Je, nyadhifa za kitaifa mf. ubunge, uwaziri na urais wapewe watanzania wenye uwezo wa kifedha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, nyadhifa za kitaifa mf. ubunge, uwaziri na urais wapewe watanzania wenye uwezo wa kifedha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wired, May 7, 2012.

 1. W

  Wired New Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kawaida kwetu watanzania kuwanafasi ya uwaziri au ubunge ni nafasi ya "kuuaga umasikini". kwa viongoziwengi pindi wapatapo fursa tajwa hapo juu ndipo huchukua mikopo ya magari,nyumba n.k

  ( Mfano suala la Maige) kudhihirisha kwamba bado hata basic needswalikua hawajazipata. Hata spika amewahi kutoa kauli jimboni kwake mwaka janaakitetea suala la kuongeza posho kuwa kuna wabunge wanatamani kurudi kwenye professionzao manake kazi ya ubunge sasa "hailipi".


  Kwa mtazamo wangu hii inatokanana kuwa na viongozi ambao bado hawajajipanga kimaisha, kwamba wakipata nafasihizo ndipo wanaanza suala la kutafuta nyumba nzuri, gari kali n.k Tenakiongozi wa namna hii akiwa kijana ndiyo kabisaaa manake hata kusomesha watotowake bado.

  Kwa kuwa hizi ni nafasi za vipindimaalum na hakuna uhakika wa kuendelea nayo kama zilivyo kazi za kuajiriwa aukujiajiri, kiongozi huyu atahakikisha anakamilisha mambo tajwa hapo juu ikiwemokujiwekea akiba au kujipatia mtaji ili hata akiondoka aweze ku-survive.

  Ikumbukwe kwamba kama umeondolewa kwenye nafasi ya waziri au ubunge, status yanafasi hizo inawia vigumu kwa muhusika kuingia kwenye ajira nyinginezo na aghalabumtu wa namna hii anakua hana uzoefu wa ujasiriamali!
  Kutokana na maelezo hayo hapo juu, kiongozi masikini atawekeza zaidi katika kujijenga kimaisha, (ikiwemokufukuzia posho zote kupitia safari, vikao na rushwa tena zilizo "cheap"kwa sababu hajazoea kushika pesa nyingi) badala ya kujikita katika kulitumikiataifa.

  Lakini kwa mtu mwenye uwezo, anakua tayari anayo hayo mahitaji ya msingina ana uhakika wa future yake, anachotafuta hapo ni heshima tu ya kuitumikiajamii (self-actualization needs kwa wale mnaofahamu maslow's need hierarchy). Mfanoni kina ndesamburo na nimrod mkono
  Naleta kwenu wana jamii kwa maoni.
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wired hiki ulichotuletea hapa ni kituko. Labda kama una scientific research inayo support kuwa mtu akiwa tajiri anakuwa na haja ya kujilimbikizia mali zaidi. Kwa nchi za wenzetu wanaamini kuwa kama umeshindwa kujiletea maendeleo binafsi kamwe huwezi kuiletea maendeleo nchi yako, lakini huku kwetu kinachotakiwa sio utajiri au umaskini wa viongozi. Kinachotakiwa ni maadili ya uongozi kuzingatiwa na sheria kuchukua mkondo wake ukiiba. Kama leo kungekuwa na viongozi wezi wamejaa kwenye magereza yetu kwa makosa ya wizi wao bila kumbagua tumshitaki huyu na huyu swahiba yetu tumuache aendelee kula, watu wengi wangeogopa kuiba. Mshahara wa waziri na posho anazopata na fursa alizonazo kukopa benki na taasisi nyingine za fedha inatosha sana kumfanya kiongozi aishi maisha mazuri na akawa mudilifu.
   
 3. d

  dandabo JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  mimi naamini KINYUME cha uliyoyaandika!
   
Loading...