Je, Polisi ndio wabambikaji kesi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,794
Hii ni mada hojaji... Ni mada ulizo... Ni mada swali... Tushirikiane kupata majibu..!!!

Hapo kabla ya awamu hii. Huko nyuma, kesi mbaya ilikuwa mauaji.. Kesi hii haina dhamana... Na watuhumiwa wakubwa wa ubambikaji(kusingiziwa mashtaka ya uongo) walikuwa ni police... Kwamba kama una bifu nao ama wamekukamata kwenye patrol zao na ukawavimbia sana, ukifikishwa selo unapewa kesi ya kichwa yaani ya mauaji.

Hii ilitokana kuwa na kesi nyingi za mauaji zisizo na watuhumiwa hivyo na kuwa na majalada open ya hizo kesi. Sambamba na hilo ubambikaji mwingine ukawa kwenye madawa ya kulevya.

Watu walichomekewa sana kete na misokoto ya bhangi, lakini uzuri wake wakati ule nyingi ya kesi hizi hazikuwa za kisiasa bali kwa sehemu kubwa mabifu ya mitaani huko kwenye jamii

Mambo yalianza kubadilika mwaka juzi kwenye juhudi za kusafisha uozo mkubwa uliokuwepo serikalini na taasisi zake.. Watu walikuwa wamepiga ndefu za kueleweka na wengi walipiga kupitia kalamu.. Na kwa sehemu kubwa walikuwa ni wafanyakazi serikalini wakishirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu

Asili ya uhujumu uchumi ni kampeni ya mwaka 1984 iliyofanywa na hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa waziri mkuu kipindi hicho.. Kampeni iliyopata baraka zote za Hayati Mwl. J. K. Nyerere.

Kampeni ile iliwalenga wafanyabiashara.. Pesa ziliadimika mtaani na bank.. Bidhaa pia ziliadimika madukani. Serikali ikagundua kuwa ni mbinu ya wafabiashara kuficha bidhaa ziadimike kisha wauze kwa bei ya kuruka ili wapate faida kubwa.

Serikali kupitia waziri huyo Mkuu Sokoine ikatoa ultimatum pesa zisalimishwe bank na bidhaa zijazwe madukani.

Na kipindi kilichowekwa kikipita na ukafanyika msako ukakutwa na pesa nyingi ndani na bidhaa.. Kwanza utafilisiwa kisha utashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.. Kilichotokea kwa waliokuwepo wakati ule wanakijua vema

Awamu hii kama nilivyotangulia kusema katika juhudi zake za kusafisha uozo serikalini, ndio ikaja na hili la uhujumu uchumi.. Kosa ambalo halina dhamana lakini baadae likaongezeka na kosa lingine lisilokuwa na dhamana pia.. Kosa la kutakatisha fedha haramu

Makosa haya mawili yakatumiwa vibaya dhidi ya wale waliokuwa na mitazamo kinzani ya kisiasa.. Ikawa sasa sio kupewa kesi ya kichwa tena ama unga bali ni uhujumu uchumi na kutakatisha fedha haramu..
Utaratibu wa kufungua kesi unajulikana... Lazima awepo mshtaki na mshtakiwa.. Ni mara chache police kuwa mshtaki na ikitokea hivyo anafanya kwa niaba ya serikali

Tumewasikia live viongozi wa KISIASA majukwaani wakiongea bila kificho na bila woga kuwa ukikataa kutii maagizo yao ama ukikinzana nao kimtazamo watakupa kesi ya uhujumu uchumi ama kutakatisha fedha ukaozee jela kwakuwa kesi hizi hazina dhamana

Tunapowatuhumu polisi kubambika kesi tusiwasahau na hawa viongozi wa KISIASA waliotamka kwa uwazi mchana kweupe na bila woga!

Jr
 
Hakuna justification ya kuruhusu sheria mbaya itumike dhidi ya raia wako. Sheria ya kunyima watu dhamana kwa makosa yasio ya mauwaji(murder) au uhaini(treason) ni sheria mbaya na yahitaji kufanyiwa marekebisho. Lugha ya "kusafisha uozo" ni lugha ya uonevu inayotokana na vyombo husika kukimbia wajibu wake wa kufanya uchunguzi wa kina kabda ya kuwakamata watu kwa kisingizio kwamba wakiwa nje kwa dhamana eti wataingilia na pengine kuharibu upelelezi! Hii si sawa

Tena alivofanya Sokoine wakati huo ilikua ni uonevu zaidi maana hata sheria yenyewe ya uhujumu uchumi haikuwepo. Kilichofanyika ni watu kukamatwa na walipokua ndani ndio sheria ikaenda kutungwa na kupitishwa na Bunge!!! Ilikua ni precedence mbaya sana na ndio wenye mamlaka wanapita nayo siku hizi

Nakumbuka kuna case ya kubaka miezi kadhaa iliyopita mwendesha mashtaka alijitokeza hadharani kwenye media kua wakimkamata muhusika wanampiga "uhujumu and money laundering!"!!! Nilishangaa sana jamii ilivopokea hilo kwa furaha kwa sababu ni kweli alichokifanya huyo culprit ni kitu kibaya na uhalifu wenye kukera kila mtu.

Kwa maoni yangu lakini hata kama tuna hasira na muhalifu na uhalifu wa aina fulani ni lazima taratibu za kisheria zifuatwe kama zilivyo, vinginevyo tunatengeneza msingi mbaya wa sheria kupindishwa kwa matakawa ya baadhi ya watu. Mshana umekaa South na umeona kule jinsi sheria zinavyofutwa na hata kesi za mauji zina dhamana.

Najiuliza hivi pale kila mtu kuanzia viongozi wa kisiasa, mahakimu, majaji na wananchi kwa ujumla wanapolalamikia msongamano kwenye magereza ya Tanzania kweli hawajui chanzo ni nini?!!!
 
Hapa polisi amekuwa mbuzi Wa hitima.
Mbuzi Wa hitima anachinjwa mchana kweupe huku watu wakishangilia.

Unataka kuniambia akina Rugemalila,kabendera, Tito hao wote wamebambikiwa na polisi?

Polisi wamejichanganya wenyewe kutumika kisiasa,. Walitakiwa kusimama kwenye nafasi yao na bila kufungamana na upande wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sesten Zakazaka, Katika hilo pia kuna hili la kesi za kutakatisha fedha haramu... Ambalo kwa kumbukumbu zangu lilianzishwa na Marekani baada ya WTC kupigwa 9/11... Na baadae maharamia wa kisomali walipokuwa wakizikamata meli rasi ya Somalia na kudai kikomboleo kilichotumika baadae kuwekeza kwenye mambo mengine ikiwemo kufadhili ugaidi.

Hapa kwetu kama sikosei zile pesa za EPA na za matapeli wa madini kipindi kile na za rushwa kubwa kubwa bila kusahau madawa ya kulevya zote ziliwekwa kwenye kundi hilo.

Mshangao mkubwa ni awamu hii daktari aliyekamatwa na rushwa ya laki 5 akipewa kesi ya kutakatisha fedha haramu

Jr
 
Mambo mengi yatapata ufumbuzi siku tutakapoacha kuchanganya siasa na ujuzi
Hapa polisi amekuwa mbuzi Wa hitima.
Mbuzi Wa hitima anachinjwa mchana kweupe huku watu wakishangilia.

Unataka kuniambia akina Rugemalila,kabendera, Tito hao wote wamebambikiwa na polisi?

Polisi wamejichanganya wenyewe kutumika kisiasa,. Walitakiwa kusimama kwenye nafasi yao na bila kufungamana na upande wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
.
8a4f88bb94007f2e241f90a11f27be64.jpeg


Jr
 
Kwa mfano polisi kama Lazaro Mambosasa anaweza kutumiwa na Makonda atakavyo , atawafungulia kesi za uhujumu uchumi maadui zake kama ilivyokuwa kwa Manji na utekaji wa MO
 
Back
Top Bottom