Je,Pete ya ndoa,....?Kwa walio oa na kuolewa.

Kisoda2

JF-Expert Member
May 30, 2008
2,475
745
Inatokea umeingia katika restaurant, club ama sehemu yeyote ya public na uko mwenyewe tu,ghafla anaingia binti mrembo/kijana mtanashati naye yupo single(hajaambatana na yeyote).Moyo unakulipuka,na unatengeneza mazingira ya kumtokea kutaka kujiweka katika himaya yake/yako.
Katika kumshushia mistari ya hapa na pale unagundua amevaa pete ya ndoa,naye bila kusita anakutandika na jibu hili:Samahani nimeolewa/nina mke mie,hivyo huna haja ya kuniimbisha kihivyo.

Je,hizi pete zinasaidia kuzuia mashambulizi ya kimahaba nk, ama ndio zinaongeza kasi ya kutamaniwa zaidi?
 
zinapunguza kwani pale tu utakapotokea sehemu yoyote ile na pete yako inaonyesha status yako

lakini siku hizi watu wanaona kama mapambo heshima ya pete ya ndoa haipo tena
kuna baadhi wanadiriki kuzivua wakiwa katika mazingira ya starehe na sehemu ambazo wanaona hazifai kuonyesha status zao
 
Na wengine wanazivaa wakati hawako kwenye ndoa. Kuna ile dhana kuwa watu walio kwenye ndoa ni dili la kimapenzi.
 
pete hazina msaada!

kama mwanamke kicheche ATAENDELEA KUWA KICHECHE.enzi zetu tumepiga sana madem wenye ndoa zao
 
Inatokea umingia katika restaurant ama club na uko mwenyewe tu,ghafla anaingia binti mrembo/kijana mtanashati naye yupo single(hajaambatana na yeyote).Moyo unakulipuka,na unatengeneza mazingira ya kumtokea kutaka kujiweka katika himaya yake/yako.
Katika kumshushia mistari ya hapa na pale unagundua amevaa pete ya ndoa,naye bila kusita anakutandika na jibu hili:Samahani nimeolewa/nina mke mie,hivyo huna haja ya kuniimbisha kihivyo.

Je,hizi pete zinasaidia kuzuia mashambulizi ya kimahaba nk, ama ndio zinaongeza kasi ya kutamaniwa zaidi?

Licha ya kupunguza mashambulizi... zinaleta heshima na taadhima kwa mvaaji! Amen
 
zinapunguza kwani pale tu utakapotokea sehemu yoyote ile na pete yako inaonyesha status yako

lakini siku hizi watu wanaona kama mapambo heshima ya pete ya ndoa haipo tena
kuna baadhi wanadiriki kuzivua wakiwa katika mazingira ya starehe na sehemu ambazo wanaona hazifai kuonyesha status zao

Sawa kabisa dada wa1.
Ila kuna kinasiye tukiambiwa nimeolewa,utasikia kwani nini bwana,..kuolewa kitu gani!!

yaana heshima imekwenda na maji kabisa.

Kuna wadada wengine ukimwambia nina mke,utashangaa na roho yako vile atakavyoshangilia ukimuliza kulikoni utaambiwa kuwa unamfaa sana,hutakua msumbufu kwake nk.
 
Licha ya kupunguza mashambulizi... zinaleta heshima na taadhima kwa mvaaji! Amen

Nani alikudangaya mazee? Hizo pete kwani zinatoka mbinguni? Hapo Kariakoo zinauzwa kama njugu. Mabaamedi na machangudoa wa kumwaga wanazivaa wakati hawajaolewa. Jidanganyeni tu na heshima za pete. The real heshima ya ndoa iko moyoni bana!
 
Swadaktaa!!!
 
Leo tuko pamoja binamu, heshima ya ndoa ya mtu iko moyoni mwake na wala si pete, kwa ufupi siku hizi wachache sana wanaojali exiztance ya hiyo pete ya ndoa, akitaka kutongoza/kutongozwa pete is not a case.
 
Kwa wanaoelewa maana yake ambao ni wachache saaaana zinasaidia.Lakini wengi wao ni fasheni tu imeingia ya kuvaa pete siku hizi.Kuna watu hawako kwenye ndoa nao wanavaa na ndio wakwanza kuingilia ndoa za wenzao.
 
Hii ni sawa na cheti kwa muhitimu wa shule, LAZIMA
Pete ni utambulisho wa Muunganiko wa Wawili Wapendanao kwa HAKI

Tatizo ni kwamba ukicheche tumeuweka mbele, hatuna tabia ya kuamini hata vile vitu vinavyoonekana. utaambiwa mtu ana UKIMWI bada watakwambia mwongo wao ni NGONO TU.Bado watataka tu.
 
Leo tuko pamoja binamu, heshima ya ndoa ya mtu iko moyoni mwake na wala si pete, kwa ufupi siku hizi wachache sana wanaojali exiztance ya hiyo pete ya ndoa, akitaka kutongoza/kutongozwa pete is not a case.

Ndoa ni watu wawili mkipendana na kuaminiana mtaishi kwa furaha sn. (avatar nimebadili kama ulivyoniambia nafikiri utafurahi sasa)
 
Sawa kabisa dada wa1.
Ila kuna kinasiye tukiambiwa nimeolewa,utasikia kwani nini bwana,..kuolewa kitu gani!!

yaana heshima imekwenda na maji kabisa.

Kuna wadada wengine ukimwambia nina mke,utashangaa na roho yako vile atakavyoshangilia ukimuliza kulikoni utaambiwa kuwa unamfaa sana,hutakua msumbufu kwake nk.

hao kina dada wanafurahi kwa sababu wanajua watakuwa wanachuna kwa kwenda mbele ..unatoka kwa wife umeshafuliwa ,nyooshewa na mahitaji yote ambayo anatakiwa mwanamke akufanyie
ukifika kwa kadada kenyewe kana kazi moja na mshiko wako

teh teh teh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom