Je, nisahihi kumshitaki mume kwa dada yake kuwa ana michepuko?

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Heri ya ku sensabika kwenu.

Mke kafuma tukio la Mimi kuchepuka na dada mmoja muuza duka. Katika mabishano ya hapa napale nikaamua nikubali ili mzozo uishe.

Leo asubuhi nimekaa sebuleni nasubiri makarani wa sensa nashangaa simu inaita kucheki ni dada yangu anapiga.
Kusudi kubwa lakupiga nikunionya kuwa wifi yake(mke wng) kamwelez kila kitu kuhusu hako kamchepuko hivyo niache mara moja. Aliongea mambo mengi kuonyesha kuwa mke wangu hakumficha chochote.

Kwa kuwa nilikuwa naongelea nje ilibidi niingie ndani kumuuliza mke sababu zakupeleka mashtaka Kama hayo kwa dada.Alichonijibu nikwamba amefanya hivyo makusudi kwa kuwa aliona kwa wifi yake ndo sehemu sahihi.

Sasa nimewaza nikaona niwashirikishe na nyie kwa njia ya maswali mawili;
Moja, nivizuri mke kumsemea mumewe kwa dada zake kuhusiana na Mambo Kama haya?(Fikiri kwamba hana mwngn wakumshirikisha)

Pili; Kwa upande wa mwanaume ni sahihi kumsemea mkeo kwa Kaka yake juu ya issue za kuchepuka?(Fikiri kwamba hana mwngn wakumshirikisha)

Wasalaam!
 
Wee tuliza ball mkuu hawa wanawake zetu maneno tuu vitendo sifuri. Hawezi kuondoka hapo kwako na mwambie tuu kuwa dada kanipigia nimesikia maneno yako am sory imeisha hiyoooo.
Mpeleke outing kidogo kwa kajihotel na upige show ya ukweli
 
Acha kuchepuka asiwe anakusemelea....

Ila katika jambo siwezi na sishauri mtu kufanya ni kuongelea mabaya ya mke/mume Kwa ndugu zake.

Maana hata iweje huwezi kuwa mzuri kuliko ndugu Yao, kitachotokea tu baadae watachoka mashtaka ya Kila siku na wewe ndio utaonekana ni tatizo.
 
Heri ya ku sensabika kwenu.

Mke kafuma tukio la Mimi kuchepuka na dada mmoja muuza duka. Katika mabishano ya hapa napale nikaamua nikubali ili mzozo uishe.
Najibu swali lako kwa kukuuliza swali jingine: Jee, ni sahihi kuanika mambo ya chumbani mwako (au nyumbani mwako kwa ujumla) kwa kutaja hadharani mkeo aliyoyafanya baada ya kukufuma na mchepuko?
 
Wewe kwa akili zako timamu unadhan dada yako amekupigia cm akuonye serious au ameamua tu amridhishe wifi yake..?
 
Ungeeleza kwanza sababu ya wewe kuchepuka kijana, umeenda kuzini so mkeo (kama ni mkristo) anayo tiketi ya kuachana nawe kisha akaolewe na ampendaye.

Eleza kwanza ukweli, kwa nini ulichepuka?
Hakuna sabab nzuri ya kuhalalisha kuchepuka mzee.Vinginevyo isingeitwa kuchepuka.
Nilichouliza,nisahihi yeye kunishtaki kwa dada?
 
Najibu swali lako kwa kukuuliza swali jingine: Jee, ni sahihi kuanika mambo ya chumbani mwako (au nyumbani mwako kwa ujumla) kwa kutaja hadharani mkeo aliyoyafanya baada ya kukufuma na mchepuko?
Ama Kuna passport size humu na kitambulisho Cha nida?
 
Mimi ningepeleka Hadi kwa mchungaji wako na kwa Boss wako, kwa dada yako haitoshi. Kwani ulishindwa Nini kuficha asijue kuwa unaruka majoka Nje? Kushindwa kuficha na kufanya upuuzi wako karibu na nyumbani Hadi mke kujua ni kosa kubwa hebu mpe heshima yake huyo mama hata akikatiza kitaa asinyanyuliwe vidole akajiona INFERIOR LOL😏
 
Hakuna sabab nzuri ya kuhalalisha kuchepuka mzee.Vinginevyo isingeitwa kuchepuka.
Nilichouliza,nisahihi yeye kunishtaki kwa dada?
Ni sahihi kabisa kama wewe ulivyoona kuwa ni sahihi kuchepuka na muuza duka.

Hata onyo alilokupa dada yako lilikuwa sahihi kabisa
 
Heri ya ku sensabika kwenu.

Mke kafuma tukio la Mimi kuchepuka na dada mmoja muuza duka. Katika mabishano ya hapa napale nikaamua nikubali ili mzozo uishe.

Leo asubuhi nimekaa sebuleni nasubiri makarani wa sensa nashangaa simu inaita kucheki ni dada yangu anapiga.
Kusudi kubwa lakupiga nikunionya kuwa wifi yake(mke wng) kamwelez kila kitu kuhusu hako kamchepuko hivyo niache mara moja. Aliongea mambo mengi kuonyesha kuwa mke wangu hakumficha chochote.

Kwa kuwa nilikuwa naongelea nje ilibidi niingie ndani kumuuliza mke sababu zakupeleka mashtaka Kama hayo kwa dada.Alichonijibu nikwamba amefanya hivyo makusudi kwa kuwa aliona kwa wifi yake ndo sehemu sahihi.

Sasa nimewaza nikaona niwashirikishe na nyie kwa njia ya maswali mawili;
Moja, nivizuri mke kumsemea mumewe kwa dada zake kuhusiana na Mambo Kama haya?(Fikiri kwamba hana mwngn wakumshirikisha)

Pili; Kwa upande wa mwanaume ni sahihi kumsemea mkeo kwa Kaka yake juu ya issue za kuchepuka?(Fikiri kwamba hana mwngn wakumshirikisha)

Wasalaam!
PERCEPTIONS
 
Sasa dada atasaidia nini....ni kufa kijerumani kama kuna uhitaji wa kutafuta pa kupumulia tafuta mtu msimulie imeisha hiyo. Kifuatacho itv kinajulikana
 
Back
Top Bottom