Je, nini maana ya kusoma na kuelimika?

mada yako nzuri bt umeitia makoro koro mengi, kitu pekee unapaswa kujua ni kua kusoma na kuelimika ni kuongeza upeo wa maarifa bt upeo huo hauwezi kumzuia mtu kufanya starehe yeyote, HUKO KUSOMA NA KUELIMIKA hakuwezi kuondosha matamanio ya mwanadam ambayo ni nature, matamanio ambayo ndo hua chanzo cha ukosefu wa mwanadam YEYOTE, tizama hata maandiko yameeleza namna mitume walivyokengeuka na kumkosea muumba wao ajili ya natural desire, inshort binadam yeyote bila kujali kasoma au lah huponzwa na matamanio HAYA ambayo ndo hupelekea kukosea OVA
Je kusoma nakuwa mafisadi... Wezi na wahujumu uchumu..

Nayo Ni matamanii?
 
Hebu tuanze na Wewe Kwanza je, Mwenzetu Wewe Umesoma na Kuelimika au kuna 'Kimojawapo' hapo 'umekikosa' na pengine unakijutia mno tu?
 
Je kusoma nakuwa mafisadi... Wezi na wahujumu uchumu..

Nayo Ni matamanii?
mkuu natural desire imetamalaki katika kila jambo, mwanadam anapokuwa na matamanio, yale matamanio ndo huifundisha akili cha kufanya ndo maana majuto huja baadae, fisadi hana tofauti na mwizi or kibaka ambae matamanio yake hua ni kukipata anachokitamani bila kujali yupo sahih au la
 
Inategemea hao wasomi wamesoma nini.

Kukarii kanuni za hisabati na matheory ya physics na kufaulu grades za juu hakukufanyi uache tabia chafu.

Na huwezi ukajua maana ya kusoma na kuelimia bila kumdefine msomi ni nani.

Msomi ni nani?
 
Nikweli hizi data. Nimechukua zaidi kwenye vyombo vya habari na Experience yangu...Wasomi ndo wanabuni namna za kutapeli Watu KILA kukicha...wasomi Wanatumia Elimu zao kuibia wateja na waajari wao katika Mabenki...

Wasomi ndo wapo mstari wa kutaka mafanikio yaharaka...hivyo hula rushwa na wengine wakiishia Jela..

Wasomi wetu kutaka mafanikio ya haraka ndo insababisha kufanya mambo Ajabu..

Lakini Hawa wasomi Somo la Ethics huwa hawalielewi au wanapuuza?
Kuna hoja kwenye bandiko lako zenye maana sana. Elimu uliyoijadili inalenga wanaume zaidi na kuwaacha kando wanawake. Wasomi wengi wanahusika na tuhuma hizi.
Maadili hujengwa nyumbani na wazazi ama walezi. Familia za wasomi hazina muda wa kuketi na watoto kuwalea, huwaachia wasaidizi wa kazi nyumbani.
Wasomi wengi pia ni waungwana sana. Wanasimama mahakamani kusaidia wenye kuelekea kutapeliwa ama kupokwa haki zao na matajiri mbumbu wasio na elimu ya darasani.
Mambo ni mengi yanayosababisha hayo yote yatokee. Kwa ufupi ndiyo maana halisi ya maendeleo ya teknolojia na ya kijamii.
 
Hebu tuanze na Wewe Kwanza je, Mwenzetu Wewe Umesoma na Kuelimika au kuna 'Kimojawapo' hapo 'umekikosa' na pengine unakijutia mno tu?
Mkuuu...nikianza kuweka MAJUTO yangu humu... Itabidi nifungue uzi.. Ila usomi was mtu na kuelimika huonekana kwenye matendo Yake...Sio KWENYE PhD zake..

Ndo Maana wasomi wengi wanakosa ethics kwani hawahusianishi .. elimu na matendo. Wanachojua Ni elimu na pesa ..ukisoma Ni kazi nzuri umetusua...
 
mkuu natural desire imetamalaki katika kila jambo, mwanadam anapokuwa na matamanio, yale matamanio ndo huifundisha akili cha kufanya ndo maana majuto huja baadae, fisadi hana tofauti na mwizi or kibaka ambae matamanio yake hua ni kukipata anachokitamani bila kujali yupo sahih au la
Sasa Kama mtu anamadegree lakini mawazo Yake Ni kuiba na kudhulumu na kunyang'anya... Je hii Elimu yetu inatusaidiaje kuwa msaada katika jamii yetu.

Je kukosa Ethics katika kazi kwa wasomi wengi ...Tena wengi wanasoma hii ethics zafani zao... Je ume elimika
 
Ni sawa Ila umebase kwa wasomi wanaume mbona wanawake wengi wasomi n wadangaji na single mothers elimu yao aijawasaidia.?
 
Sasa Kama mtu anamadegree lakini mawazo Yake Ni kuiba na kudhulumu na kunyang'anya... Je hii Elimu yetu inatusaidiaje kuwa msaada katika jamii yetu.

Je kukosa Ethics katika kazi kwa wasomi wengi ...Tena wengi wanasoma hii ethics zafani zao... Je ume elimika
mkuu kwanza unapaswa kujua kua elimu ni nyenzo ya kiutendaji na wala sio nyenzo ya kudhibiti matamanio ya mwanadam ambayo ni nature, kitu pekee kinachoweza kukusaidia kuyadhibiti walau kwa uchache matamanio ya mwanadam ni malezi na imani hivo usijidanganye kwa kua umesoma maadili ya kazi basi ndo utaepukana na adha za matamanio, sie binadam si wakamilifu hivo hata tujitahidi kuwa wakamilifu abadani hatutoweza hiyo ndio nature yetu, wala kuelimika hakuna uhusiano wowote na matendo yatokanayo na matamanio.
 
Nimekuelewa mkuu
 
Wasomi wengi ni wezi wanaibia makampuni.

Wasomi wengi ni wapiga deal

Wasomi ni watakatishaji fedha

Wasomi Ndo washinda wanabet kwenye kamari

Wasomi Ndo wazinifu na wenye kusifia huu uchafu, kuhalalisha uchepukaji

Wasomi wengi hujaza mabaa na makumbi ya starehe wakilewa

Wasomi wengine hubaka nakusingizia walishindwa kuzuia tamaa za mwili.

Sijasema wasomi wote.

Ila vijana wana mentality ya kutusua maisha bila kujali njia ilimradi awe na gari na nyumba na amiliki pisikali.

Je, msomi bila Maadili binafsi atakuwa na msaada katika jamii Yake?
We upo no ngapu apo au we sio msomi.?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom