je open university inaweza nisaidia kwa hili

Benard kombe

Senior Member
Jul 15, 2012
138
41
nina elimu ya kidato cha nne niliajiliwa kama mwalimu wa shule ya msingi mwaka 2008 baada ya kuona hailipi nikaachana nayo mwaka 2010.nikaamua kusafisha cheti bahati mbaya mwaka 2010,2011 matokeo yalikuwa siyo mazuri.
swali langu ni kwamba je nikiamua kusoma foundation kozi open university inaweza nisaidia nikafikia malengo angalau ya kupata hata digrii moja.sitaki kulisiti tena
kwa sasa nafundisha shule binafsi.
 
ndugu umerisiti mara mbili na kufeli! hebu angalia kitu kingine cha kufanya ambacho utahisi utafanya vizuri zaidi kuliko elimu ukipata digrii hata credit tatu hazijafika na competition ya ajira ilivyo utapata kazi kweli? na hata ukipata tofauti ya mshahara itakuwa ndogo sana nina jamaa ana digrii wakamwambia ataanzia mshahara wa 100,000 mpaka uje umalize hiyo digrii ya kuunga unga unafikiri ushindani wa ajira utakuwaje? jilaumu sana kwa kuacha ualimu.
 
Mhh hii kali, yaani wewe kwa sasa ni mwalimu. Tanzania nchi yangu. We mwalimu nakuomba niko chini ya miguu yako punguza speed ya kuikimbilia degree. Wana JF mmeona naibu waziri wa wizara hiyohiyo alivyo na wafuasi lukuki nyuma yake "eti kwa sasa mimi ni mwalimu" yeleuwiiiiiii

using JamiiForums
 
Hivi degree za siku hizi ni za kudesa? nini! Ina maana unaugwaya mtihani wa A-level kuliko hizo test za university. Safisha cheti bana acha woga.
 
Kaka wasikukatishe tamaa. Foundation course ni nzuri sana hasa ukipata walimu wazuri wa kukusaidia. Ukiweza kupata wastan wa masomo yote 50% ujue utaweza kusoma degree. Haina shida kabisa hao wanaokushauri uachane na kusoma degree ni waongo. Wengi tu wamefanikiwa kwa njia hiyo hiyo ni bidii yako. Kuliko kukomaa na kurisiti wakati mitihani yenyewe kusahihisha ni bahati nasibu. Njia nyingine unaweza ukaanza na diploma kwanza kwa kuwa Certificate unayo, halafu utaanza degree moja kwa moja.
 
Kama umefeli mara mbili hiyo foundation nayo jiandae. Acha uvivu wa kujisomea na kuelewa unachosoma.
 
Kaka wasikukatishe tamaa. Foundation course ni nzuri sana hasa ukipata walimu wazuri wa kukusaidia. Ukiweza kupata wastan wa masomo yote 50% ujue utaweza kusoma degree. Haina shida kabisa hao wanaokushauri uachane na kusoma degree ni waongo. Wengi tu wamefanikiwa kwa njia hiyo hiyo ni bidii yako. Kuliko kukomaa na kurisiti wakati mitihani yenyewe kusahihisha ni bahati nasibu. Njia nyingine unaweza ukaanza na diploma kwanza kwa kuwa Certificate unayo, halafu utaanza degree moja kwa moja.
Unachotafuta ni cheti kilichoandikwa 'digrii' siyo digrii yenyewe. Kama huwezi O' level digrii, ikiwa na maana ya content siyo kuiba mitihani au njia zingine za mkato, utawezaje?
 
Kwa kuwa unabidii ya elimu usikatishwe tamaa, open university wanafundisha pia Diploma ya Primary Teacher Education. Tembelea ofisi zao wakupe maelezo. Kaza msuli na degree unaweza fanikiwa kuisoma, Ukifaulu certificate na diploma kozi zao.
 
Foundation ni koz sahihi kwako, ndo maana iliwekwa makusudi kwa ajili ya watu kama wewe! wasikukatishe tamaa, kila mtu ana pita njia yake kutafuta maendeleo. Kama kweli umeamua kusoma foundation itakutoa, iko well designed, sio ,magumashi!
 
Hongera sana, hata kwa wazo zuri ulilonalo, hakika tayari degree umeshapata tena na mafanikio mengine mengi, kumbuka wanao shindwa ndio wenye kuhitiimu na mafanikio mengi sana, mifano tunayo mingi sana...
 
sijui lkn ila foundation open university sio rahisi kama unavyofikiria wewe,kama wadau wengine waliokushauri sio lazima upite form 6 ndo upate degree,ila jitihada zako binafsi ndo zitakuweza kufanya foundation mana iko tight then ukimaliza unaweza kuitafuta hiyo bachelor,kama hauko tayari ni bora tu ukae uendelee kufundisha kuliko kupoteza pesa zako
 
Back
Top Bottom