Je, Nisahihi kwa mpangaji mwenzako kukutukana kisa kuchelewesha kulipa pesa ya maji?

Yohana Daniel

Member
Mar 18, 2018
59
24
Habari za sasa ndugu zangu mimi sio mgeni ila ni mara ya kwanza kuandika katika jukwaa la Sheria.
Naomba msaada wa kisheria kwa kilichonikuta mwenzenu, hapa nilipopanga kuna mita ya maji imeharibika sababu watoto wanaichezea
Kinachotakiwa ni kwamba tunatakiwa tuchange kuinunua wapangaji wote, hiyo sio shida saana tatizo ni kwamba mpangaji mwenzangu analazimisha nitoe pesa leo hiihii hata kama sina nikakope ili nilipie hiyo mita tena kwa matusi ya nguoni kanimwagia afu kaingia mpaka chumbani kwangu bila hodi
Kibaya zaidi huyu mpangaji yeye kahamia juzi ni mgeni,bahati nzuri nimemrekodi mwanzo mwisho alichonifanyia naomba msaada nimfanyaje Huyu Asanteni.
 
Mimi si mwanasheria lkn kwakuwa kitendo alichokifanya si chakiungwana nenda serikali ya mtaa bila kusahaukumwambia mwenye nyumba
 
Mimi si mwanasheria lkn kwakuwa kitendo alichokifanya si chakiungwana nenda serikali ya mtaa bila kusahaukumwambia mwenye nyumba
Mwenye nimeshamwambia Lakini naona hatoi Majibu ya kuridhisha
"Eti tukikaa kikao utatoa dukuduku lako" mwenye nyumba huyo
 
Pole sana, nenda kamshtaki kwa balozi kama yupo au pitiliza serikali za mtaa maana ilo ni kama shambulio flani hivi.
 
Pole mkuu, ila kama unaweza potezea tu maisha yaendelee, kuna watu si wastaarabu tu ila hiyo kunifata hadi chumbani duh, ningempa roba moja hiyo angejuta.
 
Back
Top Bottom