Je Nyufa alizoziona Mwalimu Nyerere mwaka 1994 zinaelekea kuzibika au ndo zinaongezeka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Nyufa alizoziona Mwalimu Nyerere mwaka 1994 zinaelekea kuzibika au ndo zinaongezeka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Aug 18, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika hotuba ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa Kilimanjaro hotel June 14, 1994 ambayo mdau wa libeneke ameipost kwenye you tube (Hotuba ya Mwalimu Nyerere hoteli ya Kilimanjaro June 14, 1994 (Michuzi Blog) - YouTube), mwalimu alizitaja hizi zifuatazo kama nyufa kuu nchini Tanzania;

  1. Muungano-aliona kwamba unatikisika na kuna hatari za Uzanzibari na Utanganyika na alitupa angalizo kwamba hakuna mtanganyika wala Mzanzibari. Huu aliuita ufa mkubwa kabisa, ufa wa msingi.
  2. Kupuuza puuza katiba na ambayo ndo sheria ya msingi na 3. Uongozi usiofuata sheria. Hapa alisema viongozi wanajiamulia mambo yao wenyewe bila kufuata sheria akatolea mfano mtu anapata ushauri kwa mkewa katika kuamua mambo. Watu wanaendesha nchi bila kujali sheria
  4. Rushwa (“kiongozi wetu unakula rushwa?”). Alisema, nchi ikishakua na wala rushwa, maskini hawana kitu na rushwa ya Tanzania haina aibu. Pia alisema serikali corrupt haikusanyi kodi na inatumwa na wenye mali!

  Swali ni Je, mwelekeo wa nchi hii ya Tanzania katika kuziba nyufa hizi toka mwaka 1994 tunaonaje? Je ni nyufa ipi ambayo tunaona tumejitahidi kuiziba au walau kuidhibiti isiendelee? Ni hatari kwa nchi kama tukijitathmini na kuona bado tupo katika hali ya 1994 au nyufa zimezidi kupasuka!

  Nawasilisha.
   
Loading...