Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,943
- 18,665
Juzi Rais Magufuli alivyokuwa Chato alitembelea shule ya msingi aliyosomea. Pale shuleni aliwahaidi kuwachangia madarasa matatu pamoja na ofisi ya walimu. Nanukuu " Namimi nitawachangia hapa madarasa Matatu". Alisema kuwa ataleta wajenzi yeye, vifaa yeye na madarasa yatajengwa kwa usimamizi wake na atawakabizi siku yakiwa tiyari kama yeye.
Hili ni jambo jema lakini ninapata utata kuelewa hii kauli ya Rais Magufuli anaposema atajenga yeye na sio serikali. Anapotoa ahadi yeye kama yeye inamaana kwamba pesa anatoa kwenye mfuko wake na sio kodi ya watanzania.
Rais anapotoa ahadi kama serikali hapo ndipo pesa za walipa kodi hutumika.
Sasa izo pesa alizohaidi kama yeye je zinatoka wapi?