Je, nimekosea kuwapotezea baadhi ya ndugu zangu? Naomba ushauri tafadhali

Hawa ndugu Kaa nao mbali na venye una mke mzungu na Uropa umetimba yaani wanateseka Sana Sana wanatamani wawe karibu yako wakuroge urudi ulikotoka
Wajumbe sio watu,
Adui Yako ni mtu wa nyumbani mwako Kaa nao mbali kataa shobo

Kama unawasaidia watumie pocket money ila usikaribiane nao wakusikie Kwa Bomba tu Jenga ukaribu na hao ndugu zako wa tumbo Moja mkuu ndio ndugu wa kweli wengine hao wanakupendea vitu tu!

Beelzebub is devil put aside of you!

Very true. Ndugu zangu tumbo moja wanafaidi na wana access na mimi bila matatizo. Ninawanyanyua kadiri navyoweza ila wale wengine wanatafuta sana namna ya kunifikia angalau wafaidi.
 
muombe Mungu sali kwa iman yako na moyo wako utafunguka kisha wasamehe undugu na maisha mapya yaendeleee...NB maisha hayana formular binadam hatuijui kesho yetu hata ww hapo ulipo anything anytime mambo yaweza badilika...Tenda wema wende zako Kamanda Dunia hiii wote tutapita

Nimekupata
 
Msamehe mzee na umtunze,hao wengine ukianza tu kuwasaidia ndo wanaweza kuwa your downfall!binadamu wabaya,tena wanaweza kwenda kwa mganga wakuroge ufilisike,acha mazoea nao kabisa
Akufaaye kwa dhiki ndie rafiki,usisahau hilo

Mzee nimemsamehe ila upande wa pili sitaki mazoea nao
 
Full stop
...ishia hapo hapo...
Ya mzee mwache yawe ya mzee ya watoto acha yawe yawatoto...
Kutokana una uwezo na una kauli Mzee akikaza kuingilia mipaka hiyo mchane live...
Mwambie matendo yaliyotendwa ni Kwa marehem mama Yako...wakamuombe msamaha yeye akikkubali atakutafuta kiroho ..Ila kwa Sasa nafsi haipo saw na unaomba uheshimiwe maamuzi
Hiyo hela amini nakwambia ukiitoa haitasaidia na watarudi Bora uile au ujenge mahusiano na familia Zaid ya upande wa mkeo..na jamaa na marafiki walio karibu nawewe maana hao ndo dhamana Yako kesho..
Ao ndugu zako Wacha wawe ndugu wa majina na salamu Ila kunja mwanzo mwisho..walishindwa muheshimu Mungu wao wa Duniani unadhan wataheshim iyo 5mil

Tatizo Mzee wangu hanielewi. Ila yeye nimemsamehe. Matatizo yake na marehemu mama yangu niliyaweka pembeni. Ninasimamia hali yake ya afya na matunzo ya kila siku
 
Nawasalimu nyote!

Moja kwa moja kwenye mada, historia yangu ina changamoto nyingi. Naamini kila mmoja ana changamoto yake. Kwa kifupi ni kwamba nimezaliwa kwenye familia ya wake wawili.

Mama yangu ni mke wa pili kwa Mzee. Aliolewa na Mzee baada ya mamkubwa kufariki miaka ya sabini. Nikiwa mdogo sana sikuona sikujua tofauti mpaka nilivyokuwa na umri wa kupambanua mambo. Mama yangu (sasa marehemu) alikuwa mpole sana na aliwapokea wototo wa mumewe bila shida.

Tatizo ni kwamba mama yangu alikuja kupatwa na ugonjwa mmoja mbaya sana, sitalitaja lakini ule ungonjwa ukawa ndiyo mwanzo wa matatizo yooote. Kwanza Mzee wangu anaonekana alimind Kwanini babu yangu alimuozesha mama yangu huku akijua binti yake anaumwa. Nilivyokuja kufanya utafiti, nilikuja kuambiwa kwamba mama yangu hakuwahi kuumwa kabla ya kuolewa na hata alipoolewa ilichukua miaka kadhaa ndo ugonjwa ukazuka.

Huu ugonjwa ulepelekea mama yangu kuwa kama mlemavu fulani hivi. Ikawa chanzo cha unyanyapaa usiyomithilika. Katika ukoo wetu baadhi hawakusema moja kwa moja kwa heshima ya Mzee lakini chini chini tuliishia kudharauliwa sana, mama yangu alidharauliwa sana. Kibaya zaidi ni kwamba mtoto wa kiume wa kwanza kwa mamkubwa alikuwa sehemu ya waliotudharau. Baadae alivyooa mke wake akawa ndo kabisaaaaaa. Kwake hata uji kunywa ilikuwa mbinde.

Kipindi hicho Mzee anapata vijisenti kidoog kidoog akafanikiwa kuwasomesha watoto wa Nyumba kubwa kwa alivyoweza. Kaka yangu mkubwa akapelekwa chuo cha ualimu baadae akaajiriwa na serikali, mtu wa kwanza kwenye ukoo kuajiriwa serikalini. Kichwa kikavimba. Mdogo wake pia wakiume akapelekwa naye chuo cha ualimu akapata ajira. Mdogo wao wa mwisho akapelekwa mpaka sekondari akaja kuolewa na mwanaume mwenye kipato cha wastani hivyo kiburi ikaongezeka.

Sisi kwa upande wetu, dada yangu mkubwa nakumbuka alikimbilia kuolewa akiwa mdogo sana kutokana na manyanyaso ya wana ukoo. Mimi nikaja kusoma sekondari kwa kujilipia. Kila wikendi nilikuwa narudi kijijini kukata miti ambayo Mzee alikuja kuingia dili na shule kununua kwa matumizi ya jikoni hivyo ikawa kama ada yangu.

Nakumbuka Mzee aliwahi kutoa kauli kwamba sisi watoto wa mke mdogo tunamsumbua na hatuna manufaa kama walivyo wale wa mamkubwa. Nilimind sana ila sikuwa na jinsi. Kwa watoto wa kiume upande wa mama, mimi ndiye mkubwa.

Nilivyomaliza sekondari sikufaulu vizuri na Mzee akawa hana mpango wa kunipeleka chuo. Bahati mbaya sijui niseme bahati nzuri. Wakati namaliza sekondari, dada yangu upande wa mamkubwa akawa anahitimu naye ualimu Ekenford Tanga. Alipokuwa anasoma Tanga, alijenga urafiki na familia moja ya kisambaa ambayo walimpa binti yao aje kumtembelea kwetu kujenga undugu.

Huyu binti nilikutana naye kwa wito wa dada yangu aliyenitaka nimuonyeshe mji wetu kidogo. Bahati mbaya tukapendana. Tatizo likawa naye amemaliza form four na alikuwa na mpango wa kuendelea na form five.

Nilichofanya ni kutafuta sababu ya kuja Dar ili niwe Karibu naye. Baadae akajiunga na high school Mpwapwa. Mtoto alikuwa mbichi, utepe niliukata mimi. Tatizo ni kwamba dada yangu alipogundua tupo serious hakupenda na mpaka leo sijajua ni kwanini na sikuwahi kumuuliza kwani alichofanya ni kuja Dar akakutana na familia ile, wakati huo mama wa huo binti na dada zake walikuja Dar, alinichafua sana.

Kilichofuata ni kwamba yule binti alipigwa biti sana na ndugu zake kiasi cha yeye kuchanganyikiwa. Wakati huo yeye bahati mbaya alikuwa shuleni hivyo hakuweza kunitetea dhidi ya uwongo ulokuwa unasemwa juu yangu.

Siku fanya lolote, nilichomuambia dada baada ya kupata zile taarifa ni “mwisho wa ubaya ni aibu” nikatulia.

Yule binti tulikuja kuachana kwani maji yalichafuka sana. Sasa baada ya pale shemeji yangu (mume wa dada) biashara ikabuma. Akafilisika kabisa mpaka kesho.

Katika kufilisika huko, ikabidi dada atafute kazi akahitaji kwenda kusomea kozi ya kufundisha shule maalumu. Nikaombwa kupitia dada yangu tumbo moja nimchukue binti yake aje anisaidie kukaa na mtoto badala ya kumuajiri mtu mwingine. Hii hoja ilikuwa ni kumsaidia dada yangu (mfini ni wangu) apate ada. Bila hiyana nilitoa ushirikiano na kumlipa hela kiasi ambacho asingepata kwa mwingine. Nilimpiga sound mke wangu (Mzungu) aelewe Kwanini tunamlipa dada kiasi kikubwa vile.

Cha ajabu baadae yule mpwa wangu akawa na tabia za kijinga tu ambazo hazieleweki hususani kwa namna ambavyo alikuwa ana relate na mimi ila nikapotezea. Baada ya yeye kuondoka na miaka ikapita nilishangaa kumbe kipindi yupo kwangu, mama yake alianza tena kuingilia ndoa yangu. Akatia fitina za kutosha. Haya nilikuja kujua siku moja tulikuwa na ugomvi wa nyumbani na mke wangu, kwa hasira akafunguka yote aliyokuwa akiambiwa na dada yangu kupitia mpwa wangu. Kumbuka hapo nimempa hela ndefu tu ya kulipia ada akanipa binti yake anisaidie kwa wakati ule.

Sasa mimi historia ya kunyanyapaliwa mama yangu na sisi watoto wake, bahati mbaya sana mambo yamebadilika mimi kusema kweli ndo nina kipato cha kueleweka, upande wa nyumba kubwa wanataka niwape tafu. Jambo hili sijaliafiki kwani hawakunipa hata pocket money wakati nasoma, hawakunilipia ada ila mafanikio yangu wanataka kuyafaidi.

Mzee ninamtunza kwa kidogo nachopata, niliwajengea nyumba ya uhakika ila kwa ndugu hawa nimekataa kabisa.

Sasa leo nimekuja hapa kupata ushauri, Mzee wangu amenitafuta kwamba dada (mfitini) amemuomba amsaidie kuniomba 5m ana shida kubwa. Hata kama ni kukopa. Nafsi inagoma kabisa. Yeye mwenyewe hawezi kuniomba moja kwa moja.

Nikiri kwamba alishaniomba msamaha mwaka 2018. Ila huu msamaha uliombwa kimkakati kwasababu uchumi wao ulishayumba ikawa jeuri haipo tena. So ilikuwa ni kama kutafuta njia ya kunirudisha kwenye anga zake.

Nisaidieni ushauri.
Usithubutu kumpa hiyo hela
 
Full stop
...ishia hapo hapo...
Ya mzee mwache yawe ya mzee ya watoto acha yawe yawatoto...
Kutokana una uwezo na una kauli Mzee akikaza kuingilia mipaka hiyo mchane live...
Mwambie matendo yaliyotendwa ni Kwa marehem mama Yako...wakamuombe msamaha yeye akikkubali atakutafuta kiroho ..Ila kwa Sasa nafsi haipo saw na unaomba uheshimiwe maamuzi
Hiyo hela amini nakwambia ukiitoa haitasaidia na watarudi Bora uile au ujenge mahusiano na familia Zaid ya upande wa mkeo..na jamaa na marafiki walio karibu nawewe maana hao ndo dhamana Yako kesho..
Ao ndugu zako Wacha wawe ndugu wa majina na salamu Ila kunja mwanzo mwisho..walishindwa muheshimu Mungu wao wa Duniani unadhan wataheshim iyo 5mil

Nashukuru Kwa maoni. Nimeyapokea kwa mikono miwili
 
Golden chance never come twice. M/mungu hakukupa kwa bahati mbaya, kakupa wewe kisha kawaangusha wao kwa makusudi upate kulipa kisasi, sasa jifanye baba huruma halafu uje kuona cha mtema kuni.

Unamuona Diamond mjinga anavyo mdiss yule mzee wake eeh? Jifanye malaika utarudi kutuhadithia hapa! Mwanaume mzima unashindwa kuwa na misimamo, wanini ndugu kama hao, unawaweka weka karibu ili uvumbue nini kwa mfano?

Hata huyo baba ako ungempotezea tu, kwani shing ngapi? Wanakufanya jinga lao na watahakikisha wanakuharibia maisha kwa kukutumia wewe mwenyewe! Mwenye macho haambiwi 'ona', alieua kwa upanga nae afe kwa upanga. (Umenimwagisha mipovu km nakujua vile )
Kamati ya roho mbaya kazini..... Fikra zako ni sawa na zangu... Mimi ninao ndugu zangu walitunyanyasa familia yetu kisa tulikuwa masikini, tuliteseka na kwamba taabika huku wakila na kunywa kwa mirija na familia zao. Sasa meza imepinduka. Wajomba waliomtenga mama yetu marehemu, sasa wamegeuka kuwa ombaomba. Juzi kuna anko alitaka kunikopa laki tano, ila aliogopa kuni face mojakwamoja akamtumiaa Mamdogo ambaye tunaelewana kuniomba hela. Nilivyogundua nilichomoa. Kila mtu apambane
 
muombe Mungu sali kwa iman yako na moyo wako utafunguka kisha wasamehe undugu na maisha mapya yaendeleee...NB maisha hayana formular binadam hatuijui kesho yetu hata ww hapo ulipo anything anytime mambo yaweza badilika...Tenda wema wende zako Kamanda Dunia hiii wote tutapita

Kwamba kipato chake cha wote lkn walivokua wanacho wao kilikua chao.

Siafikiani ma wewe hata robo. Kutesa ni kwa zamu.
 
Nawasalimu nyote!

Moja kwa moja kwenye mada, historia yangu ina changamoto nyingi. Naamini kila mmoja ana changamoto yake. Kwa kifupi ni kwamba nimezaliwa kwenye familia ya wake wawili.

Mama yangu ni mke wa pili kwa Mzee. Aliolewa na Mzee baada ya mamkubwa kufariki miaka ya sabini. Nikiwa mdogo sana sikuona sikujua tofauti mpaka nilivyokuwa na umri wa kupambanua mambo. Mama yangu (sasa marehemu) alikuwa mpole sana na aliwapokea wototo wa mumewe bila shida.

Tatizo ni kwamba mama yangu alikuja kupatwa na ugonjwa mmoja mbaya sana, sitalitaja lakini ule ungonjwa ukawa ndiyo mwanzo wa matatizo yooote. Kwanza Mzee wangu anaonekana alimind Kwanini babu yangu alimuozesha mama yangu huku akijua binti yake anaumwa. Nilivyokuja kufanya utafiti, nilikuja kuambiwa kwamba mama yangu hakuwahi kuumwa kabla ya kuolewa na hata alipoolewa ilichukua miaka kadhaa ndo ugonjwa ukazuka.

Huu ugonjwa ulepelekea mama yangu kuwa kama mlemavu fulani hivi. Ikawa chanzo cha unyanyapaa usiyomithilika. Katika ukoo wetu baadhi hawakusema moja kwa moja kwa heshima ya Mzee lakini chini chini tuliishia kudharauliwa sana, mama yangu alidharauliwa sana. Kibaya zaidi ni kwamba mtoto wa kiume wa kwanza kwa mamkubwa alikuwa sehemu ya waliotudharau. Baadae alivyooa mke wake akawa ndo kabisaaaaaa. Kwake hata uji kunywa ilikuwa mbinde.

Kipindi hicho Mzee anapata vijisenti kidoog kidoog akafanikiwa kuwasomesha watoto wa Nyumba kubwa kwa alivyoweza. Kaka yangu mkubwa akapelekwa chuo cha ualimu baadae akaajiriwa na serikali, mtu wa kwanza kwenye ukoo kuajiriwa serikalini. Kichwa kikavimba. Mdogo wake pia wakiume akapelekwa naye chuo cha ualimu akapata ajira. Mdogo wao wa mwisho akapelekwa mpaka sekondari akaja kuolewa na mwanaume mwenye kipato cha wastani hivyo kiburi ikaongezeka.

