Je, Rais katumia Kanuni au Sheria ipi kuipa Dodoma hadhi ya Jiji ikiwa Bunge ndio lenye mamlaka hayo?

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Dodoma katika maadhimisho ya Sherehe ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ameipandisha Manispaa ya Dodoma na kuwa jiji la Dodoma. Aidha Mkurungenzi wa Manispaa hiyo amempandisha na kuwa Mkurungenzi wa jiji la Dodoma

Kwa mujibu wa Sheria na. 8 ya 2007 kifungu cha 5, mamlaka yenye uwezo wa kupandisha hadhi manispaa kuwa jiji ni Bunge

Je, kuna kifungu cha sheria au kanuni inayompa Rais wa Tanzania uwezo wa kufanya Manispaa kuwa Jiji?

IMG-20180426-WA0060.jpg
 
Kwenye muungano walichanganya udongo.. kwa saaa mwenye nchi anachanganya kila kitu... majengo, barabara, vivuko, madaraja, miji, mitaa, msaidizi wake anachanganya mpaka ndoa.... tuwe na subira tutafika
 
Katika kujibu hili tutafute kwanza idadi ya watanzania inaongezeka kwa asilimia ngapi kila mwaka.

Pia tutafute hesabu ya waliohamia dodoma tokea 2015 baada ya serikali kutangaza kuhamia dodoma wanaweza kuwa wangapi.

Baada ya kupata hesabu tuijumlishie kwenye hesabu halisi za sensa ya mwaka 2012
Serikali haikutangaza kuhamia Dodoma mwaka 2015, kuhamia Dodoma kulitangazwa na bingo miaka ya sabini chini ya sheria na si kama ulivyoaminishwa. Baada ya tangazo hill ofisi ya waziri mkuu ilikuwa ya kwanza kuhamia ikifuatiwa na bunge.
 
Katika kujibu hili tutafute kwanza idadi ya watanzania inaongezeka kwa asilimia ngapi kila mwaka.

Pia tutafute hesabu ya waliohamia dodoma tokea 2015 baada ya serikali kutangaza kuhamia dodoma wanaweza kuwa wangapi.

Baada ya kupata hesabu tuijumlishie kwenye hesabu halisi za sensa ya mwaka 2012
Usianze kuokoteza takwimu hapa, ni kinyume cha sheria za takwimu
 
Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Dodoma katika maadhimisho ya Sherehe ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ameipandisha Manispaa ya Dodoma na kuwa jiji la Dodoma. Aidha Mkurungenzi wa Manispaa hiyo amempandisha na kuwa Mkurungenzi wa jiji la Dodoma

Kwa mujibu wa Sheria na. 8 ya 2007 kifungu cha 5, mamlaka yenye uwezo wa kupandisha hadhi manispaa kuwa jiji ni Bunge si vinginevyo

Je, kuna kifungu cha sheria au kanuni inayompa Rais wa Tanzania uwezo wa kufanya Manispaa kuwa Jiji?

Soma vizuri jibu la mdau wa hapa chini, ukome kuposti vitu bila ushahidi
 
Katika kujibu hili tutafute kwanza idadi ya watanzania inaongezeka kwa asilimia ngapi kila mwaka.

Pia tutafute hesabu ya waliohamia dodoma tokea 2015 baada ya serikali kutangaza kuhamia dodoma wanaweza kuwa wangapi.

Baada ya kupata hesabu tuijumlishie kwenye hesabu halisi za sensa ya mwaka 2012
Tumia logarithmic function hapo mbona simple sana kutafuta idadi ya watu
 
Usianze kuokoteza takwimu hapa, ni kinyume cha sheria za takwimu
Ha ha ha, mkuu naona huyu kasahau kuwa ilipigwa marufuku kuokoteza na kutoa takwimu, ni shughuli ya mamlaka husika tu
 
Kulingana na sheria ya "Urban planning Act of 2007" mwenye mamlaka ya kubadili manispa kuwa jiji ni "National Assembly". Hii ni first schedule paragraph 5

Sheria yenyewe ni hii hapa
20180426_195601.jpg
 
Mkuu hivi wale madikteta mbali mbali duniani wakiwemo Mugabe, Bokassa na Mobutu maamuzi mbali mbali waliyoyafanya katika nchi zao ambayo hayakuwa na maslahi yoyote kwa Taifa wala kufuata katiba za nchi husika walitumia kanuni au sheria zipi Mkuu!? Kumbuka tuna Bunge uchwara kitengo cha magogoni.

Back
Top Bottom