Kwa hali inavyoendelea kwa sasa naona kufariki kwa mwendazake kuna sababu zipo nyuma na haikuwa mapenzi ya Mungu naomba msininukuu vibaya ni maoni yangu ili na nyinyi mniambie kama ninawaza vibaya.

Mbona ule mwelekeo tuliokua nao kwa asilimia 80% taifa lilikua na matumaini ya baadae amabyo tuliona yana tija halafu ghafla Viongozi wamegeuka kama hawakuwepo kama sio wao.

Kuna Agenda ipo nyuma, kuna mambo yanasukumwa mbona kama tushazama kwenye mtego ila viongozi wanajua ila sisi bado hatujaelewa.

Tutaelewa kwa vitendo.

Et leo bandari imekua nzuri ghafla au namba 4 ndio wameshika usukani wanatuendesha bila shaka kuna jambo lipoo hatujui ila muda utadhilisha bora tupigwe chanjo sasa kuliko hili la bwagamoyo ni dhahili hii bandari yetu itasimama ili hiyo ifanye kazi .

Bado muda utasema JPM hakua mjinga kusema mtanikumbuka kuna jambo aliona hata kama ametupiga na tukapigika ila wacha nisubiri nazidi kupata mshtuko na kinacho endelea.

Nateseka na nina sononeka kwa hizi dalili tayari adui kashika penyewe kwa hizi ishara.

MUNGU IBARIKI TANZANIA .

NAWASILISHA.
 
Hali ni tete kupita maelezo, Kuna viongozi wengine ni kama vile mijusi imekurupushwa kutoka kwenye mapango!
 
Wafuasi watiifi wa jiwe bado slow*2 na Barushi tuu hawa nao wakienda tofauti duuuh
 
Habari zenu wakuu poleni Sana na majukumu ya kulijenga hili Taifa .

Kwa haya Mambo yanayoendelea katika kila Kona ya Tanzania nachelea kusema kuna watu inawezekana kabisa wamehusika na kumzima mkuu wa nchi...
Ati nini?(kwa sauti ya yule mnywaji wa taifa Pierre Liquid)
 
kama kuna ufisadi na mambo yetu yanaenda hakuna shida Jambo ambalo wengi tunazingatia ni Kuwa vyuma vilikaza mno katika awamu ya tano.
 
Kwa hali inavyoendelea kwa sasa naona kufariki kwa mwendazake kuna sababu zipo nyuma na haikuwa mapenzi ya Mungu naomba msininukuu vibaya ni maoni yangu ili na nyinyi mniambie kama ninawaza vibaya...
Meko kajimaliza mwenyewe, hamna mkon wa mtu wewe unajua una pacemaker kwenye mwoyo arafu unadharau Corona.
 
Hapa ndo ujue wanasiasa kazi kujali matumbo yao... ni bendera fuata upepo...nchi hata iingie kwenye hasara gani yenyewe hayajali mradi wanapata posho yao... watasapoti hata kama ni white elephant project mradi wanajua wanachofaidia. Wanasiasa ndo wanaongoza kwa kukosa uzalendo...tulipigwa, tukapigwa, na sasa tunaelekea kupigwa tena...hakuna namna.
 
Asilimia 80 ya watanzania walikuwa na Imani na JPM alipoingia madarakani, jamaa alivuruga mwenyewe .... Aliamua kuchanja njia yake tuuu, ni kweli kuna indicator wamemtoa roho, Ila alivurugaaaaaaaaa..sina hamu na mwendazake japo nilikuwa fan wake mkubwa by 2015
 
Mkuu! Hao asilimia 80 unaosema wewe ni wapi? Humu JF umewahi kufanya research ukagundua watu wengi walikua na maoni gani?

Yaani kisiasa mlikua mnaona anafanya vizuri ila kwaakili tu ya kiwango changarawe unaona alikua anatupeleka shimoni.. Kulikua na Indicators nyingi kuonyesha mwendazake anatwanga maji kwenye kinu, na ili kuficha na kulinda madudu yake akataka atawale yeye mpaka Siku Tanzania inafikia Mwisho!

Alichofanikiwa yeye ni kutugawa !! Kuna uovu mwingi sana utavumbuliwa hivi karibuni, chakufanya wewe nunua popcorn tu filamu inakuja!
 
Back
Top Bottom