Je nitakumbukwa kwenye historia ya ukombozi wa awamu ya pili...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je nitakumbukwa kwenye historia ya ukombozi wa awamu ya pili...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Nov 11, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Wiki hii imekuwa na matukio makubwa matatu na achilia mbali yale madogo madogo yanayoonyesha kuwa kwa vyovyote vile kama serikali ya CCM aka Magamba hawatakubali kukaa chini na kuwauliza wenye nchi(UMMA WA WATANZANIA) namna ya kuongoza nchi yao wana wakati mgumu sana kuanzia sasa na kuendelea...Matukio yafuatayo ni dalili tosha na ujumbe tosha kwa watawala na wenye akili timamu na dhamira safi ya kusikia watafanya mabadiliko

  Arusha-mkesha wa kusukuma Mbunge wao kuachiwa..
  Mbeya-wamachinga kutaka watendewe haki..na kwa taarifa za awali ni kwamba Polisi wakawaida walishindwa kuwaimili mpaka walipofika JKT
  UDSM nao nasikia wanapiga jaramba....

  Haya ni makubwa..bado kuna madogo madogo ambayo hayafiki kwenye vyombo vya habari.....Nani amewaamsha watanzani wakafahamu haki zao namna hii? Maana zamani tuliaminishwa kuwa haki hailazimishwi unaomba...lakini sasa watu wamefahamu kuwa haki inatafutwa na nguvu yoyote ile...Baada ya kuona hali hii na kwa kuwa mimi ni great thinker nikagundua sasa kuna haja ya mimi kuwa sehemu ya ukombozi huu,maana wajukuu zangu wanategemea waje waone nimefanya nini kwa nchi hii...kwa wale wasiokubaliana na hali hii kwasasa..hakika wataachwa nyuma na watakuja kuona aibu kubwa baada ya nchi kukombolewa......Na mara zote watu duni ndio walioleta ukombozi..unaweza kusema wamachinga watafanya nini? Leo wameonyesha wao ni akina nani....

  NATAMANI KUWA SEHEMU YA HISTORIA YA UKOMBOZI WA PILI WA NCHI HII..BAADA YA UKOMBOZI WA KWANZA KUFANYWA NA NYERERE NA WENZAKE NA WANAENDELEA KUKUMBUKWA MPAKA SASA....
   
Loading...