Je, Rais Magufuli anachelewesha Baraza la Mawaziri sababu Serikali haina pesa?

Toka huu uzi tumeona matendo mengi ya serikali yanayothiirisha kwamba ni kweli. Jana Magufuli kafuta sherehe za uhuru, na mpaka leo hajateua Baraza la Mawaziri. Tumeona pia jinsi serikali ina mpango wa kuhakiki wastaafu wote kqenye pensheni, walikua wapi siku zote? Wafanyabiashara mtakoma miaka hii mitano

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Ngoja waonje joto ya jiwe. Yule waziri wa kikootoo kipya atakuwa anashinda kwa fundi sasa.
 
Katika hafla ya kumwapisha Waziri Mkuu Majaliwa na Mawaziri Mpango na Kabudi, Magufuli alisema wazi kuwa hana haraka ya kuteua baraza la mawaziri. Sababu yake ilikua ni uwingi wa wabunge wa CCM ambao unampa muda mwingi wa kufikiri na kuchambua yupi anayefaa.

Leo wakati Mwinyi wakati anatangaza mawaziri wake alisema baraza hilo halitakua na manaibu mawaziri ili kubana matumizi ya serikali, akaongeza atawateua hapo itakapohitajika. Kwa jicho la haraka hili linaweza kuonekana kama jambo jema, kwani manaibu mawaziri huwa wanaonekana kama hawana kazi ya maana sana.

Ila, kwa jicho la upana, huu uamuzi unaashiria kuwwa kuna ukata wa fedha za kuendesha serikali maana Mnaibu Mawaziri ni takwa la sheria na wanatambiliwa na katiba ya Zanzibar kifungu namba 47 na 48. Kwa namna hii Mwinyi anavunja katiba. Hatakama nia ni kubana matumzii, utaratibu na sheria za nchi zifuatwe.

Uwamuzi huu Mwinyi umenionyesha kuwa hata kwenye serikali ya Muungano, kuna ukata wa fedha. Sio siri kuwa CCM ilitumia nguvu na mali nyingi sana za serikali katika uchaguzi huu (pengine kupita chaguzi zozote zilizopita). Ukiongezea na kuwa serikali, kwa mara ya kwanza imetumia billion 260 kugharamia uchaguzi, utagundua kuna tatizo kubwa la kifedha serikalini tusiloambiwa.

Pia, jumuiya za kimataifa zinafikiria kupunguza misaada yao kwa kutofurahishwa na jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa. Ndio maana kwenye hotuba ya Magufuli aligusia sana sekta binafsi na uwekezaji. Anajua huko ndipo atategemea pesa nyingi miaka hii mitano. Na ofisi ya uwekezaji kaiweka kwenye Ofisi ya Rais aisimamie mwenyewe.

Naona wafanya biashara wanakenua na kufurahia hawajui linalokuja. Miaka mitano iliyopita tumeona jinsi walivyopewa makesi ua uhujumu uchumi na kuwekwa ndani ili baadae wanunue uhuru wao through "plea deals".

Mpango na Kabudi wameteuliwa wa kwanza mahususi ili wawatongoze mabeberu an kuwaomba fedha zao maana hali ni mbaya. Tumeshaona mawaziri walioita kama Kalemani wakizindua miradi. Je wanafanya volunteering? Wote tunajua baraza la mawaziri ni expensive. Magufuli anachelewesha kulitangaza ili asave ela hizo. Tutubirie na sherehe za uhuru zifutwe tena mwaka huu.
naona umeingia joto unataka upandwe kama lissu anavyopandwa na beberu amsterdam kwa mshahara wa eti "kumpeleka rais halali ndugu kayafa jiwe icc"

Mtapandwa mno ndugu zangu
Mimi binafsi siwezi kujipendekeza kwa beberu kama nyie timu pombe wazee wa dagi😂😂

#jr
 
Back
Top Bottom