Je, nilikosea kumwadhibu huyu mtoto wa jirani yangu?

Raymanu KE

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
6,781
12,506
Habari zenu wanajamvi? Natumai mnaendelea vyema na mishe zenu. Nawatakia Jumapili njema popote mlipo.

Juzi kati nilikuwa Niko kwetu vijijini nimeenda kuwatembelea wazee wangu kdgo.Sasa Kuna siku nilikuwa nipo nyumbani nimekaa uani na dingi wangu tunabadilishiana mawazo kuhusu Mambo fulani fulani.Ghafla nikamwona mtoto wa jirani yetu analisha mifugo yao shambani kwetu.Nikamwona Yuko bize sana anacheza na simu mpaka amewasahau mifugo wameanza kuvuka kwenye shamba la pili na kuanza kuharibu mimea ya iliyokuwa imepandwa shambani humo.

Jamaa nikainuka nikanyatia nyatia pole nikielekea upande wake nimwambie amakinike na kile kilichomleta vinginevyo nitamfukuza aondoke kbsa.Nilipofika umbali wa Kama mita5 kutoka kwake Hadi kwangu nilianza kuziskia sauti fulani kutoka kwenye simu yake ( sijui simu yenyewe kupewa na Nani maana alikuwa mtoto mdogo Sana wa miaka Kama hivi 11 kupelekea 12)

Nilimstukia mtoto nikashindwa Sana kumuona anaangalia video chafu za ngono kwenye simu aliyekuwa nayo.Nilimkamata chap nikamshika mkono nikaanza kumzaba vibao huku nachuma kiboko ili niweze kumwadhibu kutokana na ujinga aliokuwa anafanya mpaka amewasahau mifugo wamevamia mimea ya wenyewe.

Nilimchapa viboko kadhaa Akaanza kulia kwa sauti Kali ( Hapa nilijua anaigiza tu maana sikuwa namchapa kwa nguvu Wala kwa fimbo kubwa).Nilikuwa namuadhibu huku namuuliza simu kapewa na Nani na Ni kwanini alikuwa anaangalia video chafu za namna wakati yeye Bado Ni mtoto mdogo Sana.Akasema alidokoa sh' 200 kwenye wallet ya babake Kisha akaenda akamhonga jamaa fulani akampa simu ambayo ilionekana imesheheni uchafu wa video za ngono.

Baada ya muda mfupi nilimuona mama yake anakuja mbio huku anapiga makelele eti namuulia mtoto niachane naye sio wa kwangu Akabwabwaja bwaja maneno mengi plus kunitukana Mimi.Ilibidi babangu aingilie Kati kumwelewa huyo mama ila mama alidinda kbsa akalalamika Sana eti kwanini nilikuwa namuuliza mwanaye.

Binafsi sikuwa namuadhibu huyo mtoto eti kisa amewaachia mifugo wake wanakula mimea ya mwenye shamba kwa kujisahaulisha Ila nilikuwa namuadhibu baada ya kugundua anaangalia vitu vibaya kwenye wakati angali mdogo Sana Kwa hiyo nilikuwa Nampa discipline ili aachane na Mambo ya simu azingatie masomo kwanza.

Kwa mtazamo wenu wanaJF hivi nilikosea kumwadhibu huyu mtoto wa jirani yangu. Maoni yenu yatanipa mwongozo ile siku nyingine nikikumbana na case Kama hii nitajua jinsi ya kuihandle.

Nawasilisha
 
Ulikosea ungemtandika kisawasawa sio kumhurumia alaf Ungemtafta mzee wake kumueleza maana wamama wanamapenzi ya mtoto kiasi kwamba yuko radhi kugombana na majirani wote ata kama kosa kafanya mtoto wake ila atamtetea kwa nguvu zoteee..yani hawaaminigi kabsa kama watoto wao wamefanya kosa na wanamioyo milaini sanaa
 
Uonevu tu. Hakuna njia nyingine ya kumkanya zaidi ya kichapo? Au ndo vile watu weusi bila fimbo hatuendi?
 
Ulikosea ungemtandika kisawasawa sio kumhurumia alaf Ungemtafta mzee wake kumueleza maana wamama wanamapenzi ya mtoto kiasi kwamba yuko radhi kugombana na majirani wote ata kama kosa kafanya mtoto wake ila atamtetea kwa nguvu zoteee..yani hawaaminigi kabsa kama watoto wao wamefanya kosa na wanamioyo milaini sanaa
Kimbee!!
 
Habari zenu wanajamvi? Natumai mnaendelea vyema na mishe zenu.Nawatakia Jumapili njema popote mlipo.

Juzi kati nilikuwa Niko kwetu vijijini nimeenda kuwatembelea wazee wangu kdgo.Sasa Kuna siku nilikuwa nipo nyumbani nimekaa uani na dingi wangu tunabadilishiana mawazo kuhusu Mambo fulani fulani.Ghafla nikamwona mtoto wa jirani yetu analisha mifugo yao shambani kwetu.Nikamwona Yuko bize Sana anacheza na simu mpaka amewasahau mifugo wameanza kuvuka kwenye shamba la pili na kuanza kuharibu mimea ya iliyokuwa imepandwa shambani humo.


Nawasilisha
Kwa kizazi cha zamani ulichofanya ni sawa kabisa, ila kwa sasa hivi mambo yamebadilika
 
Back
Top Bottom