Je, nitakuwa nimemuharibu mtoto?

Anna pita

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
227
425
Mimi nina mtoto wa miezi 10 sasa, niliachana na aliyenipa ujauzito nikiwa na mimba ya miezi 2 mwaka jana mwezi wa 2, na tangu mwaka jana nilikua sijakutana kimwili na mwanaume yoyote yaani nimekaa mwaka 1 na miezi 5.

Miezi mitatu iliyopita nilikutana na kaka mmoja akawa anataka kunioa, but juzi nikashiriki nae tendo kibinadamu, na mimi na hisia kweli. Nilisex nae mara 1 tu na nilienda kuoga kabla sijamnyonyesha mtoto.

Naomba kuuliza, inaweza kumdhuru mtoto?

Je, nifanyeje?

Msinielewe vibaya ndugu zangu, baba mtoto yuko mbali na ana mwanamke mwingine. Hana muda na mimi kabisa, mimi ni binadamu hisia zilinizidi tu nikawa nimefanya hivyo.
 
Anna pita

Kuna kitu kinaitwa kuchanganya joto, kama joto la huyo mwanaume mpya likisigana na la mtoto shida kidogo yaweza kutokea, lakini hili hakuna proof ya kisayansi
Ushauri wangu jitahidi unapokutana na jamaa hakikisha unaoga vizuri na kujipa muda wa kutosha kabla hujamrudia mtoto
Jitahidi sana mtoto asiwe na tatizo lolote kwakuwa kuna watu wanaosubiri ukosee wapate pa kusemea
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini usisubiri umalize kunyonyesha bibie.....hizi dyudyu zipo tu
 
Kuna kitu kinaitwa kuchanganya joto, kama joto la huyo mwanaume mpya likisigana na la mtoto shida kidogo yaweza kutokea, lakini hili hakuna proof ya kisayansi
Ushauri wangu jitahidi unapokutana na jamaa hakikisha unaoga vizuri na kujipa muda wa kutosha kabla hujamrudia mtoto
Jitahidi sana mtoto asiwe na tatizo lolote kwakuwa kuna watu wanaosubiri ukosee wapate pa kusemea

asante japo nimesex nae mara 1 na najutia mno sitegemei kama nitaridia tena nadhani mpaka mtoto wangu aache kunyonya,, baada ya tendo nilienda kuoga
 
...hakuna uhusiano juu ya sex na afya ya mtoto. Hivyo vyote ni vitu vya kufikirika tu na imani za kijadi. Ila kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uchafu wa mama na mtoto. So ishu ni uchafu hata usiposex lakini ukiwa mchafu mtoto ataharibika kwa maana ya kukosa afya bora. Juu ya yote si salama kufanya nje ya ndoa, kama angekuwa mume wako ningekwambia unaweza kuendelea na sex muda wote bila wasi....
 
  • Thanks
Reactions: nao
Usimshike mtoto wako kabla hujaoga, pia hakikisha jamaa anavaa condom. Kinyume na hapo mtoto atakuwa kama katuni
 
Ndio kuna uhuusiano. Unapofanya sex na mtu tayari mnajenga soul ties; kummbuka mwanao pia anahusiana nawe kidamu na soul. Sasa naye unamuunganisha kwenye kifungo na huyo bwana wako. Kama huyo ana mambo yake basi yatampata mtoto pia. Just like akikuambukiza ukimwi nawe waweza muambukiza mtoto thru maziwa.
Angekuwa ni baba yake hamna shida kwani wana tie already.

Ufanyaje sasa? Tubu na jifungue hicho kifungo kwa damu ya Yesu. Denounce maneno yote ulliyoyaahidi ukiwa ktk mahaba na kujiweka huru kwa Damu ya Yesu, maana tumekombolewa kwa Damu ya Mwanakondoo na neno la ushuhuda.


Anyway Anna Pita siauamini uzi wako kutokana na history ya nyuzi zako za nyuma, but nimeandika kwa faida ya wengine
 
Wala usihofu. Hakuna madhara yoyote ambayo mtoto anapata kutokana na hili. Hii dhana ya kuharibu mtoto ilitumika enzi zile hakuna mbinu za uzazi wa mpango ili kumsaidia mama kupanga uzazi watoto wasipishane umri kama wa kuku. Na pia kumsaidia mama apumzike (manake wababa wa enzi zetu za mwalimu si haba. Hawa wa chipsi zege na pilipili wanarashia tu lol). Kuharibu mtoto ni malnutrition tu, kwa kukosa lishe bora.

Wewe jilie tundi kwa raha zako. Ila mambo matatu zingatia, magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi (hilo jamaa umepima nalo?). Pili uzazi wa mpango, usije ukajisapraizi na baby mwingine hapa kabla hujatualika harusi. Tatu na muhimu, usijirushe na penzi jipya ukasahau kuangalia mwanao, ale vizuri na awe na ratiba inayoeleweka.
asante japo nimesex nae mara 1 na najutia mno sitegemei kama nitaridia tena nadhani mpaka mtoto wangu aache kunyonya,, baada ya tendo nilienda kuoga
 
Pole sana kwa mfadhaiko huo, ni vema ukasubiri mtoto aache kunyonya kwanza na ikiwezekana mwachishe sasa kama unaweza kumudu lishe mbadala! Zaidi muombe Mungu akusamehe na akupe muongozo sahihi!
 
Sina uzoefu sana na hilo, ila tumia condom kuzuia uharibifu wa maziwa, maana toto hatakiwi kunyonya kama mama kakutana namwanaume tofaut nababa wadamu, ila nahis Mungu atatia mkono wake.

Jitahid ufunge ndoa rasmi isijekuwa na huyo nae akakuchezea akakuacha, pia omba ushauri clinic, manesi watakusaidia namna ya kufanya ili unyonyeshe wakati una stepfather, usimwachishe mtoto, maziwa ya mama ni kinga kwa mtoto dhidi ya maradhi.
 
Hakuna uhusiano wowote kati ya sex kwa mama na afya ya mwanao hzo ni imani tu na woga wako..
 
Back
Top Bottom