Je, nimuomba msamaha au nikaushe kuonesha ndio ukidume na kufuatilia matendo ya mke wangu?

Hicho
Si unaona wanavyoshauriana hapa wanamjaza mwenzao huku ndoa inateketea. Hamna kitu kinaharibu mahusiano kama Ego, maana am sure hadi jamaa amekuja kuomba ushauri hapa basi hiko kitu kimemuuma sana ila ndio 'uanaume' nao umeshika hatamu.

Kwa wanawake siku zote tunafundishwa kujishusha na ndoa nyingi ukifatilia utaona zinadumu sababu ya uvumilivu wa mwanamke. Pole dear ila jitahid utimize wajibu wako tu vizuri kama mke mwenyewe atajirudi tu.

Mkuu kabwinyola mradi umetambua kosa lako na kwa afya ya ndoa yako muombe tu msamaha huyo ni mkeo, na utaona jinsi atakavyofurahi na amani itarudi ndani ya nyumba na wala hawezi kukudharau.
Hicho ndicho ninachofanya kuplay part yangu as a woman no way out
 
Huyo mke wake mtarajiwa kamzidi sana akili na pia yeye badala ya kuchunguza anaishia kuuliza uliza. Tafuta ushahidi amwache huyo mwanamke si mwaminifu

Hapo anajilaumu anaona kakosea saba baada ya kupitia Cctv camera na kumuuliza mlinzi wakati alishapiga simu hazikupokelewa kabla. Nikijarib kuunganisha matukio naona kabisa jamaa kasalitiwa ila bado anaona amekosea
 
Habari za asubuhi

Week iliyopita nilisafiri nje ya Mkoa wa DSM, nikamucha mchumba wangu, (Mke mtarajiwa) huko. Weekend akaniomba kwamba anaenda kutembea hivyo ana hamu ya kutoka out, nikasema sawa nikampa mpaka nauli na hela ya kunywa nikamsihi aende maeneo ambayo ingekuwa rahisi kummonita, kupitia vyanzo vyangu mbali mbali.

Akaenda alivyofika tukawasiliana vema, akaanza kunywa, nikamwambia akilewa achukue bajaji aende nyumbani. Akalewa kweli japo si sana akachukua bajaji akaondoka. Nikapewa habari na mwananke fulani kwamba vipi mkeo mbona namuona hapa? We ndio umemruhusu? Nikasema hapana, ili nisikie jibu linalofuata. Akasema yuko na Mr xxxx na wako very close.

Nikasema powa, nikamuuliza akasema tena wameondoka wote kwa gari muda si mrefu. Nikampigia mke wangu mara saba simu hapokei nikapiga tena video call hapokei, nikajua kama kalewa huwa hapokei hata simu, lakin nikajiuliza kwanini hajaniambia kwamba angalau kafika nyumbani, mawazo yakaanza kunijia kichwani kwamba huyu atakuwa ukweli kachepuka na huyo mtu.

Nikawaza sana, asubuhi na mapema akanipigia kwamba kafika usiku sana na kapiga simu mara kadhaa haikupatikana, nikawaza mbona nilikuwa hewani, lakin nikaamua tu kuendelea kumpeleleza yule mwanamke akasema na sasa hivi karudi naye yule jamaa wamekaa wanakunywa, hapo ni Jumapili. Nikapiga simu mke akapokea akasema anajiandaa kwenda kanisani, nikakausha ila nikaumia.

Ikabidi nifunge safari kurudi Dar, nikaenda Nyumbani bila kumwambia mke nikamkuta pale kibarazani amekaa na mdogo wake, nikaingia ndani kwa jazba, nikaanza kumuuliza mke wangu juzi alipokuwa na hakurudi nyumbani.

Akapanik naye akasema wapi, nikamwambia na aliyekuwa naye akasema si ukweli katika kulazimishana aseme ukweli nikamnasa kibao akalia kwa uchungu, bahati nzuri hata umpige mke wangu uwa si wa kunitukana wala kupiga matusi, akajifungia akalia, akaja kwa magoti mbele yangu nimweleze habari nilipozipata na tuthibitishe.

Nikamwambia aliyekuwa naye, akasema basi twende kwake tumuulize. Nikakataa akasema twende umuonye tu angalau kwamba sitaki mazoea na mke wangu kama umejiridhisha kweli. Nikiwa na hasira kali, nikamfukuza mbele yangu nikitamani kumchapa tena.

