Je nimemjibu jamaa vibaya kuhusu mchumba wangu??

pole sana mkuu,kumbuka kila kitu hutokea kwa sababu. hyo hakuwa wako,wako yupo ushapangiwa na Mungu!

Nashukuru sana charminglady na nAamini hivyo maneno yako yana ukweli.asante sana.kila kitu kinapangwa na kinakuja kwa sababu.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Umefanya VIBAYA!!
Demu alishamwaga Ugali kwa kukukana,
Nawe ungemwaga mboga kwa kumwambia huyo mwanaume mwenzio kua yeye ndio mwizi na we we ndio mmiliki.
Kama una ushahidi mbalimbali juu ya kwamba uhusiano wenu ni wa kitambo zaidi kuliko wa huyo jamaa ungemuonyesha ili azidi kukuamini kua yeye ndio mwizi.
Mwisho wa siku akija kukubali na kuamini kua yeye ndio aliongilia mahusiano yenu akakata kamba ndipo nawe Pia unakata kamba umuache demu anatapatapa.
Jamaa sio m'baya wako hata kidogo, Bali demu. So ungesuka plan ya kumharibia ili ajute kukupotezea muda


Mkuu nashukuru sana nimesoma hii comment nikaanza kucheka mwenyewe,yes ni ushauri mzuri sana ila ile time nilikuwa nimechanganyikiwa sana plus demu alivyofikia na kunipigia simu na kuniambia ongea na bf wangu ndio kabisa nilikuwa sijielewi kabisaaaa,so nikaamua tu kusema wacha nikubali yaishe,ni kweli kabisa kanipotezea mdaaaa mwingi sanaaaa sio kidogo huu mda niliokuwa naye na anafanya mambo ya ajabu ningeshakuwa nimeplan maisha yangu tayari,imeniuma sana,yeah demu ndio amefanya vibaya alikuwa ananificha siku zote hizo. Again thank u sana mkuu wangu

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Safi sana kwa busara ulizozitumia,zinazo washinda wanaume wengi. Usiache hizo busara ziende zake.umemuonesha wewe ni mwanaume.
 
jamani papizo pole! pole sana, i knw it will take tym for u to forget, but beter now kuliko yangekukuta haya kwenye ndoa. wadada wengi wapo kimaslahi zaidi and not real love, oh lord have mercy!


Nashukuru sana ila tatizo angesema mapema ingekuwa afadhali na si kupotezeana muda si ndio??yeah nitasahau tu na nazidi kumuomba mungu kwa kila jambo,yeah wengi wao wapo kima slahi zaidi ndio tatizo kubwa hilo

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
pola sana kaka yangu...mimi binafsi nakupongeza kwa kuwa na ustaarabu na utu wa namna hiyo kwani ni wachache sana wenye uwezo huo. Ok, mimi nakushauri UACHANE kabisa na huyo dada maana atakupotezea muda wako kwa kufikiri labda umepata kumbe hakuna kitu. Pia ninavyojua mambo kama haya, usije kushangaa akakujia tena kukuomba msamaha akishatibuliwa na huyo mumewe mtarajiwa...sidhani hata kama kuna ndoa hapo, utakuja kusema! mimi nakuombea kwa Mungu akujaalie mwanamke mwenye mapenzi ya dhati na busara na hekima kama za kwako, ilui muishi maisha ya ndoa yaliyotawaliwa na furaha, upendo, amani na uaminifu. Inshaalah!
Wakuu naomba msaada,maana leo nimepata drama ambayo sijawahi kuipata,nitaandika inshort tu,actual nilikuwa na mchumba niseme ambayo hivi mwezi wa saba narudi tuliplan maisha na kwenda kwa family,sasa kwa vile tupo mbali tukawa tunawasiliana sana na tukawa tuna share password zetu,basi ikafikia wakati nikaona mambo ya ajabu ajabu mara kachange password nikimuuliza hana sababu again ya kuniambia na attitude akawa anayo na dharau nyingi,hapo hapo tufahamu sijaanzana nae jana wala leo since nipo form 1 mda mrefu sana tupo wote.
Kama 2 months ilifikia akaniambia mimi na wewe basi eti nina wanawake wengi sana nikamuuliza ume prove ninao??akawa hana la kunijibu,nikamwambia ok fine hamna tatizo na maisha mema,sasa week kama 3 zilizopita akaja kuniomba msamaha na kusema nimsamehe me nikamuelewa nikamsamehe coz sikutaka relationship ife hivi hivi nikakaza moyo nikamsamehe.

Lakini tulivyokuwa tunawasiliana nikawa naona kuna somethin wrong sio normal nikamwambia akasema ananipenda sana hamna kitu. Na nimuamini nikamuuliza sasa mbona una tabia za ajabu ajabu anasema ndio nilivyo,basi me nikawa mpole sana na mvumilivu kwa kweli kwanza huwa sipendi kugombana kwa ajili ya vitu vidogo.

Sasa leo hii nimepigiwa simu mchana majira ya saa kumi namsikia mchumba wangu ananiambia kwamba ongea na bf wangu nikamuuliza unasemaje??na wewe ni nani??akanitajia jina lake coz sikuamini kama ni yeye,akasema ongea na bf wangu mwambie kwamba mimi na wewe tumeachana,me nilishasemaga sitokuja kugombana kisa mwanamke.akampa simu jamaaa akawa anawaka vibaya sana nikamwambia kaka calm down sawa wala usijali,akaniambia nimeona sehemu fulani umetumiana message za ajabu ajabu na huyo msichana wewe ni nani??Nikamjibu kwanza hajakuambia mimi ni nani??akasema wewe ndio niambie nikamwambia niulize swali lingine kipindi hicho kichwa hakifanyi kazi,akaniambia huyu ni gf wangu na next week naenda kutoa mahali kwao,nikasema ohhh ok sawa nikamuuliza umeanzana nae lini akasema miaka 2 iliyopita,me nikakauka kimya,akasema basi naomba mawasiliano yaishe na mke wangu nikamjibu wewe ni ndugu yangu na sisi wote ni wanaume so mkuu usijali zaidi tuzidi kuwasiliana sisi wote ni ndugu,nimemjibu kisomi na sikuonyesha kupanic,

Je wakuu wangu kuna mahali nimejibu vibaya??au yule alikuwa mchumba wangu kumbe mwanamke ana mwanaume mwingine kulikuwa na haja ya mimi kugombana na jamaa kwa ajili ya mwanamke??je majibu niliyomjibu kuepusha shari na kumuachia mwanamke nimefanya vizuri au nimekosea??
 
.....papizo pole sana. Shukuru mungu sana, sana, sana kwa hayo yaliyokutokea. Mw'mungu amekuumbulia mnafiki, na sasa umejua rasmi haktwa mkweli kwako.

Niliwahi pata a similar experience 2002....na nakumbuka nilipigiwa simu na kuambiwa 'huyu mimi ni gf wangu, nataka kumuoa'....nami nikamuuliza fiancee wangu, aamue....(akanichagua mimi!)...

Kilichofuatia miaka katika miaka tisa ya mahusiano-saba ya ndoa....ni aheri ningemuachia jamaa hilo zigo. DONT YOU DARE ati kesho au keshokutwa akikurudia na kilio cha msamaha nawe ukakubali kumsamehe. USITHUBUTU kurudiana nae hata kama unampenda vipi!!!! Pse bro...

Sana mkuu wangu kwa kweli amenipa mwangaza maana sikutegemea kabisaaa hata kidogo. Mkuu wangu asante sana na wazo lako nimeliweka kichwani sitoweza kufanya hivyo kabisaaaa na wala sitojaribu kufanya hiyo mistakes ya kurudiana nae hata kidogo, Again nashukuru sana ndugu yangu na wewe pia pole sana tena sana kwa yaliyokukuta kwa kweli.
 
SAFI SANA KAKA ,MIMI KAMA MTU NINAYEPENDA SANA PESA ,CHAKWANZA RUDI KWENYE MASUALA TA ATM BADILI PASSWORD ZAKO WATAKULIZA,
THEN HUYU DADA ATARUDI TU.YOU WILL PROVE ME BEYOND REASONABLE DOUGHT ,TENA WANAUME KAMA NYINYI YOUR WORTH IN THIS WORLD,SASA IYO KISA YAKO IGEUZE MIMI NILISHAFANYIWA HIVYO NA MWANAUME ILA NILIMKOMESHA NILIMWACHA KABISAAAA NA TULIKUWA KWENYE LAST STAGE YA MARRIAGE.NILIMWACHA ALIKUJA MPAKA NA WAZEE NIKAMWAMBIA HAPANA KABISA,MAANA ALIFANYA HIVYO 3TIMES WANAWAKE TOFAUTO NA BORA WEWE ALITUMIA SIMU YAKE ,MIMI ALITUMIA SIMU YA WANAWAKE ZAKE KWA DHARAU ZAIDI NI KITENDO KILICHONIUMA SANA SANA . ALIRUDI KWA MAGOTI ILA nikampa wimbo wa witney hauston
"On My Own"






 
Papizo Nimekugongea LIKE kuonyesha msisitizo maana ulichowaambia kinaitwa Psychological Torture, yaani alitegemea utaumia sana na badala yake ume-reverse maumivu kwake. Alitaka uumie, alitaka akuonyeshe ufahari, lakini plan yake imefail na huo ndio ukomavu ndugu yangu, Hongera sana, In short hio ni mojawapo ya story fupi sana kwene mapenzi.

Nashukuru sana ndugu yangu, yeah nilimuona jinsi alivyoanza kuongea ni kama anataka ugomvi fulani as nimemchukulia demu wake, lakini mimi nikawa mstaarabu na nashukuru mungu sijawa na ugomvi nae na nipo normal now, nashukuru mkuu wangu na ndio hivyo inabidi kumsoma binadamu mwenzako na kujua namna gani jinsi ya ku respond anythin. Nashukuru sana mkuu
 
Mi nataka kuamini kuwa hii ni gia mpya wamekuja nayo wadada...imenitokea hivi karibuni though sio serious kama yako na kwangu ilikuwa ni nyumba ndogo ambayo nilikuwa nayo for 6 months na niliaminishwa kuwa mi ndo stering mwenyewe.Hapa juzi kati nikaona message kuwa ''Tafadhali linda ndoa yako na mi nilinde mahusiano yangu tusiwasiliane tena''.Sikuamini kama yalikuwa ni maneno ya laazizi nyumbba ndogo nikapiga simu akapokea huyo mtawala mpya na kuanza kunipiga mkwara mbuzi kuwa nikae mbali na wake wa ubani other wise atanilipua kwa wife kwani anafahamu anakofanya kazi na ananifahamu vizuri.Nilikata simu nikiwa mpolee na sasa kila mtu akiniangalia mara 2 2 tu nahisi sijui ndo atakuwa jamaa mwenyewe!!!
 
Mkuu kwanza pole kwa yaliyotokea,nilivyoona hapo wewe alikua anakutumia kama ATM na Huyo jamaa yake ndio aliyekua anamkuna kimapenzi so mapenzi yamemzidi na wewe akaona sio muoaji akaona bora aende kwa msela na akupige chini na hela zako hizo hila nakusifu sana kwa uvumilivu.

Mkuu kwa kweli labda alikuwa ananitumia kama ATM ila tatizo me sikuwa na problem coz hatukuanzana jana wala juzi miaka na miaka ndio maana nikawa happy kwa anything namfanyia vile vile sio nilikuwa sio muoaji nadhani ungeipitia hiyo topic ambayo nimeandika ungeona nilichosema....ila nashukuru mkuu na ndio hali halisi ilivyo na matatizo ni kawaida kwenye relationship, Tupo pamoja sana mkuu wangu
 
Pole sana mkuu ila kuna siku atakukumbuka tena wala si nyingi, wengi yamewatokea haya mambo. Congrats for your emotional control
 
U did the right thing mkuu. That being a gentleman, we are defined by our actions esp in hard times, I've upgraded u thou sikujui kwahakika mke mzuri na mwema anakuja upesi on your way.
 
Duh, kama u-true gentleman unapatikana hivo, then I guess I'll never be one of them.
Yaani hiyo kwangu ni dharau moja kubwa ambayo ni ngumu sana kuvumilia. Ee Mungu nisaidie niwe true gentleman maana huu ungekuwa ni mtihani moja mgumu sana asee.
NB: Ni bora angeniambia mapema na sio kufanya kama alivyofanya, hapo I would have done something which she (Not me) would regret for the rest of her misery life.. kudadadek..
Yaani imeniuma as if mimi ndo victim...:A S 12:

Inabidi kuwa mvumilivu sana mkuu maana hasira hasara kwa kweli na ni kweli ni dharau tosha amenifanyia ila mungu anaona, hamna kilichoniuma hapa kama hivi alivyofanya amefanya kitu kibaya sana tena sana, zaidi kilichoniuma ni kwamba last time nilimuuliza kabisa kwanza una mtu mwingine mbona una behave hivyo kama unaye niambie ukweli wako usinifiche basi akawa anasema hapana hamna kitu chochote nipo mwenyewe, so jana ndio nikasema why alikuwa ananichezea akili as nimemfanyia kitu kibaya sana. ila nashukuru sana kaka naona ungekuwa wewe jana ingekuwa habari nyingine
 
Safi sana kwa busara ulizozitumia,zinazo washinda wanaume wengi. Usiache hizo busara ziende zake.umemuonesha wewe ni mwanaume.

Nashukuruu sana mkuu wangu, yeah ni busara tosha kwa sababu jamaa alitegemea na mimi nitamsemea mbovu ila niliamua kumjibu kiustaarabu tu kwa kweli.....
 
pola sana kaka yangu...mimi binafsi nakupongeza kwa kuwa na ustaarabu na utu wa namna hiyo kwani ni wachache sana wenye uwezo huo. Ok, mimi nakushauri UACHANE kabisa na huyo dada maana atakupotezea muda wako kwa kufikiri labda umepata kumbe hakuna kitu. Pia ninavyojua mambo kama haya, usije kushangaa akakujia tena kukuomba msamaha akishatibuliwa na huyo mumewe mtarajiwa...sidhani hata kama kuna ndoa hapo, utakuja kusema! mimi nakuombea kwa Mungu akujaalie mwanamke mwenye mapenzi ya dhati na busara na hekima kama za kwako, ilui muishi maisha ya ndoa yaliyotawaliwa na furaha, upendo, amani na uaminifu. Inshaalah!

Nashukuru sana tena sana kwa mawazo yako na msaada wako kwa kweli, nimefurahi kusoma comment nzuri na ya kutoa moyo asante sana, Sana so far ameshanipotezea mda mwingi sana mambo mengi sana yame ni cost kwa kweli najuta na siku tegemea leo itakuja kuwa hivi ila mipango ya mungu na yeye ndio mpangaji wa kila kitu kwa kweli.Sidhani kama kuna ndoa siajabu jamaa alitumia tu hilo neno ndoa kwangu kama mkwara, nashukuru sana na inshaalah kila kitu kitakuwa sawa na nitarudi kwenye hali ya kawaida na kuendelea na maisha ya kawaida, Asante sana kwa ushauri wako,
 
huyo mwanamke hafai,ila ingekuwa mimi,ningemueleza ukweli huyo jamaa,ila aelewe ni mwanamke wa aina gani.kama aamue kuwa nae ni sawa.kwa nini wanawake tunajidhalilisha hivi.ila nakuomba usihisi wanawake wote ni wabaya,u never know,ipo siku utampata mtu ambae atakuwa muaminifu
 
SAFI SANA KAKA ,MIMI KAMA MTU NINAYEPENDA SANA PESA ,CHAKWANZA RUDI KWENYE MASUALA TA ATM BADILI PASSWORD ZAKO WATAKULIZA,
THEN HUYU DADA ATARUDI TU.YOU WILL PROVE ME BEYOND REASONABLE DOUGHT ,TENA WANAUME KAMA NYINYI YOUR WORTH IN THIS WORLD,SASA IYO KISA YAKO IGEUZE MIMI NILISHAFANYIWA HIVYO NA MWANAUME ILA NILIMKOMESHA NILIMWACHA KABISAAAA NA TULIKUWA KWENYE LAST STAGE YA MARRIAGE.NILIMWACHA ALIKUJA MPAKA NA WAZEE NIKAMWAMBIA HAPANA KABISA,MAANA ALIFANYA HIVYO 3TIMES WANAWAKE TOFAUTO NA BORA WEWE ALITUMIA SIMU YAKE ,MIMI ALITUMIA SIMU YA WANAWAKE ZAKE KWA DHARAU ZAIDI NI KITENDO KILICHONIUMA SANA SANA . ALIRUDI KWA MAGOTI ILA nikampa wimbo wa witney hauston
"On My Own"


Nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri nimefurahi sana, na vile vile nimeshafanya kama ulivyosema toka jana muda ule ule nilifanya, nashukuru sana, pia alitumia simu ya jamaa yeye ndio alianza kuonea then ndio akampa huyo jamaa mwenyewe, ndio maana sikuamini kabisaa ikafikia nikamuuliza jina lako nani maana nilishasikia sauti yake na jinsi alivyoniambia nikawa shocked,Daaaa na wewe pole sana tena sana kwa yaliyokukuta kwa kweli ni mwenyezi mungu ametuepusha na mengi plus nadhani hawajui nini wanataka ndio maana. Daaa pole sana kwa kweli.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom