Je, Peter Msigwa aliwezaje kumkosoa ndugu yake Rais Magufuli?

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
243
1,000
Peter Msigwa ulisimamia haki, Hukuogopa vikao vya familia na undugu wako na Hayati Rais Magufuli.

Moja kati ya watu ambao wangeamua kuwa na kiburi basi ni Peter Msigwa angeweza fanya kiburi. Na hata angehamia CCM ndugu yake Magufuli angekupitisha Iringa mjini bila kupingwa.

Hata ndugu yako Gerson Msigwa wa Ikulu pale alipojifanya familia imekaa kikao Ikulu na kuamua wewe wakuchangie pesa utoke mahabusu, ulisimamia haki.

Ingawa Rais Magufuli ndie aliyekuwa mwenyekiti wa vikao vyenu vya undugu hukumuogopa kusema Bungeni hata mtaani.

Hata pale Magufuli alipotaka kuweka coverage kwa kukuchangia pesa ya dhamana bado ulikataa kupanda gari za CCM alizokuja nazo Humprey Polepole.

Ni watu wachache sana Tanzania wanaweza kataa undugu na mtu ambaye ni Rais wa nchi.

Hongera Peter Msigwa, Uliweza kutofautisha mambo ya undugu wako na Magufuli na kuamua kusimamia haki.

Hukusita kumpa Magufuli ukweli wake mchungu bila hofu ya wanafamilia na undugu wenu.
 

Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
2,557
2,000
Navyojua
Msigwa wa Ikulu hana undugu na Msigwa wa CHADEMA

Walaa Magufuli hana undugu wa damu na Magufuli ,isipokuwa mtoto wa dadake Msigwa ameolewa kwa Magufuli.

Hivo vikao vya akina Magufuli ,Msigwa haingii.
Sawa ila kuoleana si kunatengeneza undugu
 

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,595
2,000
... naupenda ujasiri wa Msigwa JAPO SIKUBALIANI NA WAZO LA KUMKABIDHI CHAMA KAMA MWENYEKITI MPAKA PUMZI YANGU YA MWISHO!
... I smell a rat somewhere!
 

BigBro

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,585
2,000
Yes ndio huyo, Kumbuka Yeye na Magufuli ni ndugu, Plus Gerson Msigwa wa Ikulu

Mara nyingi alimtuhumu Magufuli kuwa anavunja haki za watu
Mkuu Gerson Msigwa hana udungu kabisa na Peter ni majina tu yamefanana kama ilivyo Kwa wachaga majina ya Macha, Shayo, Mosha. Msigwa wa Ikulu ndugu yake ni Omar Msigwa mwenye mabasi ya Superfeo ambaye maskani yake ni Songea huko
 

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
243
1,000
Navyojua
Msigwa wa Ikulu hana undugu na Msigwa wa CHADEMA

Walaa Magufuli hana undugu wa damu na Magufuli ,isipokuwa mtoto wa dadake Msigwa ameolewa kwa Magufuli.

Hivo vikao vya akina Magufuli ,Msigwa haingii.
Mama yako na Baba yako wana undugu gani?

Kila mtu alizaliwa kwa wazazi wake

Inakuaje Baba yako na Mama yako wawe ndugu wakati wamekutana wakiwa watu wazima na kila mtu na malezi na matatizo yake

Think Thrice
 

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
243
1,000
Mkuu Gerson Msigwa hana udungu kabisa na Peter ni majina tu yamefanana kama ilivyo Kwa wachaga majina ya Macha, Shayo, Mosha. Msigwa wa Ikulu ndugu yake ni Omar Msigwa mwenye mabasi ya Superfeo ambaye maskani yake ni Songea huko
Ahaaa Omar wa Masjid na Peter wa sinagogi

Mkuu acha kuwachanganya makafiri/wagalatia na Wapelestine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom