru MUNGU kwa maana alitupa rais aliyetawala kwa amani na tena ameyafanya mapenzi yake MUNGU kwani ametutawala na kutuongoza ktk haki na kweli bila kusahau kuwa hata kipindi chake cha uongozi limekuwepo janga la corona alitutia moyo na ujasiri mkubwa sana watanzania kiasi cha kutuondolea hofu iliyoitawaka dunia nzima na badala yake akatuongoza kumtegemea MUNGU zaidi huku yukichapa kazi na hatimaye MUNGU ametushindia.

Kimefika kipindi kingine cha uchaguzi watanzania msiache na wala msichoke kumwomba MUNGU kutuchagulia tena rais kwa mara nyingine ili tutakapokuwa tumemaliza uchaguzi na tukampata rais tutakayempata tumshukuru MUNGU na tumpe ushirikiano kwa sababu tutakuwa tumepewa na MUNGU na hii ni bila kujali ikiwa rais huyo ajaye ni yule umpendaye ama usiyempenda.

Mwamini MUNGU naye atakuchagulia mtawala mfalme,ikitokea akawa rais ni MAGUFULI kwa kipindi kingine tufanye furaha na vigelegele maana ni MUNGU atakuwa amefanya ili taifa la TANZANIA likapate kumtukuza kwa sababu hiyo,
Hakuna dikteta anayetoka kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom