Je, pikipiki zilizotolewa na serikali kwa maafisa Ugani na maafisa elimu kata nchi nzima nao watauziwa kwa mkopo?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,802
21,398
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amependekeza Serikali kubadili utaratibu uliopo ili kuwakopesha magari watumishi wa umma wenye hadhi ya kuwa na gari la Serikali ikiwa ni mkakati wa kubana na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima.

Amesema kuwa utaratibu huo alioupendekeza utasaitia kuokoa gharama za matumizi ya magari kwa zaidi ya Sh500 bilioni.

Dk Mwigulu amesema hayo bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.

Amesema kuwa utaratibu huo mpya ukianzishwa utapunguza gharama zinazotokana na magari hayo pamoja na usimamizi mzuri.

“Kwa upande wa hatua za muda wa kati na muda mrefu, napendekeza Serikali kubadili kabisa utaratibu uliopo kwa kuwakopesha magari watumishi wenye hadhi ya kuwa na gari la Serikali wawe na magari yao wenyewe, wafanye matengenezo wenyewe, wanunue vipuri wenyewe na masuala ya mafuta yaangaliwe kwa utaratibu utakaoonekana unafaa” amesema Dk Mwigulu ambaye anasoma bajeti bungeni.

Amesema kuwa “Kwa sasa Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mitambo 373 na inatumia zaidi ya Sh558 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa magari, ununuzi wa mafuta ya uendeshaji, ununuzi wa vipuri na matengenezo ambapo kwa sasa ni zaidi ya shilingi bilioni 500” amesema nakuongeza.

Ukiondoa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Mahakama, upande wa Serikali wabaki viongozi wakuu wa Wizara, Mashirika, wakala, mikoa, wilaya na Miradi ambao wasimamizi watakuwa eneo la mradi (site) muda mwingi ambapo kwenye makundi haya hawatazidi watano kwa taasisi, wengine wote wenye stahili ya gari la Serikali wakopeshwe, watumie magari yao, watasimamia vizuri matumizi, matengenezo, mafuta na vipuri” amesema.

Dk Mwigulu amesema kuwa hali hiyo pia itaondoa utaratibu uliopo sasa ambapo dereva anasafiri na gari lakini bosi wake anasafiri na ndege.

“Tutaondoa utaratibu uliozoeleka, dereva na gari anapitishwa chini, bosi anapanda ndege mpaka Mwanza au Mbeya kutoka Dar es Salaam na kurudi hivyo hivyo. Kuna utafiti wa siri ulifanywa, kwa siku moja yalibainika magari ya Serikali yaliyotoka Dodoma kwenda Dar es Salaam yalikuwa 132, na yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam yakipishana kuja Dodoma yalikuwa 76, na mengine 8 yalikuwa yamepinduka. Je kwa mwezi ni gharama kiasi gani?” amehoji Waziri huyo wa Fedha na Mipango.

Amesema kuwa utaratibu huo alioupendekeza utasaitia kuokoa gharama za matumizi ya magari.

“Utaratibu huo gharama za matumizi ya magari serikalini zitakuwa takribani shilingi 50,508,038,843.09. Zaidi ya shilingi billion 500 zitaokolewa na kuelekezwa kwenye ununuzi wa dawa muhimu hospitalini, kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati, na kutekeleza miradi ya maendeleo. Tumezidi kupenda ubosi, magari 17 makubwa kwa kila mtu serikalini, matumizi ya starehe, wakati katika nchi yetu bado kuna watu wanapata shida kupata mlo mmoja”.

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania
ameielekeza Wizara ya Fedha na Mipango ifanyie kazi jambo hili la kuelekeza fedha kwenye matumizi ya msingi tu”. Amesema Dk Mwigulu
 
Mbona hizo pikipiki waliambiwa wanatumia miaka 2 zinakuwa zao
 
Mbona hizo pikipiki waliambiwa wanatumia miaka 2 zinakuwa zao
Bado serikali haijatoa maelezo ila ni muhimu serikali Ilaria tamko Ili waliopewa waanze kurejesha malipo ya hizo pikipiki
 
Back
Top Bottom