Je Nyerere angekuwepo angelisherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Nyerere angekuwepo angelisherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ehud, Apr 5, 2011.

 1. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu serikali ya Tanzania inajiandaa kusherekea miaka 50 ya uhuru. Wapo wanaosema bado Tanzania haijafikisha miaka 50 kwani Tanzania ilizaliwa mwaka 1964 hivyo ina miaka 47 tu. Wapo wanaosema viongozi wetu wanapaswa kuwa wakweli na kusema wazi kuwa kitakachosherekewa mwaka huu ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Lakini katika Tanzania ya leo neno Tanganyika limekuwa neno linaloogopwa kiasi kwamba hata viongozi wanaona aibu kulitaja hadharani.

  Swali nalotaka sote tujiulize ni Je kama waasisi wa taifa hili la Tanzania wangelikuwa hai leo hususani Mwl. Nyerere je angetoka hadharani na kutuambia kuwa sherehe hizi za miaka 50 ni za uhuru wa Tanzania au Tanganyika?
   
Loading...