Je Nyerere alishawahi kukutana na Magufuli?

Nyerere alimweka MKAPA na MWINYI, MTANDAO Ukamweka KIKWETE, then MKAPA Kamweka MAGUFULI

Je, una swali ?
Naomba maelezo ya kina mkuu.. Kwa faida yangu ambae sijang'amua kitu hapa ingawaje nadhani lipo la kujifunza
 
Ndugu yangu kwa sasa hakuna mtu mwenye nguvu ya Kufanya maamuzi makubwa ya nchi kisiasa hapa nchini kama MKAPA
 
Kukutana au kuonana na Nyerere sio kigezo cha kuwa kiongozi bora, Huyo Nyerere alikuwa binadamu wa kawaida sana.
 
Hii bandiko outward linaonekana la kijinga lakini lina undani wake!
Nilikuwa najiuliza mfano marais kama Nelson Mandela ameandika vitabu ambavyo ni refeence point ya maisha ya wengi wetu na nimeona kitabu kingine cha Mzee Thabo Mbeki kina kurasa zaidi ya 900.
Kwa Tanzania nimeona vitabu vya Mwalimu pekee ndiye alijitahidi kuandika. Sijaona kitabu chochote cha Mwinyi, Mkapa ni kile alichoandika akiwa Makerere, JK hata makala yake kwenye gazeti sijawahi kuiona na sasa tunaye JPM. Hiyo list inajumuisha mawaziri wakuu, makatibu, wakurugenzi nk japo wengine ni maprofesa na madaktar. Nasikia Mzee Makamba alijitutumua lakini kilikuwa cha watoto wa Primary na akaiomba wizara ikiweke kwenye mitahala!
Sasa najiuliza tutawakumbuka vipi hawa watu kama hawajayadocument nawazo yao na ushauri juu ya mustakabali wa nchi walizoziongoza!?

Jinsi ya Viongozi wanavyoandika vitabu.
Sio wao wenyewe wanakaa kuandika. Anakuwa pembeni mwandishi maalum, anamuhoji historia ya maisha yake yote, harakati na kazi zake, fikra na msimamo wake, wanakusanya kumbukumbu kutoka sehemu nk. Ni mradi maalum kwa nia ya kutangaza propaganda fulani, au kuhifadhi historia au kupanua elimu kwenye taasisi za Elimu au hata pia ni biashara.

Tutakumbuka Tanzania tulikuwa tunapewa vitabu vya Mao Se Tung na majarida ya bure ya Sauti ya Umma kutoka Iran wakati wa vita vya Iraq na Iran?

Vitabu vingi huandikwa na watu mbali lakini anapewa kiongozi fulani kufanya uhariri na kukiidhinisha, na baadae kinaenda kwenye kazi ya uchapishaji.

Thabo Mbeki katika vitabu ambavyo amevipendekeza kwa wanafunzi wake ni vitabu vya Mwalimu Nyerere. Na kweli ukisoma vitabu vya Mwalimu Nyerere, huwa vinasisimua. Hata vile vilivyochapishwa kwa lugha ya Kingereza. Mtu anatamani angekuwa nae karibu.
 
Mkuu walikuwa wanaandika Yale waliyoyaamini na kuyatetea. Hawa marais wa .com hawana wanayoamini wala wanayoyatetea. Hivyo inakuwa ngumu kuandika
 
Alikuwa bado hajaingia kwenye harakati .Nyerere angekuwepo angepata kazi ya kukemea kila siku sijui angechoka?
Nadhani angeishia ubunge wa awamu moja tu,sifa ya kuwa rais ilikuwa lazima uwe umehudumu nje ya nchi mbalimbali na kupata uzoefu na kupata mwanga juu ya uongozi sio kutoka kijijni kwenu na kugombea urais
 
Alikuwa bado hajaingia kwenye harakati .Nyerere angekuwepo angepata kazi ya kukemea kila siku sijui angechoka?
Mkuu.....
Magufuli hakuwahi kua mwana harakati. Na hakuwahi kutamani wala hakujua kama atakuja kua mkubwa wa nchi.
 
EL alikua anaonekana kabisa kuwa kiongozi mzuri wa baadae "we waiting for you EL"
 
Jinsi ya Viongozi wanavyoandika vitabu.
Sio wao wenyewe wanakaa kuandika. Anakuwa pembeni mwandishi maalum, anamuhoji historia ya maisha yake yote, harakati na kazi zake, fikra na msimamo wake, wanakusanya kumbukumbu kutoka sehemu nk. Ni mradi maalum kwa nia ya kutangaza propaganda fulani, au kuhifadhi historia au kupanua elimu kwenye taasisi za Elimu au hata pia ni biashara.

Tutakumbuka Tanzania tulikuwa tunapewa vitabu vya Mao Se Tung na majarida ya bure ya Sauti ya Umma kutoka Iran wakati wa vita vya Iraq na Iran?

Vitabu vingi huandikwa na watu mbali lakini anapewa kiongozi fulani kufanya uhariri na kukiidhinisha, na baadae kinaenda kwenye kazi ya uchapishaji.

Thabo Mbeki katika vitabu ambavyo amevipendekeza kwa wanafunzi wake ni vitabu vya Mwalimu Nyerere. Na kweli ukisoma vitabu vya Mwalimu Nyerere, huwa vinasisimua. Hata vile vilivyochapishwa kwa lugha ya Kingereza. Mtu anatamani angekuwa nae karibu.
Umenikumbusha hili jarida la "Sauti Ya Umma" kutoka Irani, likimchamba Saddam Hussein, ukiwa member basi ulikuwa unatumiwa bure kila mwezi enzi hizooo
 
Kabisa. Kwamba Mungu hawezi kukupatia vyote...mfano Lowassa kukkosa urais licha ya kuwekeza mabilioni, funzo la pili ni kwamba Mungu humuinua mwenye haki, mfano Magufuli
Hivi kumbe ni rahisi sana kutambua mwenye haki,Kama wewe unavyotambua?
 
Hivi hawa vijana wa zamani akina Jk na ENL nao walikuwa wanajipendekeza na kujikombakomba kama hawa vijana tulionao wakati huu??
Haiwezekani kwa kuwa ni miongoni mwa vitu alivyokuwa akivipinga mwl.Nyerere yaani kujipendekeza na kujirahisisha kwa wakubwa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom