Je, Pasco Mayalla kachochea kufuatiliwa kwa Jamii Media?

Habari zenu wakuu!

Tushukuru kwa Mungu kuiona siku nyengine kwani kuna watu waliamka jana na kutegemea kuiona leo lakin Mungu hajawapa nafasi hiyo.

Huo ni utangulizi ila si moja ya mada ambayo ilibidi niandike hapa, mada halisi ni kuhoji; Je, Bwana Pasco Mayalla(NJAA) ndio chanzo ya haya?

Tukumbuke mwezi uliopita mh rais wa Tanzania aliita kikao na waandishi wa habari lengo ni kujua dira yake n.k.

Sasa katika mahojiano hayo maswali mengi yaliulizwa ikiwemo mkurugenzi wa TBC, JamiiForums members n.k

Katika maswali yalioulizwa yalikuwa mengine ni rahisi kujibiwa kwa kuwa tuliyaona lakini mengine ni magumu sana kwa rais kuyajibu lakini kiuhalisia hakuna swali gumu ila inategemea na mjibuji.

Swali aliouliza Pasco Mayalla kiukweli lilishtusha watu kwa kuwa ni zitto licha ya kuliweka katika mfumo ulio rahisi kwa mtu asiyejua maswali kuona ni kitu simple lakini lile swali halikupata jibu sahihi.

Ndiyo maana mijadala mengi ilianzishwa humu ndani mpaka Facebook n.k.

So, hebu tujadili; Je, Pasco Mayalla kachochea kufutiliwa kwa Jamii Media kutokana na maswali yake tata?

Naomba kuwasilisha..
Kuna mada 2 humu zilikuwa moto wakuotea mbali sana
1. Sizonje
2. Pogba
Hizi mada watu walifunguka hasa na kila aina ya kejeli kila aina, kuna muda jamaa alikuwa anawafuma wasaidizi wake wakicheka vibweka vya jf. Na wengine wakirusha madongo kwa siri
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom