Je Rais Magufuli alieleweka aliposema kuwa wasaidizi wake hawamuelewi anachotaka?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Wakati wa kumuapisha Waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugora, alieleza kwa kirefu namna ambavyo baadhi ya wasaidizi wake anaowateua namna ambavyo hawamuelewi anachokitaka katika Utendaji wao.

Hakufafanua zaidi ni nini hiko anachokitaka kutoka kwa wasaidizi wake

Lakini kutokana na teuzi za Jana, nadhani wengi watakuwa wamemuelewa......

Amemteua Ali Hapi na kumpandisha cheo kuwa RC wa Iringa

Tukumbuke pia kuwa huyu Ali Hapi aliwahi kumweka ndani kwa Masaa 48, mbunge wa kuchaguliwa na wananchi, mbunge wa Kawe, kwa tiketi ya Chadema, Halima Mzee

Tusisahau pia kuwa wilaya yake imefanya uchaguzi mdogo hivi karibuni, uchaguzi ambao umelalamikiwa sana na upinzani kuwa haukuwa huru na haki

Amemteua pia Jerry Muro kuwa DC mpya wa Arumeru

Tukumbuke kuwa huyu Jerry Muro anaaminika kuwa anapenda kutumia "mkono wa chuma" katika mambo yake mengi anayoyafanya

Tukumbuke pia huyo Jerry Muro anamrithi DC Alexander Mnyeti ambaye naye alipandishwa cheo na kuwa RC wa Manyara kutokana na kazi "nzuri" aliyofanya hapo Arumeru.

Tukumbuke kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Joshua Nassari aliwaonyesha waandishi wa habari clip ya video inayomwomyesha Mkuu huyo wa wilaya, Alexander Mnyeti, "akiwanunua" madiwani wa Chadema

Je uteuzi wa jana wa Mheshimiwa Rais unamaanisha nini?

Kwa jinsi nilivyouelewa Mimi ni kuwa uteuzi huo "unawahamasisha" viongozi wa upinzani wahamie CCM, ambako kuna "uhakika" wa uteuzi wa chap chap katika nafasi za Uongozi wa Umma!

Na wale walioko ndani ya CCM, nilichojifunza ni kuwa wateule hao wa Rais, hususani katika maeneo ambayo yana mbunge na madiwani wengi wa upinzani, wamechaguliwa wale ambao wanaweza kuutumia vyema "mkono wa chuma"

Je "mkono wa chuma" ndicho alichomaanisha Mheshimiwa Rais aliposema kuwa wasaidizi wake wengi hawamuelewi anataka nini katika serikali yake??
 
Last edited:
Kweli kabisa Mkuu..
Hata uteuzi wa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe una akisi kabisa Mheshimiwa anataka watendaji wa namna gani.
 
Kila kitu ukiuliza unasikia rais kakataa kisifanyike,

Si kweli,rais kakataa kisifanyike kwa njia za hovyo,ila anataka kifanyike kwa njia nzuri ambazo zinanufaisha nchi na watu wake.

Kiukweli biashara nyingi za usafirishaji bidhaa mbali mbali nje ya nchi haziko sawa,tatizo kubwa ni wasaidizi wa rais kushindwa kubadilisha taratibu za zamani ziwe za kisasa ili ziweze kinufaisha nchi na wananchi.

Watendaji wengi wa serikali ngazi ya maamuzi wamekaa kimya sana,kila kitu wanasubiri rais aseme au afanye!! Ajabu sana.

Mh,rais wa Tanzania nia yako ni nzuri sana,lakini watendaji wako hawajaweza kuielewa vilivyo nia yako,ikiwezekana kila week kutana na mawaziri,makatibu wakuu,na watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali ili uwaeleweshe lengo lako juu ya hii nchi.!!

Ndugu watanzania tumsaidie rais wetu.
 
Tatizo Rais hajawaachia huru watendaji wake wafanye kwa bongo zao na ukikurupuka tu unatenguliwa
 
Back
Top Bottom