Je, Rais aliona Ripoti ya CAG kabla ya safari ya Brazil?

Rais wako huwa hana kasumba ya kusoma, hata akipelekewa hoja ya kwamba ajiudhuru anaweza akasaini tu! Huyu jamaa analiingiza taifa katika matatizo makubwa tu, yuko kama watemi wa zamani waliokuwa wakisaini mikataba wakati hawajui kusoma wala kuandika.
Kumbuka mswada wa katiba aliousaini .....
 
Hamjamsoma raisi wenu naona, kasoma report ya mkaguzi na kwakuwa kagundua maovu, kaamua isomwe bungeni kwanza ili watanzania waione kisha hata akisema anamfukuza flani sababu ya kutosha iwepo ifahamike ili mtu asiseme kaonewa...hakurupuki kumfukuza mtu anatafuta sababu nzuri na nzito then unayefukuzwa utajaji mwenyewe kama umeonewa au la...
 
Aliiona ila kuisoma?Sidhani , ila aliipokea kwa mbwembwe na kamera nyingi, Mashaka yangu ni kuilewa, anaweza soma bila kuelewa, Na haraka za Kutalii si ingempotezea muda.
 
Katika sifa haci za JK moja ni kutokuwa na tabia ya kusoma documents muhimu anazoletewa.. Ana kawaida ya kuwaamini wasaidizi wake wazipitie na kutoa recommendations ili aweze kusaini maamuzi.. Na hili lilianza kutokea toka mwanzoni mwa utawala wake.. Hata habari nyeti toka kwa usalama wa taifa hakuwa anazisoma.. Na hili ndilo lililosababisha kwa kiaci kikubwa tufike hapa tulipofika.. Maana wasaidizi wako kimaslahi zaidi na wanajipigia ndefu zaidi.. Hata JK anapokuja kugundua anashindwa kutoa maamuzi kwa maana hana usafi huo..!
 
Back
Top Bottom