Je, niwekeze kupitia JATU Company PLC?

Matapeli hawa na sielewi kwanini wameruhusiwa kuuza hisa na kukusanya zaidi ya Billion 5. Wanadai wamelima na kuvuna, lakini hawataki kulipa wakulima wao. Cha kushangaza naskia hata kwenye hio App yao ya kuuzia chakula, chakula hakuna. Ukute hata hawajalima geresha tu.

Wanachukua pesa za watu alafu hawataki kulipa. Wafanyakazi wakiulizwa hawana majibu, ukimfata Mkurugenzi anaku'block.

Hawa watu watakiwa kukamatwa mapema kabla ya majanga walokutana nayo watu kwenye Mr Kuku.
 
Kutokana na watu wengi kuniandikia kuniuliza kama ni salama kuwekeza pesa JATU company PLC. Nimeamua kufanya utafiti na maswali kwenye utafiti wangu yalikuwa kama ifuatavyo;-

1. Nani anaongoza JATU?
2. Je, ni biashara gani wanafanya? Pia hii biashara ni hatarishi kwa pesa yangu?
3. Je, nini maana ya shares za JATU? Pia ni salama?

Nani anaongoza Jatu?
Kawaida kabla ya kufanya uwamuzi wa kuwekeza, ni swala la msingi kujiuliza kwamba nani unampa pesa yako. Hapa unatakiwa kuangalia "managament" ya kampuni husika. Kwasababu management ndio inatoa DIRA yote ya biashara, na hii DIRA ndio itafanya wewe kupata pesa au kupoteza pesa. Unatakiwa kusoma wasifu wa management nzima na kujiuliza swali, je hawa watu kwenye management, wana uzoefu wa kutosha kuendesha aina ya hii biashara? Kanuni ni kwamba, "ukitaka kulinda pesa yako,utawekeza sehemu ambayo una uwakika kwamba mtu ambaye utampa pesa ana uzoefu wa kutosha, kama si hivyo,kuna uwezekano wa kupoteza pesa".

Ukiangalia kwa sasa, management ya JATU anaongozwa na wana sheria, ambao hakuna sehemu yeyote wameonesha uzoefu kwenye maswala ya kilimo,Viwanda na Saccos. Management hii ingefaa kama JATU ingekuwa ni kampuni ya sheria.

Biashara
Biashara kubwa ya kampuni ni uwekezaji kwenye kilimo. Kilimo ni uwekezaji ambao unategemea na msimu, rutuba ya sehemu na ubora wa mazo husika. Pia ni biashara yenye hatari kubwa. Kwasabu ya bei kushuka na kupanda.

Pia lengo lao ni kukusanya wakulima wadogo na kuwawezesha kulima kwa kisasa. Ni wazo zuri,lakini halina Tija au ni biashara mabayo haina faida. Hii ni kwasabu kimo kidogo kina gharama kubwa kuliko kilimo kikubwa. kuwekeza strategy kwenye wakulima wadogo, sio strategy endelevu kwa afya ya kampuni.

Strategies:-
a/Ili kuweza kunufaika na kilimo, kampuni inatakiwa kuja na mpango au namna ya kuhifazi mazao,ili kuweza kukabili bei ya mazo ikiwa chini na kuepuka hasara. Paka sasa, hakuna sehemu yeyote ambayo wameonesha namna ambayo watatumia kuepuka hasara ya kushuka kwa bei ya mazo.

b/Njia nyingine ya kuweza kunufaika na kilimo, ni kutumia "Viwanda".Hii ni kubadilisha mazo na kufanya bidhaa. Kwenye maelezo, wanasema wanampango wa kufungua viwanda,lakini paka sasa hawajaweza kuonesha hivyo. Pia wanasema watakuwa wananunua mazo, lakini hakuna sehemu yeyote ambayo wameonesha kwamba wanatarajia kufanya nini na ayo mazo baada ya kununua.

Shares
Shares ambazo wanatoa ni "ordinary shares". Ukiwa na hizi share, wanakuhesabu wewe kuwa ni moja ya sehemu ya kampuni. Inamaana utakuwa na uwezo wa kupanga mipango ya uwendeshaji wa kampuni. Hatari ya kuwa na shares za aina hii ni kwamba, kuna uwezekano au hatarini kupoteza 100% ya uwekezaji wako. Pia utalipwa faida tu, pale management watapo amua kuwalipa.

Hitimisho

Kuna red flags nyingi sana namna ya hii kampuni inavyo endeshwa. Wameweza kuja na wazo zuri, lakini hawajaweza kuonesha ni namna gani watafanya kufikia malego. Pia kampuni imeanzishwa toka mwaka 2016 lakini, paka sasa hawajaweza kuonesha mahesabu yao ya mwaka tangu waanze kufanya biashara. Bila shaka hiii sio safe investment.

Hii ni kubwa sana kwangu imenifungua sana maana hawa jamaa wanavyojitangaza ni balaa kama ni marketing sijui ndio sales basi balaa ila back to operations seems there are alot of problmes.

Mwaka huu wakanishawishi na mtindo wao wa kilimo cha karatasi kuhusu soya ukiwekeza kama 900,000kwa ekari unapata 1,800,000 ukitoa ujinga ujinga unapata faida ya 600,000. Wanasema wanabima ya kilimoo sijui kama kwelii.

kwa hii Thread yako mkuu siweki hata mia watu tangia 2016 hawajaweka wazi vitabu. Basi watu wengi wameliwa sana.
 
Wanasumbua kulipa hawa JATU. Usipoteze muda wako.
 
Umefanya uamuzi sahihi. Wanahaha kutafuta hela ya kuwalipa wakulima sasa hivi. Jmosi iloisha wamebanwa hadi ya Takukuru walipe hela za watu
 
Back
Top Bottom