Je, nimuomba msamaha au nikaushe kuonesha ndio ukidume na kufuatilia matendo ya mke wangu?

kabwinyola

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
560
1,000
Habari za asubuhi

Week iliyopita nilisafiri nje ya Mkoa wa DSM, nikamucha mchumba wangu, (Mke mtarajiwa) huko. Weekend akaniomba kwamba anaenda kutembea hivyo ana hamu ya kutoka out, nikasema sawa nikampa mpaka nauli na hela ya kunywa nikamsihi aende maeneo ambayo ingekuwa rahisi kummonita, kupitia vyanzo vyangu mbali mbali.

Akaenda alivyofika tukawasiliana vema, akaanza kunywa, nikamwambia akilewa achukue bajaji aende nyumbani. Akalewa kweli japo si sana akachukua bajaji akaondoka. Nikapewa habari na mwananke fulani kwamba vipi mkeo mbona namuona hapa? We ndio umemruhusu? Nikasema hapana, ili nisikie jibu linalofuata. Akasema yuko na Mr xxxx na wako very close.

Nikasema powa, nikamuuliza akasema tena wameondoka wote kwa gari muda si mrefu. Nikampigia mke wangu mara saba simu hapokei nikapiga tena video call hapokei, nikajua kama kalewa huwa hapokei hata simu, lakin nikajiuliza kwanini hajaniambia kwamba angalau kafika nyumbani, mawazo yakaanza kunijia kichwani kwamba huyu atakuwa ukweli kachepuka na huyo mtu.

Nikawaza sana, asubuhi na mapema akanipigia kwamba kafika usiku sana na kapiga simu mara kadhaa haikupatikana, nikawaza mbona nilikuwa hewani, lakin nikaamua tu kuendelea kumpeleleza yule mwanamke akasema na sasa hivi karudi naye yule jamaa wamekaa wanakunywa, hapo ni Jumapili. Nikapiga simu mke akapokea akasema anajiandaa kwenda kanisani, nikakausha ila nikaumia.

Ikabidi nifunge safari kurudi Dar, nikaenda Nyumbani bila kumwambia mke nikamkuta pale kibarazani amekaa na mdogo wake, nikaingia ndani kwa jazba, nikaanza kumuuliza mke wangu juzi alipokuwa na hakurudi nyumbani.

Akapanik naye akasema wapi, nikamwambia na aliyekuwa naye akasema si ukweli katika kulazimishana aseme ukweli nikamnasa kibao akalia kwa uchungu, bahati nzuri hata umpige mke wangu uwa si wa kunitukana wala kupiga matusi, akajifungia akalia, akaja kwa magoti mbele yangu nimweleze habari nilipozipata na tuthibitishe.


Nikamwambia aliyekuwa naye, akasema basi twende kwake tumuulize. Nikakataa akasema twende umuonye tu angalau kwamba sitaki mazoea na mke wangu kama umejiridhisha kweli. Nikiwa na hasira kali, nikamfukuza mbele yangu nikitamani kumchapa tena.

Nilikaa bar moja jana nikaamua niseme sasa ngoja nimface huyo mwanamue nimweleze ukweli. Nikafunga safari nilipofika kwake nikaambiwa ana siku kadhaa yuko hospitali alianguka na pikipiki ana kama siku 5 nyuma, sikuamini nikaamua kwenda hospital kumuona alikuwa kweli ana P.O.P

Niliporudi kwangu nikaendelea kukausha mbele ya mke, nikiendelea na uchunguzi. Nikamuulizaa ulitoka bar kule saa ngapi, akasema saa 7 usiku, na ukaelekea wapi akajibu hapa nyumbani uliletwa na nani akasema bajaji. Nikakausha nikaenda kumuuliza mlinzi akasema yes saa saba na nusu mpaka saa nane kuna bajaji siku fulani iliingia ndani na kutoka.

Nikaenda control room ya nyumba tunazokaa kuna CcTv camera nikaangalia kweli bajaji ilirudi na Mke alishuka akiwa amevaa mavazi fulani. Nikamuuliza je, Jumapili ulikaa wapi, akasema niliendaka kanisani kusali na nilisali na fulani na fulani na kwenye Jumuiya niliwasilisha mchango wetu kwa Muinjiristi.

Nikapeleleza ni ukweli alienda huko. Sasa nimegundua nimemtuhumu visivyo na ameonesha heshima kubwa kwangu. Je, nimuombe msamaha au nifanye nini kuonesha nilimkosea, au nisiombe msamaha maana nilikuwa natimiza wajibu wangu wa kumlinda mke? Tatu yule alonipa habari ni wa sehemu fulani amelewa sijui nimwambie
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,122
2,000
mimi wife nimempa ratiba ambayo anaiishi, atafanya mambo yake yote bt ratiba lazima izingatiwe na akienda kinyume na ratiba ugomvi wake hadi wazazi ndo huamua hii imenisaidia kum-control coz mwanamke haaminiki na ukimpa uhuru zaidi ujue umejitafutia matatizo.

usimuombe samahani kausha huo ndo uanaume
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
12,561
2,000
Kwa taarifa yako umegongewa. Hakuna mtu anayeweza kumzushia yote hayo mkeo mtarajiwa. Kwanza kwa nini mtu anataka kuolewa aanze kutoka out mpk alewe? Na inawezekanaje awe peke yake baa kama mchawi? unachapiwa na umeshindwa kuhusisha akili yako. Baki hivyo hivyo ila nakuambia mie nimeoa mwaka wa 20 sasa, hapo hamna mke mzee
 

gspain

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,776
2,000
Hawa watu bhana wanataka kujifanya wao tu ndio wana mioyo ya kuumia ila sie aah haiumi.
Mume wangu tuna mwezi sasa hayuna maelewano ndani sababu zenyewe za kijinga kanikosea sana heshima na kaishagundua kosa lake ila bado kakomaa tu kuonesha uanaume ila mimi nikimkosea napelekwa mpaka kwa wazee wa kanisa
Ukitaka kumkomesha muombe yeye msamaha kwa kukukosea wewe heshima.

Niliwahi kuwa na mwanamke wa hivi, yaani me nikikosea ye ananiomba msamaha kwamba inawezekana ye hakusimama kwenye nafasi yake kama mwanamke, alijua kunikomesha aisee..
 

Lenie

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
5,976
2,000
Hawa watu bhana wanataka kujifanya wao tu ndio wana mioyo ya kuumia ila sie aah haiumi.
Mume wangu tuna mwezi sasa hayuna maelewano ndani sababu zenyewe za kijinga kanikosea sana heshima na kaishagundua kosa lake ila bado kakomaa tu kuonesha uanaume ila mimi nikimkosea napelekwa mpaka kwa wazee wa kanisa
Si unaona wanavyoshauriana hapa wanamjaza mwenzao huku ndoa inateketea. Hamna kitu kinaharibu mahusiano kama Ego, maana am sure hadi jamaa amekuja kuomba ushauri hapa basi hiko kitu kimemuuma sana ila ndio 'uanaume' nao umeshika hatamu.

Kwa wanawake siku zote tunafundishwa kujishusha na ndoa nyingi ukifatilia utaona zinadumu sababu ya uvumilivu wa mwanamke. Pole dear ila jitahid utimize wajibu wako tu vizuri kama mke mwenyewe atajirudi tu.

Mkuu kabwinyola mradi umetambua kosa lako na kwa afya ya ndoa yako muombe tu msamaha huyo ni mkeo, na utaona jinsi atakavyofurahi na amani itarudi ndani ya nyumba na wala hawezi kukudharau.
 

The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
15,129
2,000
Kama ana nia ya kufanya kweli hata asipo ombwa msamaha atafanya tu
Akifanya kweli hio screnario ingine itategemea na script yake kwa wakati huo

Ila Sasa jamaa kahisi alimshutumu tu na anapaswa kuomba msamaha kiungwana na njia pekee ya kuomba msamaha yeye Kama mume Ni kwa vitendo sio kufungua mdomo wake .

Na pia ujue kuwa jazba na hasira za jamaa zimepa alert huyo mwanamke so no vema ikabaki hivyo kuwa alert akiomba msamaha anaharibu kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom