Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,495
- 51,090
Kikao cha UN General assembly kinafanyika tena mwezi wa tisa mwaka huu kama ilivyo ada
Ni mwaka wa nne huu wa utawala wa Rais Magufuli hajawahi kusafiri kutoka nje ya Afrika, tofauti na watangulizi wake, Mheshimiwa Magufuli hajahudhuria kikao hata kimoja cha UN General assembly.
Kikawaida vikao vya General assmebly ni vikao vyenye hadhi ya wakuu wa nchi ambapo mambo mengi huzungumzwa pale lakini ukiacha mbali na hapo huwa ni nafasi nzuri kwa mkuu wa nchi mmoja kupata nafasi ya kuongea na kukubaliana mambo mengi ya maendeleo na wakuu wenzie wa nchi mbalimbali.
Kwa sasa mathalani zao letu la korosho limeyumba, huu ulikuwa ni muda muafaka wa raisi Magufuli kuongea na wakuu wenzie wenye viwanda na masoko ya korosho kuona Tanzania inaweza kunufaika vipi na fursa zilizoko kwao.
Lakini pia nchi yetu inahitaji uwekezaji mbalimbali wa mitaji, hii ni nafasi ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa ambao hufunga safari kipindi hiki ili waweze kukutana na viongozi wa nchi mbalimbali kuzungumza masuala ya uwekezaji.
Pia kwa kuwa nchi yetu ina utalii basi hiyo pia ni fursa nzuri ya kuongea na wadau wa utalii na kuona namna gani tunaweza kuleta watalii wengi zaidi.
Swali langu ni kwamba Miaka minne Mheshimiwa Raisi hajaenda kukutana na Kiongozi yeyote wa Taifa kubwa na wala hajahudhuria kikao chochote cha UN General assembly.
Je safari hii itaenda?