seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
184
1,000
Hawa ni Wasomi kutoka Stanford University na mungine Harvard University

Prof Lipumba, Huyu ameishi Stanford University na Kufundisha hapo, Gharama za kusoma chuo hicho ni zaidi ya dollar za kimarekani 55,000 kwa mwaka mmoja sawa na pesa za kitanzania zaidi ya Milioni 120 kwa mwaka mmoja.

Kupata nafasi Stanford ni kazi ngumu mpaka sasa, Kwa watu wote wanaoomba na ambao wanarekodi nzuri za kitaaluma ni asilimia 8‰ tu wanapata nafasi hizo Katika walioomba kutokana na mchujo mkali . Hiki ni chuo ambacho mpangilio wa" Internet " yaani architecture of Internet ulivumbuliwa, Deoxynubleic Acid(DNA) ilivumbuliwa hapa Stanford university

Prof Lipumba, Huyu ni nguli na ameondoka hapo Stanford University moja kati ya wanafunzi bora wa Economics

Je, Prof Lipumba amelisaidia Taifa? Kuna umuhimu gani wa kupeleka watu nje Halafu hawatoi mchango kwa kile walichojifunza

Je, Siasa ndio inarudisha nyuma mchango wa Wasomi hawa kama Prof Lipumba?

Kwanini tunapoteza muda kupitia mitaala ya elimu kama baadhi ya watu waliosoma vyuo bora wanaitwa wasaliti ndani ya Taifa lao

Mheshimiwa, Andrew Chenge. Huyu ni nguli wa sheria na msomi toka Harvard University

Andrew Chenge amepata umaarufu sio kwa mambo mazuri bali kwa kutumia akili zake na Penseli kufinyanga mambo na kujitapa kuwa, Yeye havunji wala haibi kwa nguvu bali anatumia Penseli na Pen tu kukwapua mali.

Mvumbuzi wa Facebook alipita hapa Harvard na akaacha chuo hapa baada ya kupata wazo akiwa hapo.

Leo Serikali inajadili habari za kubadili mitaala ya shule iwe ya kisasa kama Marekani na uingereza wakati watu waliosoma huko hatuoni faida yake

Je, Chenge ametuangusha kama Taifa au Siasa ndio zinaharibu?

Je, mitaala ikifanyiwa marekebisho hivyo hakutakuwa tena na watu kukanyaga katiba kama wale wabunge feki 19 wa Chadema bungeni.

Je, mitaala ikafanyiwa marekebisho watu wataacha kuamini nyungu na kuamini Sayansi, Mbona Wasomi hao ndio walikuwa wa kwanza kujenga chumba cha kupiga nyungu hospitali kuu ya Taifa.
 

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,613
2,000
Nathani mfumo wa nchi na Sheria zipo ovyo so watu Kama Chenge wanatumia mwanya huo kutuchezea lakini kama Sheria zetu nzuri na siasa zikawa na mda maalumu Basi hawa wasomi wangeweza kutusaidia vizuri sana
 

dem boy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
4,213
2,000
Msukuma akisema hawa wanaojiita wasomi hawana faida wanamuona ana wivu eti kisa yeye hakusoma...nijuavyo mimi ukweli tu ndio mchungu.
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,046
2,000
Tatizo sio watu, tatizo kuipa siasa HADHI KUBWA kuliko Elimu au kitu chochote kile kingine. Pia ubovu wa KATIBA yetu, kwa katiba hii hata aje Biden hatutoboi kamwe.

Kubadilisha MITAALA ya Elimu bila kubadilisha Katiba ni kazi bure. THIS I GUARANTEE YOU.

Ova
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,093
2,000
Nathani mfumo wa nchi na Sheria zipo ovyo so watu Kama Chenge wanatumia mwanya huo kutuchezea lakini kama Sheria zetu nzuri na siasa zikawa na mda maalumu Basi hawa wasomi wangeweza kutusaidia vizuri sana
Mtu aliyewahi kuwa AG anasubiri sheria ziwe nzuri wakati alikuwa na mamlaka ya kuzifanya ziwe nzuri ?
 

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,613
2,000
Mtu aliyewahi kuwa AG anasubiri sheria ziwe nzuri wakati alikuwa na mamlaka ya kuzifanya ziwe nzuri ?
Sasa hata Kama ni wewe mkuu umepewa kibarua ulime shamba unaweza kumchagulia mwenye shamba mbegu za kupanda?
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,168
2,000
Kabla ya kurusha dongo kwa hao Wasomi, jiulize Wewe kwa chochote ulichonacho jee Umelisaidia Taifa lako?, Wewe unadhan Ile US unayoiona unadhan ni mchango wa Wasomi peke yao?

Kila Mtanzania anapaswa kwa nafasi na Maarifa yake kwa kadri alivyojaaliwa kusaidia Taifa lake kwa nguvu na Maarifa yote bila ya kujali wengine wanasaidia au kuhujumu Taifa lao

Hata huko US wapo wengi tu wanahujumu Taifa lao kwa maslahi binafsi

Hata ukinywa Maji na kutupa chupa mita moja kutoka ilipo kifaa cha kukusanyia Uchafu ni Hujuma dhidi ya Taifa lako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom