Je, Rais Magufuli anatoa ahadi hewa kwa wafanyakazi? Mwaka huu haondoki madarakani? Anajiamini vipi kama atabaki??

Natamani sana kukuelimisha juu ya uamzi wa kutopiga kura...

Huoni kuwa hiyo ni njia ya moja kwa moja ya kumfanya abaki madarakani, tena njia anayoipenda sana. Rejea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kutopiga kura ni kumchagua yeye.

Kupiga kura na kushiriki kuhakikisha kura yako haipotei ndiyo njia pekee ya uhakika wa kumwondoa kama hutaki aendelee.
Bonge la point mkuu, tupige kura nyingi za kumkataa
 
kwenye ilaniya ccm ya mwaka 2015 hakukuwa na ahadi ya kuongeza mishahara.infact mishahara imeongezwa kimya kimya, uliza watumishi wa umma sehemu kama TRA,nk watakuambia.
 
Natamani sana kukuelimisha juu ya uamzi wa kutopiga kura...

Huoni kuwa hiyo ni njia ya moja kwa moja ya kumfanya abaki madarakani, tena njia anayoipenda sana. Rejea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kutopiga kura ni kumchagua yeye.

Kupiga kura na kushiriki kuhakikisha kura yako haipotei ndiyo njia pekee ya uhakika wa kumwondoa kama hutaki aendelee.
Mugabe,Mobutu,n.k.

Kumbuka kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtu akiwa Kagera aliwahi kusema "KWENYE KAMPENI ZAKE HAKUAHIDI KULETA TETEMEKO"
Kweli watz wanaonekana ni wapumbavu sana yani...............
 
Tuombee tu hiyo 2025 iwapo Mungu atamjalia uzima na afya tele, basi aiheshimu Katiba na hivyo aondoke madarakani kwa hiyari yake na kwa mujibu wa Katiba na Sheria baada ya kutumikia vipindi viwili mfululizo.

Maana anaogopesha sana kwa kiasi kikubwa! Haonekani kutoka moyoni mwake kama anatamani kuishi maisha nje ya Urais hata siku moja! Ingawa mara nyingi ametamka kwa mdomo kama huo Urais ni kazi ngumu. Ila kiukweli anaupenda! Na zaidi ni kule kinyenyekewa na kusujudiwa na wale wapambe wake wanafiki na wachumia tumbo.

Anachokisema leo, sicho anachokitenda kesho. Akiamua tu kung'ang'ania madaraka kama wapambe wake wanavyo mpamba basi tujiandae kulima kwa kutumia meno. Hakika tutapoteana. Labda akubali kubadilika.
 
Natamani sana kukuelimisha juu ya
uamzi wa kutopiga kura...
Huoni kuwa hiyo ni njia ya moja kwa
moja ya kumfanya abaki madarakani, tena njia anayoipenda sana. Rejea
uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kutopiga kura ni kumchagua yeye.

Kupiga kura na kushiriki kuhakikisha
kura yako haipotei ndiyo njia pekee ya
uhakika wa kumwondoa kama hutaki
aendelee.
Haina haja ya kunielimisha mkuu natambua haki na wajibu wangu kidemokrasia..shida inakuja haki yangu itaminywa tu hata nifanyeje maana tume yake,Polisi wanamsikikiza yeye..huoni kama kashashinda hadi hapo.???.. sasa ya nini nikapate corona kwenye foleni za kupiga kura kumchagua mtu aliyejichagua mwenyewe?
 
kwenye ilaniya ccm ya mwaka 2015 hakukuwa na ahadi ya kuongeza mishahara.infact mishahara imeongezwa kimya kimya, uliza watumishi wa umma sehemu kama TRA,nk watakuambia.

Suala la mishahara ya wafanyakazi na ilani ya uchaguzi Ni vitu viwili tofauti...

Wapo wanao neemeka awamu hii Askari wanapandishiwa vyeo na mishahara Kama kawaida... Walimu wakuu wameongezewa posho ya majukumu... Polisi nao posho yao ipo Kama kawaida... Huu Ni ubaguzi.
 
Rais magufuli tangu aingie madarakani hajawahi kuongeza mshahara kwa watumishi wa umma.

Mei mosi 2016 alisema bado anashughulikia vyeti feki

Mei mosi 2017 akaahidi kuwa atapandisha mshahara.

Mei mosi 2018 TUCTA wakamkumbusha kuhusu ahadi ya 2017 akawajibu kuwa walimnukuu vibaya. Anatekeleza miradi mikubwa kwanza.

Mei mosi 2019 MEI MOSI 2019: Rais Magufuli asisitiza kuwa ataongeza mishahara akikaribia kuondoka madarakani. Awataka wafanyakazi kuwa na subira - JamiiForums

Mei mosi 2020 ??? Corona??? Hajakaribia kutoja madarakani?

Mei mosi 2021.!?.!?
Kwani TUCTA bado ipo?
 
Haina haja ya kunielimisha mkuu natambua haki na wajibu wangu kidemokrasia..shida inakuja haki yangu itaminywa tu hata nifanyeje maana tume yake,Polisi wanamsikikiza yeye..huoni kama kashashinda hadi hapo.???.. sasa ya nini nikapate corona kwenye foleni za kupiga kura kumchagua mtu aliyejichagua mwenyewe?
Tukiweka pembeni woga wa coronavirus, na hata huko kupoteza muda kukaa foleni; je isingesaidia kwako kujua kwamba kura yako ya kumkataa itakuwa ni ushahidi usiofutika hata kama atalazimisha kuwepo madarakani kwa njia hizo ulizozitaja? Na je, huwezi kuona kwamba kura yako na za wengi wengine waliomkataa zinaweza kuwa kichocheo cha kumwondoa kwa njia nyingine hapo akilazimisha kubaki?

Kwa nini uwanyime haki ya kuutumia ushahidi wa kura yako waTanzania wenzako ambao watapenda kuutumia ushahidi huo!
 
Kuna wapuuzi 2020 watamchagua tena huyohuyo..aisee Mimi kama hajatokea mbadala wake anayeweza kufit urais wa Tanzania either kutoka CCM au WAPINZANI ni bora nisipige kura tu inatosha sasa sioni hata anapotupeleka
PIGA KURA TIMIZA WAJIBU WAKO
 
Back
Top Bottom