Mzee Madoshi
Senior Member
- Feb 16, 2011
- 134
- 41
Ippmedia imetoa picha ya wananchi wa KIJIJI MWAMASHIMBA waliofurika kisawasawa katika mikutano ya CUF na CDM jana, na kwa sababu tumekuwa tukitumia picha kama kielelezo kimoja wapo cha ushindi picha hizi zinatoa changamoto muhimu sana. Tuchukulie kijiji hiki kama kipimo cha nani atapata kura nyingi kati ya CUF na CDM, Je ni rahisi kutoa uamuzi nani atashinda kwa kuangalia picha hizi?, Je wingi wa watu ni kipimo sahihi cha kumtambua mshindi? Tatu, kama CUF/CDM watazoa kura za watu wote hawa CCM wana kitu kweli hapa ikizingatia kijiji hiki ndio Kafumu amekuwa akijivunia kuwa mlezi wa vijana wao.
Nawasilisha