Nilikaa bar moja jana nikaamua niseme sasa ngoja nimface huyo mwanamue nimweleze ukweli. Nikafunga safari nilipofika kwake nikaambiwa ana siku kadhaa yuko hospitali alianguka na pikipiki ana kama siku 5 nyuma, sikuamini nikaamua kwenda hospital kumuona alikuwa kweli ana P.O.P

Niliporudi kwangu nikaendelea kukausha mbele ya mke, nikiendelea na uchunguzi. Nikamuulizaa ulitoka bar kule saa ngapi, akasema saa 7 usiku, na ukaelekea wapi akajibu hapa nyumbani uliletwa na nani akasema bajaji. Nikakausha nikaenda kumuuliza mlinzi akasema yes saa saba na nusu mpaka saa nane kuna bajaji siku fulani iliingia ndani na kutoka.

Nikaenda control room ya nyumba tunazokaa kuna CcTv camera nikaangalia kweli bajaji ilirudi na Mke alishuka akiwa amevaa mavazi fulani. Nikamuuliza je, Jumapili ulikaa wapi, akasema niliendaka kanisani kusali na nilisali na fulani na fulani na kwenye Jumuiya niliwasilisha mchango wetu kwa Muinjiristi.

Nikapeleleza ni ukweli alienda huko. Sasa nimegundua nimemtuhumu visivyo na ameonesha heshima kubwa kwangu. Je, nimuombe msamaha au nifanye nini kuonesha nilimkosea, au nisiombe msamaha maana nilikuwa natimiza wajibu wangu wa kumlinda mke? Tatu yule alonipa habari ni wa sehemu fulani amelewa sijui nimwambie
Ni aibu ni aibu Dunia hii kuwa na wanaume wa Dizaini yako...Roho imeniuma imeniuma sana utadhani hayo ametendewa mke wangu.

Nimeoa kwa zaidi ya miaka 12 iliyopita sijawahi na sitawahi kumgusa mke wangu eti kumpiga kwa sababu yoyote ile..hapana...
Kama ni makosa kanikosea mengi sana..mapungufu anayo mengi sana lakini nikikumbuka na mapungufu yangu na makosa mengi ninayomkosea na ananivumilia...aisee hapana siwezi kufanya huo upumbavu wa kupiga mke never ever eee Mungu nisaidie.

Ni mwanaume gani usiye na haya unaeendekeza ujinga wa kuruhusu mtu baki wa nje eti akupe habari za mkeo???
Upo sawa kweli..yaani habari za mahusiano yenu ya ndoa umruhusu mtu mwingine ayazungumzie huo ni uanaume kweli???

Humjui mkeo kweli mpaka upokee maneno kutoka nje???
Hujiamini kiasi hicho??

Inaonekana una mapungufu mengi sana na matendo yasiyofaa ndio maana hujiamini..ungekuwa okay trust me usingethubutu kupoteza muda na Kuhatarisha ndoa kisa eti ukisafiri tuu basi lazima eti umweke mke kwenye Rada..aiseee..
Nisamehe sana kaka kwa lugha kali niliotumia nisamehe sana ila nimeumia mno mno eti kumwomba msamaha unasubiri uje uulize huku kweli..ni dhambi na uonevu mkubwa sana

Unapaswa uombe uombe msamaha kwake na toba kwa Mungu wako..

Vinginevyo unakaribisha mabalaa huko mbele kwenye maisha yako...kwenye kazi zako..biashara zako..ndugu na Watoto wako..uonevu kwa Innocent ni jambo baya mno..halafu unagundua kosa unajikausha mpaka muda huu kweli..

Utajikuta na wewe unapata majanga ya kusingiziwa kazini hata kufukuzwa kazi..kusingiziwa kesi..kubambikiwa tuhuma za kutisha..hata kuishia jela kwa kuonewa kosa usilofanya..hata wenye mamlaka wakibaini huna kosa umesingiziwa hutaachiwa nakwambia...mioyo yao itafungwa wasikupe haki yako.

Anayenufaika na msamaha sio mkeo ni wewe..upate baraka na amani rohoni..

Niliapa siwezi kumfanyia jambo lolote mtu asiye weza kujitetea ni dhambi na karma itakuhukumu tuu..you will pay one day no matter what..unampiga kwa kumuonea halafu bado anakupigia magoti jamani so painful...na bado huombi msamaha aisee.
 
Siku utakayoomba msamaha Kwa ili jua kuwa kichwa kishaliwa alafu unamruusu vp mkeo akanywe peke yake kama kaimc pombe anger nyumbani na jaribu sana tena Sana mfanye aache maana kupigiwa lazima
 
Kuomba msamaha sio lazima upige magoti mkuu,waweza rudi nyumbani na zawadi ndogo ndogo ukampa ikisindikizwa na maneno machache tuu (yameisha mke wangu, usinune). Au ukampea zawadi chumbani ukaongea naye maneno mazuri ukapiga pipe zako fresh kila kitu iko poa.

Mwanamke mpe tuu faraja ya moyo usiombe msamaha moja kwa moja. Na kuwa makini na mke wako chunguza unavyoweza.
Ni lazima kuomba msamaha Utamke au umwandikie hata sms..zawadi sio msamaha..tuache roho nguvu zisizo na tija..kusema nisamehe mke wangu maneno mawili au moja yana gharama gani kuliko kupoteza muda na fedha za kutafuta zawadi??zawadi zije kama malipizi baada ya kuomba msamaha...tusikwepe wajibu wapendwa..ebu wanaume tukishinde kiburi kisicho na faida yeyote..umekosea sema I'm sorry kwisha..sio kuzunguka mbuyu kwa visababu visivyo na kichwa wala miguu...
Mbona wengine tukikosea huomba msamaha na upendo huongezeka mara dufu.
 
Mke anakaa Bar mpaka saa 7? Mke? Mke ni Mama wa watoto, ni Mlevi! Haya ndo maandalizi? Kweli usioe kwanza! Ngoja ukue!
Na akiowa aisee ameingia kwenye tanuru mwenyewe yani pombe Hadi saa7 na yeye ayupo Aya Bana ulitoa kibali cha kudinyiwa
 
Mwanamke yupi huyo asiyepigwa? Hawa hawa wa Kijichi au wa masaki mzee??
Jishushe uombe msamaha kama umemkosea mkeo...kumbuka huyo ni mkeo, mwandani wako, laazizi wako....kingine mwananmke hapigwi shekhe! Omba msamaha haraka!
 
Ni aibu ni aibu Dunia hii kuwa na wanaume wa Dizaini yako...Roho imeniuma imeniuma sana utadhani hayo ametendewa mke wangu.

Nimeoa kwa zaidi ya miaka 12 iliyopita sijawahi na sitawahi kumgusa mke wangu eti kumpiga kwa sababu yoyote ile..hapana...
Kama ni makosa kanikosea mengi sana..mapungufu anayo mengi sana lakini nikikumbuka na mapungufu yangu na makosa mengi ninayomkosea na ananivumilia...aisee hapana siwezi kufanya huo upumbavu wa kupiga mke never ever eee Mungu nisaidie.

Ni mwanaume gani usiye na haya unaeendekeza ujinga wa kuruhusu mtu baki wa nje eti akupe habari za mkeo???
Upo sawa kweli..yaani habari za mahusiano yenu ya ndoa umruhusu mtu mwingine ayazungumzie huo ni uanaume kweli???

Humjui mkeo kweli mpaka upokee maneno kutoka nje???
Hujiamini kiasi hicho??

Inaonekana una mapungufu mengi sana na matendo yasiyofaa ndio maana hujiamini..ungekuwa okay trust me usingethubutu kupoteza muda na Kuhatarisha ndoa kisa eti ukisafiri tuu basi lazima eti umweke mke kwenye Rada..aiseee..
Nisamehe sana kaka kwa lugha kali niliotumia nisamehe sana ila nimeumia mno mno eti kumwomba msamaha unasubiri uje uulize huku kweli..ni dhambi na uonevu mkubwa sana

Unapaswa uombe uombe msamaha kwake na toba kwa Mungu wako..

Vinginevyo unakaribisha mabalaa huko mbele kwenye maisha yako...kwenye kazi zako..biashara zako..ndugu na Watoto wako..uonevu kwa Innocent ni jambo baya mno..halafu unagundua kosa unajikausha mpaka muda huu kweli..

Utajikuta na wewe unapata majanga ya kusingiziwa kazini hata kufukuzwa kazi..kusingiziwa kesi..kubambikiwa tuhuma za kutisha..hata kuishia jela kwa kuonewa kosa usilofanya..hata wenye mamlaka wakibaini huna kosa umesingiziwa hutaachiwa nakwambia...mioyo yao itafungwa wasikupe haki yako.

Anayenufaika na msamaha sio mkeo ni wewe..upate baraka na amani rohoni..

