Je,nipo salama hapa?..naomba mawazo yenu wadau

chwechinyong

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
223
105
ni kwamba nipo nje ya nchi kimasomo yapata miaka miwili sasa na nimeoa.huwa narudi kila baada ya mda fulani ili kutoa huduma kwa familia na kuepusha vishawishi kuingilia ndoa yetu. Mara ya mwisho nilirudi mwezi wa 12 tarehe 13 mwaka jana 2012. Kufika mwezi wa kwanza tarehe 5, yaani wiki 3 tu baada ya kurudi mke wangu akalalamikia tumbo kuuma baada ya siku kama 4 alienda kupima na kuambiwa kuwa ni mjamzito, ndo mwezi ulikuwa unakaribia toka nirudi.je hili linawezekana?
Baada ya mda kupita juzi ameenda kupima tena hospitali na kuambiwa kuwa ana ujauzito wa wiki 30 ambapo kwa mahesabu yangu wiki 30 nyuma inaangukia mwezi wa 11 katikati...je hapanimebambikiwa au wadau hizi wiki huwa zinahesabiwa vipi?. Naombeni maoni yenu wadau
 
Mi nasikia uvivu kuhesabu baba. Muamini tu ni mkeo, asingekuchakachulia bana! Angeweza kutoa hiyo mimba na wala usijue.
 
kwa kawaida week kwenye utrasound huwa zinatangulia kama two weeks mbele na hata jinsi ya kuhesabu wewe ukihesabu utaona ni two weeks lkn madaktari watakwambia ni five weeks, na week inaanza kuhesabiwa from the day of last menstration period, so kwa mujibu wa maelezo yako naona kama huyo kijacho ni kwako kabisaaaaaa, wala usitie shaka.
 
Ahsante sana mdau king'asti kwa mawazo yako na kwa ushauri wako

Ni ngumu kukadiria mimba ina umri gani siku za kwanza, huwa tunabahatisha kwa kuhesabu siku ya mwisho ya bleeding. Hiyo itakuwa yako ila haijatimiza siku thelathini ni chini ya hapo.
 
Mmmh 30 weeks ni sawa na miezi 7.5 rewind back yaani hiyo mimba imeingia late 11. Lakini saana nyingine makisio yanaweza kuwa +/- 2 weeks.

Weka imani mtoto wako ikizidi si atazaliwa chukua DNA
 
kwa kawaida week kwenye utrasound huwa zinatangulia kama two weeks mbele na hata jinsi ya kuhesabu wewe ukihesabu utaona ni two weeks lkn madaktari watakwambia ni five weeks, na week inaanza kuhesabiwa from the day of last menstration period, so kwa mujibu wa maelezo yako naona kama huyo kijacho ni kwako kabisaaaaaa, wala usitie shaka.

Pia akiwa na mashaka zaidi, baadaye anaweza kuja kufanya DNA test, lakini awe mwangalifu maana anaweza kuleta ugomvi na hali ya kutoaminiana kama atalihandle suala hili vibaya au hatakuwa na ushahidi wa kimazingira wa kutosha ...!
 
Ahsanteni sana wadau wote kwa mawazo na ushauri wenu na kwa kunipatia majibu ya nilichokiuliza.
 
Hiyo pesa ya kuja na kurudi Bongo kila mara ingetosha kumleta na kuka na mama majuu na yeye aoshe macho. Na kama ungekuwa naye hapo ulipo yote hii ya kuhisi/kutokuaminiana na kupoteza muda kuuliza maswali ya kiuchunguzi kusingekuwepo.
 
Jamani mbona unawasiwasi au na wewe pia unaiba? wanasema kitanda hakizai haramu na wala hujui nani atakusaidia kukushikia fimbo ukizeeka muachie mungu au muombe mungu kwa sana kama unawasiwasi na jibu utalipata....
 
ni kwamba nipo nje ya nchi kimasomo yapata miaka miwili sasa na nimeoa.huwa narudi kila baada ya mda fulani ili kutoa huduma kwa familia na kuepusha vishawishi kuingilia ndoa yetu. Mara ya mwisho nilirudi mwezi wa 12 tarehe 13 mwaka jana 2012. Kufika mwezi wa kwanza tarehe 5, yaani wiki 3 tu baada ya kurudi mke wangu akalalamikia tumbo kuuma baada ya siku kama 4 alienda kupima na kuambiwa kuwa ni mjamzito, ndo mwezi ulikuwa unakaribia toka nirudi.je hili linawezekana?
Baada ya mda kupita juzi ameenda kupima tena hospitali na kuambiwa kuwa ana ujauzito wa wiki 30 ambapo kwa mahesabu yangu wiki 30 nyuma inaangukia mwezi wa 11 katikati...je hapanimebambikiwa au wadau hizi wiki huwa zinahesabiwa vipi?. Naombeni maoni yenu wadau

Kaka, ukiona manyoya ujue keshaliwa!Pole sana, ila we lea tu huyo mtoto kwa moyo wote isipokuwa siku akija mtu na kudai kuwa ni mtoto wake hapo nakuruhusu, piga hadi azimie ila usiue tu
 
usipate pressure sana wakati mwingine clinic za hapa bongo zinakosea kutabiri, inaweza ikawa ki ukweli ilikua ni mwezi wa 12 kipindi ambacho we umerudi. ila kua mwangalifu unaweza lea mwana si wako maana wanawake wa kibongo bana
 
ni kwamba nipo nje ya nchi kimasomo yapata miaka miwili sasa na nimeoa.huwa narudi kila baada ya mda fulani ili kutoa huduma kwa familia na kuepusha vishawishi kuingilia ndoa yetu. Mara ya mwisho nilirudi mwezi wa 12 tarehe 13 mwaka jana 2012. Kufika mwezi wa kwanza tarehe 5, yaani wiki 3 tu baada ya kurudi mke wangu akalalamikia tumbo kuuma baada ya siku kama 4 alienda kupima na kuambiwa kuwa ni mjamzito, ndo mwezi ulikuwa unakaribia toka nirudi.je hili linawezekana?
Baada ya mda kupita juzi ameenda kupima tena hospitali na kuambiwa kuwa ana ujauzito wa wiki 30 ambapo kwa mahesabu yangu wiki 30 nyuma inaangukia mwezi wa 11 katikati...je hapanimebambikiwa au wadau hizi wiki huwa zinahesabiwa vipi?. Naombeni maoni yenu wadau

Sijui lakini hali ni tete ikiwa wiki 30 ni siku 180 yaani Januari yote hadi mwisho wa June. Ukichukulia siku 12 ulizokuwa hupo Januari. Lakini inawezekana ni kuwa madaktari hawako sahihi na hizo wiki 30 bali ni hesabu ya kukisia tu.
Mke wangu mimi anasema akiamka asbuhi ya pili basi anajuwa kama goli limetinga! Roho mganga, kama unamwamini mkeo basi mwamini tu!
 
Yaani mkuu kama unatakiwa uwe na uvumilivu na subira basi ni kipindi hichi.Pole kwa majaribu
 
Kwenye sheria za ndoa kuna pressumption kwamba kila mtoto anayezaliwa na wanandoa ni mtoto wa wanandoa hao unless proved otherwise.
 
Back
Top Bottom