Je, nini hasa kimefanya mgao wa umeme kuwa historia nchini Tanzania?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
20,433
2,000
Bado nakumbuka machungu makali tuliyopitia Watanzania mnamo mwaka 2006 enzi za mkwere wakati taifa lilipopitia kipindi kigumu cha mgao wa umeme kuwahi kushuhudiwa katika historia.

Je, nini hasa kimefanyika kukomesha mgao? Au wale waliokuwa wakihongwa kufungulia mabwawa wamestaafu au ni nini? Whats going on?!
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
25,302
2,000
Unajiuliza swali wakati unajua kabisa kuna waratibu wa ule mpango hawapo uraiani muda huu, yule muhindi wa IPTL na yule dingi si wako selo sahivi!

Wamekula nondo mpaka wameisha kabisa...ila nafuu yetu huku moto unawaka full time na ukizima basi ni hitilafu za asili tu sio za kutengenezwa.
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
23,211
2,000
Wakati Ule Biashara Ya Generators Ilikuwa Ya Wakubwa . Kulikuwa Na Kitengo Kazi Yake Kuachia Maji Yasiingie Kwenye Mashine Za Kufua Umeme!🙄😎

Biashara Zao Zinakwenda . Awamu Ya Tano Ikatoa Onyo, Ikipatikana Zamu Umeme Unakatika Sababu Huna, Ujue Wazi Wazi Huna Kazi
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,130
2,000
Umeme miaka ya nyuma ulikuwa unategemea mabwawa ya Mtera, Kidatu, Kihansi na Nyumba ya Mungu peke yake. Ugunduzi wa gesi wakati wa Mkapa na ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi wakati wa Kikwete umefanya Tz isitegemee tena mvua kuzalisha umeme wake.

Sasa tunazalisha umeme mwingi kuliko tunavyohitaji angalau kwa 300MW zaidi. Pia mtandao wa usambazaji umeme mikoani na pia katika miji umeboreshwa sana kipindi cha Kikwete na Magufuli. Siku zijazo baada ya kukamilika kwa mradi wa Stiegler tutakuwa na ziada kubwa ya umeme hasa kuanzia mwaka 2023 kwa kipindi fulani tutatafuta tumwuuzie nani umeme, lakini kuanzia 2027 tunaweza tukaanza tena kutafuta namna ya kuongeza uzalishaji wa umeme.
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
1,967
2,000
Ile ilikuwa Hujuma mkuu haswa ya Hizi IPPL ili wafanye biashara ya kuwauzia tanesco umeme na biashara ya generators pia ifanyike ila baada ya mzee kuingia aliamua ku deal nao perpindicular ndio mana unaona saivi mgao ni historia na wanaopata blackout ndogondogo wako well informed na zinatokea kwa sababu ya swala la planned maintenance
 

Okwanyo58

JF-Expert Member
May 3, 2020
1,500
2,000
Umeme miaka ya nyuma ulikuwa unategemea mabwawa ya Mtera, Kidatu, Kihansi na Nyumba ya Mungu peke yake. Ugunduzi wa gesi wakati wa Mkapa na ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi wakati wa Kikwete umefanya Tz isitegemee tena mvua kuzalisha umeme wake. Sasa tunazalisha umeme mwingi kuliko tunavyohitaji angalau kwa 300MW zaidi. Pia mtandao wa usambazaji umeme mikoani na pia katika miji umeboreshwa sana kipindi cha Kikwete na Magufuli. Siku zijazo baada ya kukamilika kwa mradi wa Stiegler tutakuwa na ziada kubwa ya umeme hasa kuanzia mwaka 2023 kwa kipindi fulani tutatafuta tumwuuzie nani umeme, lakini kuanzia 2027 tunaweza tukaanza tena kutafuta namna ya kuongeza uzalishaji wa umeme.
Safi kabisa Mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom