Je, Pinda ameshajibu barua ya Umoja wa Wanafunzi Elimu ya Juu Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Pinda ameshajibu barua ya Umoja wa Wanafunzi Elimu ya Juu Tanzania?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Magobe T, Oct 6, 2010.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana JF, wiki moja iliyopita EA TV walikuwa na kipindi juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na mada iliyokuwa inajadiliwa ilihusu jinsi gani Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) watakavyopiga kura wakati watakuwa likizo kwa vile watafungua vyuo baada ya uchaguzi mkuu. Walisema ni agizo lililotolewa na serikali likidai ingekuwa gharama kubwa kwa serikali kama vyuo vingefunguliwa kabla ya kupiga kura.

  Walisema kwa vile ratiba ya vyuo huwa inatolewa muda mrefu, mamlaka husika zingeweza kuweka utaratibu mzuri ili wanavyuo hao wajiandikishe kwenye vituo vyao wakiwa likizo au vyuoni. Walidai pia kuwa utaratibu uliowekwa mwaka huu unaonesha una lengo la kuwanyima hao wanavyuo haki yao ya kupiga kura. Pamoja na hayo, walikuwa na matumaini kuwa Waziri Mkuu atawasikiliza na kuwaeleza namna gani watakavyoshiriki uchaguzi mkuu wakiwa likizo. Je, kuna mwenye taarifa nzuri kuhusu hili: yaani, kama Waziri Mkuu amewajibu na ni kitu gani kinaendelea?
   
Loading...