Je nimpe talaka au nifanyaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je nimpe talaka au nifanyaje

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by majuto, Dec 24, 2009.

 1. m

  majuto Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenzangu anisikii kabisa, amekuwa mbishi umwambii kitu akifanye; anajibizana nami kama watoto,mwana mke wangu ni mchafu sana ina bidi wakati nikichoka nikubali kuwa mchafu kidogo, asafishi nyumba, jiko ni chafu, bafu chafu, ukiweka glass chini sebuleni inaweza kukaa wiki anaipita anaipiga teke na haikoti, si glasi tu kitu chochote, ukinunua vyakula na groceries ukaleta nyumbani anachofanya ni kuyachukua vitu na kutupa ndani ya makabati ukimuhuliza alipoweka kitu ajui. Na akisha weka kitu hakumbuki nini kaweka wapi hata mwaka unapita kitu hakijaguswa mpaka nifanye campeni ya kukagua kila kitu na kuweka nje ili nijue vilipo.
  Fridge ni chafu, haipangwi vitu vinatupwa tu ndani yake bila hata kuoshwa vikitoka kwenye store. Chakula akipika nimemwambia siku nyingi inabidi kuya toa kwenye sufuria na kuweka kwenye makopo madogo ndo yawekwe kwenye fridge. Yeye akisha kula ana acha sufuria hapo hapo juu ya jiko bila hata kufunika na vijiko alivyotumia kuchotea chakula anaweka juu ya jiko hapo alafu anakwenda kulala, uki msema anachukua sufuria anaingiza ndani ya fridge na afuniki ingawa zipo wraping-makaratasi ya kufunika vyakula. Vyombo vina lala hapo kwenye sink mpaka kesho yake asubuhi.

  Afui shuka mpaka ichafuke kweli au umwambie na akifua nguo au mashuka apigi pasi analundika hapo chini au popote pale alafu ana chambua mmoja baada ya nyingine na kupiga pasi akitaka kwenda sehemu alafu baada muda anarudi kuyafua tena unakuta ngua nyingine wala hazija valiwa zinafuliwa tena; Nimejaribu kuongea na kufundisha lakini asikii, aelewi au hajifunzi
  Akilala nimeisha mwambia afunike nywele kwani anaweka dawa lakini afanyi hivyo mashuka na mito yote ina utomvu wa curls, watoto wanashindwa kupumua kwa sababu ya hewa nzito. Nimemnunulia cover ya nywele ya kulala lakini hajui alipo ziweka na ata kama ipo mpaka nimwambie kwa force ndo aweke.

  Nnguo zake zina toa harufu mbaya nimemwambia kwa muda mrefu lakini asikii wala hafanyi jitihada kubadilika. Kupika ndo hajui kabisa anajua kupika chakula cha aina mmoja chakula cha mchuzi. Kupika Kuku wa mchuzi na nyama ya mchuzi hajui kupika hata andazi akipika vhapati utavunja meno ngumu kama jiwe. Nimeangalia kwenye internet siku mmoja nikiamka asubuhi nikapika kama mandazi 60 na yakawa mazuri kama ya mama nitilie na watoto wakayapenda lakini ukimwambia apike tena ingwa nimeandika kila kitu hawezi.Anayo internet 24 hours nyumbani
  Nikitoka nje wala anipokei wala ani tengei chakula mezani labda kama wote tuko nyumbani ndo anapika alafu anaweka chakula mezani.
  Wakati watu wakila yeye akai na watu mezani anakula peke yake, asubuhi namwacha analala wakati nakwenda kazini wala anipikii chai, napika mwenywe. Nawa ogesh watoto kabla ya kuwapeleka shule na kuwa tengea chai. Yeye akiamka anakwenda kwenye nywele za motto ndo anacho jua. Hamsaidii motto na assignment mpaka motto analia nikiingia kuwa mama hanisaidii. Hata kuwasomea watotoneno nalo ni shida nawakuta watoto wana nisubiri niwaombee ili walale yeye wakati huo analala.

  Nimemwambia mke wangu awe incharge wa nyumba ajue matumizi yetu ya kila siku lakini hadi leo hajafanya na hajui tunatumia kiasi ghani au tunalipa bill kiasi gain kwa mwezi hajui
  Nina ka imani kidogo kabla ya kwenda kulala nataka tisome biblia na kuomba lakini yeye kila siku akisha kula yuko kwenye TV mkitaka kuomba yeye anakwenda kulala.
  Sijawahi kumwona mke wangu ameshika kitabu anasoma kitu ambacho ni kibaya sana
  Siku nimetoka kazini ghafla nilisahau kitu nyumbani nikarudi nikakuta amekaa chumbani n a chai niliyo mwandalia Baba yangu anaye tutembelea hajamtolea sukari na kikombe anywe hivyo ikabidi nimpe Baba yangu chai. Kusudi baba asione tunashirikiana kumfanyia ubaya nikamuuliza kwa sauti kabisa kwanini hujampa baba chai?

  Najua Biblia imeandika uache mke kwa Uasherati tu je hii si zaidi ya uasherati?

  Mke wangu afanyi kazi ni mimi ndo naleta kila kitu sasa ni miaka mitano ila naelekea ukingoni. Nilikuwa msafi lakini naelekea kuwa mchafu. Mtoto akitoka shule amwambii akaoghe anamwambia utaoga kesho, dawa akipewa au ya watoto anakunywa mara mmoja tu alafu anatupa hapa mezani – Nifanyaje –Kukwepauchafu nemetoa nguo zangu zote kwenye makabati na kuyafungia kwenye sanduku na nimebadilisha namba ili niwe na nguo hata mmoja ya kutokea, kwani yeye hana nguo ya kutoka zote ni za sokoni na za kutokea
   
 2. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hii ni breaking news. Umeiweka kwenye spostishi
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Bana Eh!! Hiyo peleka kunakohusika huku sio kabisa..Modes saidia hii mutu. Huyo manzi wako kama yuko hivyo? Ulijuanga lini hiyo habari? Si mlikuwanga ati boy and girl friend, hukujua hiyo maneno yote?? acha vuruga kichwa yetu weweeee...
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  majuto
  Junior Member
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Join Date: Thu Dec 2009
  Posts: 2
  Thanks: 0
  Thanked 0 Times in 0 Posts

  Msimlaumu huyu jamaa wandugu, bado ni mgeni sana!


  This story is unnecessarily too long!


  Sisi ni watu wazima na waelewa, na tungekuelewa hata kwa nusu tu ya maelezo yoote uliyoweka!..Naamini hata hivyo si hayo tu anayokufanyia, kuna mengi zaidi ambayo hujayaandika!...

  Pole sana ndugu majuto, lakini kumwacha si suluhisho. Kama unampenda na ungependa tabia yake ibadilike na kuwa njema, basi umsaidie kwa kila hali ili muendeleze maisha yenu ya kawaida.

  Wanasema tabia haina dawa, lakini mi naamini akifundishwa taratibu ataweza kubadilika japo kwa minimum!

  Miaka mi5 bado ni mapema sana kwa ndoa, so still you have a chance to do something.
   
 5. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Pole yako Majuto.
  unajua wanawake namna hii wanatokana na malezi huko kwao na pia hata wewe mwenyewe ulipo anza kumkaribisha kwa home yako hukutaka kujifunza juu yake.
  Nainawezekana kabisa ulikua ni mtu wa kumpeleka kwenye take away everytime akija kwako.
  Kwa mtu aliyezoea kufanyiwa kazi na house girl mpaka chupi yake ndo matatizo hayo.

  Hivyo mvumilie na jaribu kukaa nae chini mzungumze taratibu atabadilika tu.

  Ama uliletewa mke na wazazi wako,kwamba huyu oa la sivyo laana naiwe juu yako!!

  japo intro hukutoa ulimpataje, basi yawezekana makosa makubwa yako kwako hukusoma alama za nyakati toka day one.
   
 6. c

  compressor Member

  #6
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!,
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  AGRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRR!HHHHH
  summary please!namna hii kweli mnatuchosha wachangiaji
   
 8. C

  Chief JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Reminds me of Nairobi...LOL!
   
 9. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huna tofauti na mke wangu ila wangu wangu ananipagawisha acrobatic zake usiku ndio maana hua simsemi kama wewe
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kweli hii kali,Lakini fanya hivi,

  1. Huyo kuna tatizo zaidi ya usafi,labda hujui au hujawa muwazi.Ni psychological problem/matatizo ya akili. ambayo inakimbilia kwenye uzembe,uchafu na uvivu.Mchunguzeujue ana tatizo gani,kisha tafuta wataalamu wa ushauri,wamshauri
  2.Tafuta mama mmoja mwaminifu kanisani,kama akiwa mama mchungaji itakuwa nzuri zaidi,awe anakuja hapo nyumbani na kumpa semina ikiwezekana kwa vitendo.Na wakati mwingine atoke kwenda kuona nyumba za wenzie.
  3.Mtafutie hausigeli au hausiboi
  4.Jina lako la majuto linakufatilia,badilisha.
  5.Vumilia huku ukiendelea kumuelekeza.
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...uliminya jicho moja ulipomchumbia na kumuoa, yakubidi sasa uyafunge yote mawili upate kuishi naye.

  BTW, mapungufu yake yapo ndani ya uwezo wako, ...angekuwa mwasherati tungekuwa tushakuzika.
   
 12. Guyana Halima

  Guyana Halima Member

  #12
  Dec 24, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hajafundwa huyo!!? Kabila gani?? Ni mtoto pekee kwao au wa mwisho?? Pole sana kaka Mjuto!! Nafkiri huo ushauri hapo juu utakusaidia sana ukiutilia maanani!!!
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Kaka Majuto

  Kama ni kweli hiyo ni kali ila kila mtu ana mapungufu yake.. Je kuanzia mnaoana yupo hivi mpaka leo? Mawasiliano yenu mazuri yaani kumwelezea hivi vitu vinavyokukera abadilike au umsaidie kubadilika?
  Isijekuwa unaelezea yote hapa wakati hujafanya bidii zozote za kumrekebisha hapo kwenye mji wenu..
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu upo?
   
 15. KwayuG

  KwayuG Member

  #15
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 14, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  we mwenyewe si ndo ulikula kiapo Mbele ya Mungu kwamba mpaka kifo kiwatenganishe?. nadhani kama ulikuwa umekaa nae kwa muda mrefu ukamsoma vizuri ulifahamu wazi tabia yake kabla hamjaoona.
  Vumilia naye tuu, ila unatakiwa uwe mkali kwake ili akuheshimu na afuate maelekezo yako.
  ukiwa unamwabia mke wangu jamani mbona hujafanya hivi au vile hatakuwa akusikilizi kamwe, mpigishe rigwaride siku moja
   
 16. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Pole sana Mzee. Matatizo kama hayo ni ya kawaida katika ndoa kutokana na tofauti ya malezi na makuzi. ni jukumu lako kutafuta njia muafaka ya kumuelekeza nini cha kufanya, hata ikibidi kuwatumia wataalamu. Atarekebishika.
   
 17. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  We Kapongo (A.K.A Kadoda a.k.a kabeberu)...... hiyo ya kusema "Matatizo kama hayo ni ya kawaida katika ndoa" ndiyo inayotufanya tufe na TAI shingoni. Cha msingi ashirikishe ndugu wa mkewe katika kutatua hili.
   
 18. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Majuto,
  thread hii naona ni ya kweli yamekukuta. Pole sana lakini yaelekea hamkuwa na muda wa uchumba. Kama ulikuwepo basi mlikalia kumegana tu bila kuchunguzana tabia. Unavuna ulichopanda. Anyway pole
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
   
 20. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
   
Loading...