Je nini asili au chanzo cha misemo hii kutumika?

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Kuna baadhi ya misemo inanitatiza, lakini naamini hapa kuna wajuzi wa lugha, ya Kiswahili ambao watanipatia msaada.
Ninachotaka kujua, Je nini asili au chanzo cha misemo hii kutumika?

Misemo yenyewe ni hii ifuatayo:

Haikufua dafu (Msemo huu hutumika zaidi pale mtu anapojaribu kitu kikashidikana, kwa mfano mtu anaweza kuumwa akanywa dawa fulani kisha ikashindwa kufanya kazi, anaweza kusema nimekunywa dawa Fulani lakini haikufua dafu-Tafsiri ni yangu)

Mungu sio Athumani (Huu msemo nao hutumika pale mtu anapokuwa amefanikiwam katika jambo ambalo hakulitarajia-Tafsiri ni yangu)

Hamadi Kibindoni (Msemo huu hutumika pale mtu anapokuwa amepata bahati ya kuokota kitu aua kupata kitu-Tafsiri ni yangu)

Kasimama pale kama mzungu wa reli (Msemo huu unatumika pale mtu anaposimama mahali muda mrefu bila kusogea, na ndo huambiwa kuwa amesimama kama mzungu wa reli-Tafsiri ni yangu)
 
Hii inamaanisha kuwa Mungu anauwezo wa hali ya juu,haufanani na wa binadamu!!
 
Mzungu wa reli.......wakati reli ya kati inajengwa wasimamizi walikuwa wajerumani,waliweza kusimama muda mrefu bila kukaa wakiwaangalia watu wakichapa kazi, ili kuona kazi inafanyika
 
Kufua dafu ni kufanikisha jambo hata likafauru,aghalabu jambo gumu,haikufua dafu - ni kinyume chake yaani kushindwa kufaulisha

.................................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Back
Top Bottom