Sisi kwa upande wetu, dada yangu mkubwa nakumbuka alikimbilia kuolewa akiwa mdogo sana kutokana na manyanyaso ya wana ukoo. Mimi nikaja kusoma sekondari kwa kujilipia. Kila wikendi nilikuwa narudi kijijini kukata miti ambayo Mzee alikuja kuingia dili na shule kununua kwa matumizi ya jikoni hivyo ikawa kama ada yangu.

Nakumbuka Mzee aliwahi kutoa kauli kwamba sisi watoto wa mke mdogo tunamsumbua na hatuna manufaa kama walivyo wale wa mamkubwa. Nilimind sana ila sikuwa na jinsi. Kwa watoto wa kiume upande wa mama, mimi ndiye mkubwa.

Nilivyomaliza sekondari sikufaulu vizuri na Mzee akawa hana mpango wa kunipeleka chuo. Bahati mbaya sijui niseme bahati nzuri. Wakati namaliza sekondari, dada yangu upande wa mamkubwa akawa anahitimu naye ualimu Ekenford Tanga. Alipokuwa anasoma Tanga, alijenga urafiki na familia moja ya kisambaa ambayo walimpa binti yao aje kumtembelea kwetu kujenga undugu.

Huyu binti nilikutana naye kwa wito wa dada yangu aliyenitaka nimuonyeshe mji wetu kidogo. Bahati mbaya tukapendana. Tatizo likawa naye amemaliza form four na alikuwa na mpango wa kuendelea na form five.

Nilichofanya ni kutafuta sababu ya kuja Dar ili niwe Karibu naye. Baadae akajiunga na high school Mpwapwa. Mtoto alikuwa mbichi, utepe niliukata mimi. Tatizo ni kwamba dada yangu alipogundua tupo serious hakupenda na mpaka leo sijajua ni kwanini na sikuwahi kumuuliza kwani alichofanya ni kuja Dar akakutana na familia ile, wakati huo mama wa huo binti na dada zake walikuja Dar, alinichafua sana.

Kilichofuata ni kwamba yule binti alipigwa biti sana na ndugu zake kiasi cha yeye kuchanganyikiwa. Wakati huo yeye bahati mbaya alikuwa shuleni hivyo hakuweza kunitetea dhidi ya uwongo ulokuwa unasemwa juu yangu.

Siku fanya lolote, nilichomuambia dada baada ya kupata zile taarifa ni “mwisho wa ubaya ni aibu” nikatulia.

Yule binti tulikuja kuachana kwani maji yalichafuka sana. Sasa baada ya pale shemeji yangu (mume wa dada) biashara ikabuma. Akafilisika kabisa mpaka kesho.

Katika kufilisika huko, ikabidi dada atafute kazi akahitaji kwenda kusomea kozi ya kufundisha shule maalumu. Nikaombwa kupitia dada yangu tumbo moja nimchukue binti yake aje anisaidie kukaa na mtoto badala ya kumuajiri mtu mwingine. Hii hoja ilikuwa ni kumsaidia dada yangu (mfini ni wangu) apate ada. Bila hiyana nilitoa ushirikiano na kumlipa hela kiasi ambacho asingepata kwa mwingine. Nilimpiga sound mke wangu (Mzungu) aelewe Kwanini tunamlipa dada kiasi kikubwa vile.

Cha ajabu baadae yule mpwa wangu akawa na tabia za kijinga tu ambazo hazieleweki hususani kwa namna ambavyo alikuwa ana relate na mimi ila nikapotezea. Baada ya yeye kuondoka na miaka ikapita nilishangaa kumbe kipindi yupo kwangu, mama yake alianza tena kuingilia ndoa yangu. Akatia fitina za kutosha. Haya nilikuja kujua siku moja tulikuwa na ugomvi wa nyumbani na mke wangu, kwa hasira akafunguka yote aliyokuwa akiambiwa na dada yangu kupitia mpwa wangu. Kumbuka hapo nimempa hela ndefu tu ya kulipia ada akanipa binti yake anisaidie kwa wakati ule.

Sasa mimi historia ya kunyanyapaliwa mama yangu na sisi watoto wake, bahati mbaya sana mambo yamebadilika mimi kusema kweli ndo nina kipato cha kueleweka, upande wa nyumba kubwa wanataka niwape tafu. Jambo hili sijaliafiki kwani hawakunipa hata pocket money wakati nasoma, hawakunilipia ada ila mafanikio yangu wanataka kuyafaidi.

Mzee ninamtunza kwa kidogo nachopata, niliwajengea nyumba ya uhakika ila kwa ndugu hawa nimekataa kabisa.

Sasa leo nimekuja hapa kupata ushauri, Mzee wangu amenitafuta kwamba dada (mfitini) amemuomba amsaidie kuniomba 5m ana shida kubwa. Hata kama ni kukopa. Nafsi inagoma kabisa. Yeye mwenyewe hawezi kuniomba moja kwa moja.

Nikiri kwamba alishaniomba msamaha mwaka 2018. Ila huu msamaha uliombwa kimkakati kwasababu uchumi wao ulishayumba ikawa jeuri haipo tena. So ilikuwa ni kama kutafuta njia ya kunirudisha kwenye anga zake.

Nisaidieni ushauri.
Tenda wema nenda zako!
 
Nashukuru Kwa maoni. Nimeyapokea kwa mikono miwili
Na famaham tunakushauri from experience
Nasema haya Kwa kupitia same scenerio Ila Mimi ni ilikuwa dingi mdogo...
Yani mwaka wa tano saiz kimyaaa nimenyuti maisha yanaenda shida iliowafanya waombe msamaha nilisaheme Ila kuitatua nilikaza Sina Hela althogh wanaona lifestyle..ao Wanae waliokuwa vinara wa vijembe alikuja magu akawanyoosha mavyeti feki wakarudi mabench heshma ikarejea ..tunaonana status tu Ila Cha msingi shida haziishi na hawafi bas waendelee kupambana kama nami navopambana
 
Usiache kumkumbusha mzee ile kauli ya nyumba kubwa na ndogo.
Ila iwe kwa wema au utan
 
😂😂ubaya ubaya
 
NDUGU WA KWELI NI WATOTO WAKO!WATUNZE SANA!!!HAO NDUGU WENGINE WEKA KANDO HATA WAKIHITAJI MSAADA ISIZIDI HATA 30000/=!!!LABDA KAMA UMEWAAJIRI WALIPE KUTOKANA NA KAZI!!!USIWAKOPESHE HELA NYINGI KAMA HIZO WAAMBIE HUNA!!MTUNZE BABA KAMA KAWAIDA LAKINI USIMPE MTAJI WALA CHOCHOTE CHA MAANA!!!!MWANAUME ALIEZAA NA MAMA YANGU AKAMDHARAU NA KUMTESA MAMA YANGU NI MBWA KAMA MBWA MWINGINE MKUU! TAMBUA HILO!!!!!
 
Usiache kumkumbusha mzee ile kauli ya nyumba kubwa na ndogo.
Ila iwe kwa wema au utan

Mzee siku hizi kama piriton maana nyumba mimi ndo nilikuja kumjengea wakati mwanaye aliyemsomesha na kupata kazi serikali hakujali.

Siku hizi anatambua kwamba mimi ndo nipo kwa ajili yake. Ila kumkumbusha naona siyo Sawa. Nafanya yangu nasubiri afe tu zake maana umri umeenda
 
NDUGU WA KWELI NI WATOTO WAKO!WATUNZE SANA!!!HAO NDUGU WENGINE WEKA KANDO HATA WAKIHITAJI MSAADA ISIZIDI HATA 30000/=!!!LABDA KAMA UMEWAAJIRI WALIPE KUTOKANA NA KAZI!!!USIWAKOPESHE HELA NYINGI KAMA HIZO WAAMBIE HUNA!!MTUNZE BABA KAMA KAWAIDA LAKINI USIMPE MTAJI WALA CHOCHOTE CHA MAANA!!!!MWANAUME ALIEZAA NA MAMA YANGU AKAMDHARAU NA KUMTESA MAMA YANGU NI MBWA KAMA MBWA MWINGINE MKUU! TAMBUA HILO!!!!!

Nimepokea ushauri mkuu
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom