Je, nini hasa huvutia wageni kwenda kuuona mlima Kilimanjaro kwa upande wa Kenya badala ya Tanzania?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,059
40,722
Kuna baadhi ya wadau walifikia hatua ya kusema tuweke pazia kubwa mlima Kilimanjaro kama la dirisha ili kuzuia usionekane bali tu kwa kutokea upande wa Tanzania, ila hicho kitakua kituko.

Sasa tutafakari, kama ni ndege kubwa za kuketa watalii kwa direct flights tumeshanunua, kama ni kiwanja kikubwa cha ndege terminal 3 tumeshazindua, kama ni mahoteli ya kulala tunayo, kama ni kivutio kipo kwetu, shida iko wapi?

Tujadili chanzo cha watalii kufosi kuupanda na kuuona mlima huu wakitokea Kenya, kama tuna sera mbovu tuambiwe, tunakosea wapi?

Hivi vitu vinachanganya sana na kutia hasira, je marketing strategy yetu ni mbovu, je baketi ya matangazo ni ndogo, tatizo nini? Tunakwama wapi?

D4327E13-94D1-4029-9A06-4A1342B94EA7.jpeg
61C84BAF-0FA0-4622-8DB7-F3117C3FE1E3.jpeg
DAEDA6FC-FE2F-43E5-A68C-04181D80E282.jpeg
 
Kupanda mlima kupitia Kenya haipo Mkuu Kwasababu huo ni mlima upo Tanzania

Upande wa Tanzania mlima kwa masaa mengi hufunikwa na mawingu kuliko upande wa kenya
 
Mlima ulikuwepo kabla ya ,,nchi” za TZ/Ke, na ni swala la Jiofrafia, ukiwa upande wa Kaskazini Mlima unaonekana vizuri zaidi, lkn unataka kuleta drama hata kwenye hilo? Yoyote ansyepanda Mlima ni lazima aje TZ na hakuna anayefunga safari kuja Ke eti kuangalia Mlima bali hiyo huwa by the way, sasa unataka kuwakataza Wakenya hata wasiuangalie Mlima? Unataka wakiuona waangalie pembeni? Ml uko 100% kijiografia TZ, na kila anayepanda ni lazima aje kwetu, sasa kama hilo bado halitoshi basi una matatizo, ...
 
Mlima ulikuwepo kabla ya ,,nchi” za TZ/Ke, na ni swala la Jiofrafia, ukiwa upande wa Kaskazini Mlima unaonekana vizuri zaidi, lkn unataka kuleta drama hata kwenye hilo? Yoyote ansyepanda Mlima ni lazima aje TZ na hakuna anayefunga safari kuja Ke eti kuangalia Mlima bali hiyo huwa by the way, sasa unataka kuwakataza Wakenya hata wasiuangalie Mlima? Unataka wakiuona waangalie pembeni? Ml uko 100% kijiografia TZ, na kila anayepanda ni lazima aje kwetu, sasa kama hilo bado halitoshi basi una matatizo, ...
Sawa, tufanyeje basi wawe wanafikia moja kwa moja Tanzania?
 
Katika hilo suala la kupanda mlima kutokea Kenya sina hakika maana mlima upo ndani ya mipaka ya Tanzania hivyo ni lazima kwanza uingie Tanzania.

Kuhusu nini kifanyike watalii wafike moja kwa moja Tanzania, basi wafanye yafuatayo:-

Zitengenezwe Direct Flights za kutoka-kwenda maeneo muhimu mfano Amsterdam, London, Berlin, New York, Beijing, Ottawa, Los Angeles, Johannesburg, Dubai, Rio de Janeiro, Paris, Madrid, Rome, Lagos to Kilimanjaro moja kwa moja.

Waanze kwa kufanya promotion kupitia "Must Hit - P - B" ikiwa ni kutumia Television/Radio za kimataifa za nchi zenye walengwa wengi. Mfano, Tumia Sky Sports, BT Sports, CHF1, Canal, BeIN kipindi cha Premier League na league nyingine barani Europa.

Kutoa udhamini kwa mashindano makubwa kwa kutumia brand husika mfano, Visit Tanzania! Dhamini US Open, Shanghai Marathon, EFL Cup and Co. Kuhakikisha hamtoki katika midomo ya watu

Tumia watu wenye ushawishi na wafuasi wengi zaidi, mkamate J Balvin, Hamilton, Beyonce wapige propaganda matokeo yake utayaona wazi wazi.

Tumia Divide and Rule, nenda Nairobi to Mombasa nunua Billboards zote za barabarani na majengo makubwa weka Visit Tanzania, Climb Kilimanjaro, See Sanzibar, Experience Serengeti, You Must See Burigi-Chato, Have a Ride in Saadani and co.

Matokeo lazima yapatikane!.
 
Acha wivu we jamaa kwani wakifikia kenya wewe unateseka nini wakitaka kuupanda lazma wavuke mpaka kuja Tanzania na wanatumia si chini ya siku tano wakiwa nchini maana yake wanaspend wakiwa kwetu tatizo liko wapi hapo BTW wakenya ni jirani na ndugu na member wa EAC tatizo liko wapi wakifaidika japo kwa kuwapokea wageni wetu wanaokuja kupanda mlima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom