Je, Polisi katika nchi za kiislam wana vikosi vya mbwa? Kama jibu ni ndio, kwanini wakati mbwa ni haramu?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania;

UTANGULIZI: Kwa msio nifahamu mimi Infantry Soldier ni mkristo ila ninafahamu fika ya kuwa uislamu si ugaidi na wala waislamu si magaidi bali wahalifu wachache hujificha katika kivuli cha uislamu ili kutenda ugaidi na kuua watu.

Uislamu ni dini safi tena ya watu waungwana sana inayohubiri amani na upendo kama ilivyo dini ya kikristo.

BACK TO THE TOPIC: Naomba kujibiwa swali langu kama kichwa cha thread hii kinavyouliza. Polisi kwenye nchi za kiislam kuna vikosi vya mbwa? Kama jibu ni ndio, ni kwanini wakati mbwa ni haram?

Naomba swali hili lisipinduliwe na kuwa mjadala wa kidini baina ya dini kuu mbili watu wakaanza kutukanana. Sisi watanzania bado ni wamoja licha ya tofauti zetu za kidini, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii. Asante Mungu.

Naomba kwa mwana JF anayejua kuhusu hili atuelimishe. Kama aliwahi kuishi katika nchi ambazo ni jamuhiri za kiislam itakuwa ni vema zaidi.

Thanks in advance.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mbwa uharam wake unakuja anapokunusa au kunusa vyombo unavyotumia.anapokunusa unapata 'NAJSI'katika najisi ni pamoja na damu,mkojo au kinyesi.hivyo mbwa ni najisi ikiwa wanawatumia au wanawafuga kidini hairuhusiwi!sababu huwez kuishi na mbwa ukaikwepa najisi.hivyo kama wanawatumia kwa muktadha wa usalama au ulinzi basi wameshanajisiwa km sio kulawitiwa
 
Mbwa mwenyewe sio haramu,kwa kumfuga,uharamu uko kwenye kula mbwa,umajimaji wa pua yake na mate yake.Mbwa anaruhusiwa katika uislamu,kuwindia,kutumika katika ulinzi.Ila umaji maji wa mbwa,kama pua,mate yake,ndio najisi,inatakiwa yakikugusa,uoshe na maji na mchanga,kuondoa najisi hiyo.Huwenda kwa ikawa sehemu hizo za mbwa zina bakiteria wabaya,na dawa yake ndio hiyo.Lakini mbwa kama mbwa mwenyewe,sio haramu,kumtumia katika uwindaji na ulinzi,akipewa mafunzo maalumu.
 
Mbwa uharam wake unakuja anapokunusa au kunusa vyombo unavyotumia.anapokunusa unapata 'NAJSI'katika najisi ni pamoja na damu,mkojo au kinyesi.hivyo mbwa ni najisi ikiwa wanawatumia au wanawafuga kidini hairuhusiwi!sababu huwez kuishi na mbwa ukaikwepa najisi.hivyo kama wanawatumia kwa muktadha wa usalama au ulinzi basi wameshanajisiwa km sio kulawitiwa
Kulawitiwa maana yake nini? maana ushaniacha hapa!
 
Mbwa uharam wake unakuja anapokunusa au kunusa vyombo unavyotumia.anapokunusa unapata 'NAJSI'katika najisi ni pamoja na damu,mkojo au kinyesi.hivyo mbwa ni najisi ikiwa wanawatumia au wanawafuga kidini hairuhusiwi!sababu huwez kuishi na mbwa ukaikwepa najisi.hivyo kama wanawatumia kwa muktadha wa usalama au ulinzi basi wameshanajisiwa km sio kulawitiwa
Well said mkuu nadhani atakua ameelewa
 
TUNATAMBUA KUWA NCHI ZA KIISLAMU PIA KUNA WASIO WAISLAM NA WAMEAJIRIWA KTK SEHEMU KAMA ZA VIKOSI, SIO KUWA POLISI WOTE WALIOKO NCHI ZA KIISLAMU NI WAISLAMU, KWA HIO AMBAO SI WAISLAMU NDIO WANAPEWA MAJUKUMU YA KUTUMIA MBWA KAMA KWA NJIA YA USALAMA, kwa sheria za kiislamu ITABAKI pale pale kuwa mbwa ana najis na najis ni haram, So sidhani kama kuna polisi ambae ni muislamu ktk nchi ya kiislam ambae anagusa mbwa na kama Yuko basi atakua anaenda kinyume na DINI yake ilivyosema kuwa mbwa ana najis
 
Mbwa ni najis na wapo katika majeshi ya police karibia nchi nyingi na za kiarabu zikiwemo ila Somalia kwa kweli sijaona lakini Emirates wapo na nchi zingine kwa ajili ya uhalifu na madawa ya kulevya kwani binadamu hawezi bila msaada wa mbwa
Airports nyingi wanawatumia mbwa
 
Kwa waislam mbwa ni haramu kama ukimgusa tu.kwahiyo unaweza kumgusa na ukaenda kujiosha kwa mujibu wa sheria na taratibu za dini.kumtumia kwa mambo mengine aijakatazwa.
 
Kweli ni haram lakini huruhusiwi kuishi nae ndani ni lazima awe nje
Mbwa wanaruhusiwa kwa mawindo pia
Na uchungaji
 
Mbwa uharam wake unakuja anapokunusa au kunusa vyombo unavyotumia.anapokunusa unapata 'NAJSI'katika najisi ni pamoja na damu,mkojo au kinyesi.hivyo mbwa ni najisi ikiwa wanawatumia au wanawafuga kidini hairuhusiwi!sababu huwez kuishi na mbwa ukaikwepa najisi.hivyo kama wanawatumia kwa muktadha wa usalama au ulinzi basi wameshanajisiwa km sio kulawitiwa
Hilo neno la mwisho limeingiaje kwenye maelezo yako??
 
Uharamu wa Mbwa unakuja kwenye mate yake kwa maana ndio najisi lakini hajakatazwa mtu kumfuga kwa ulinzi au kwa kupenda tu wanyama.
Na najisi yake ni kwamba unaosha pale alipogusa maisha yanaendelea.

Ndio ninavyojua.
 
View attachment 765636
Habari za wakati huu ndugu kaka na dada zangu.

Naomba kujibiwa swali langu kama kichwa cha thread hii kinavyouliza.

Naomba swali hili lisipinduliwe na kuwa mjadala wa kidini baina ya dini kuu mbili watu wakaanza kutukanana. Sisi watanzania bado ni wamoja licha ya tofauti zetu za kidini, kiuchumi na hata kijamii. Asante Mungu.

Naomba kwa mwana JF anayejua kuhusu hili atuelimishe. Kama aliwahi kuishi katika nchi ambazo ni jamuhiri za kiislam itakuwa ni vema zaidi.

Thanks in advance.
Mkuu
Nenda kasome Qur'an 5:4
Ni matarajio yangu kuwa utapata mwanga kidogo
Screenshot_20180504-182322.jpg
 
Watoa majibu ya hili swali lazima wawe wamebobea katika maskhala ya misingi ya kidini ya kiislamu wenyewe ndugu zetu wanaita fiqh (Islamic jurisprudence) , ni sawa mtu akuulize swali " tuamini nini kati ya conventional current na electronic current flow?" hapa kama mtu haujabobea katika maskhala ya kiumeme hutaweza kujibu ili swali badali yake utajibu blur blur, swali kama hili litahitaji kujibiwa na mtu aliye bobea katika maskhala ya ki umeme, na katika maswali hivyo hivyo majibu lazima yajibiwe na wataalamu wa mambo husika.
 
Back
Top Bottom