Niliapa siwezi kumfanyia jambo lolote mtu asiye weza kujitetea ni dhambi na karma itakuhukumu tuu..you will pay one day no matter what..unampiga kwa kumuonea halafu bado anakupigia magoti jamani so painful...na bado huombi msamaha aisee.
Umeandika kama unaongea na mwanao embu lala kwanza uamke alafu uoge kabisa
 
Umeandika kama unaongea na mwanao embu lala kwanza uamke alafu uoge kabisa
Nisamehe kwa kukukwaza ndugu..sio lengo wala nia yangu..but katika maisha lifanye jambo kama wewe ndio ulietendewa..mf kusingiziwa na kupigwa ndio wewe umefanyiwa..na mtu au mamlaka yoyote yenye nguvu kuliko wewe..natanguliza samani tena na tena...maana ndicho tunachokijadili hapa kumwomba msamaha uliemkosea kwa kumsingizia..
 
Na akiowa aisee ameingia kwenye tanuru mwenyewe yani pombe Hadi saa7 na yeye ayupo Aya Bana ulitoa kibali cha kudinyiwa
Kaka ukichunguza vizuri utagundua ndio life style yao..kwake yeye inaonekana haoni tatizo huyo mke wake kunywa tena kasema akilewa achukue bajaji that means wanajuana na wameridhiana aina hiyo ya maisha..tena alikwenda kwa kibali cha mume na fedha kapewa.
 
Mkuu wanawake hawalindwi kwa hiyo style uliyotumia, wanawake wanahitaji trust zaidi.
Huyu mwanamke alokupa huo umbea ni wa kuanza nae akueleze kwa nini alisema uongo, lengo lilikuwa nini??

Ila mkuu inakuwaje unamruhusu mchumba wako aende bar hadi saa 7 usiku tena peke yake?? Hata kama angekuwa na marafiki zake bado huo muda sio rafiki.

Mwanaume kuomba msamaha hakumwondolei uanaume wake, it makes him more human! Neno samahani lina maana kubwa sana for both sides, jishushe kama unampenda huyo mwanamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wala hamna uongo hapo jamaa kagongewa na huyo mwanamke hamfai
 
Ni lazima kuomba msamaha Utamke au umwandikie hata sms..zawadi sio msamaha..tuache roho nguvu zisizo na tija..kusema nisamehe mke wangu maneno mawili au moja yana gharama gani kuliko kupoteza muda na fedha za kutafuta zawadi??zawadi zije kama malipizi baada ya kuomba msamaha...tusikwepe wajibu wapendwa..ebu wanaume tukishinde kiburi kisicho na faida yeyote..umekosea sema I'm sorry kwisha..sio kuzunguka mbuyu kwa visababu visivyo na kichwa wala miguu...
Mbona wengine tukikosea huomba msamaha na upendo huongezeka mara dufu.

Sikufuzwa hivyo mkuu, na iyo njia imenisaidia sana so kikubwa mleta mada angamue ipi kwake ni bora. Mwanamke anaitaji faraja na kudhaminiwa
 
Sikufuzwa hivyo mkuu, na iyo njia imenisaidia sana so kikubwa mleta mada angamue ipi kwake ni bora. Mwanamke anaitaji faraja na kudhaminiwa
Upo sahihi ndugu..mengi tunayoyafanya ni matokeo ya athari za kimazingira..kitamaduni..imani..malezi na nk..hata mimi nimetoka kwenye jamii hizo hizo..ndani ya familia ndio kabisa..Baba ni Baba..kwenye ukoo ndio tumekuzwa kujitambua na kujipambanua uanaume wetu...lakini kadiri nilivyozidi kujitambua..nikaanza kuchuja which is best for my life.

Mengi ni dhana tuu za kipuuzi tulizopandikizwa ambazo zinatuathiri sana sisi mwenyewe kuliko tunaowadhania kuwa tunawakomoa..

Mimi nimemtengeneza my wife kuwa my very very best friend...yaa ni rafiki haswaa...mbali ya utofauti mwingi tulionao huwa najikaza na kupuuza na kujikita kwenye mazuri yake...tumetoka makabila tofauti yasio endana kabisa kwa mengi...lakini tuka hamonize yote na kuunda kabila letu wenyewe tunaloliishi.

Namsikiliza sana na kumsapoti..tukichanganya akili zake ..maarifa yake...hekima zake na zangu yaani maisha yanaenda balaaa..safi kabisa..mzee mwenyewe anashangaa mno maana aliniona mwanzo kama mwanaume mjinga mjinga sana naye endekeza mwanamke.
Lakini leo ndio kila leo nikumsifia mkwewe kuwa ni mkwe bora kuliko wote.

Maana kama ni maendeleo tulipo toka na tulipo na tunakoelekea sio haba..waheshimuni wanawake..wapeni nafasi..shikamaneni..acheni mifumo dume but upendo uwe hakimu wenu..mtaiona mbingu Duniani..
 
Back
Top Bottom