Je nilazima kila umkutapo mwanamke na mwanamume faragha ni yale yale?

mringi

Member
Apr 4, 2012
99
0
Inakuwaje watu wenye akili zao wafikirie kila unapomkuta mwanamke na mwanamume faragha eti wanazungumzia mambo ya kuzaa tu,au eti ukiweka miadi na mwanamke mkutane sehemu fulani ni kwa ajili ya mambo ya kuzaa tu,kwani wanawake hawako kwenye mipango ya kiuchumi?hatuwezi kuzungumza na wanawake masuala ya biashara? masuala ya kuanzisha miradi? ushauri katika masuala ya maisha?.masuala ya uadilifu,masuala ya utu wema?.Yaani ukikutwa na mwanamke wapo wanaofikiria ni uzinzi tu,uchafu tu,.Watu tubadilike tuwape Wanawake ,mama zetu Heshima zao na wanaume tuwe na staha,tujiheshimu ,tutoe maboriti kwenye macho yetu, na tuzipe raha na ujasiri nafsi zetu.Aliye msafi na awe wa kwanza kurusha jiwe.
 
Daud omar

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
2,459
1,225
Faragha unayongelea wew ni ipi?? Manaake faragha zipo nyingi, huwezi kumchukua mke wa mtu eti unaenda nae faragha kuzungumza biashara, na huyo atakae kuelewa atakuwa sio timamu
 
Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
20,925
2,000
Mkishakutwa faragha inaleta utata kidogo,msikae faragha kaeni sehemu ya wazi.
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,024
1,500
Tatizo lako wewe unahusisha kujamiiana na uzinzi na uchafu, badilika kwanza.

Kwani kuzaa sio japo jema na la kiadilifu? Unaangalia kujamiiana kama tendo la ngono(watu wanaofanya kwa kuridhisha tamaa zao za kimwili)

Unasahau kujamiana kunaweza kuwa 'tendo la ndoa-ndani ya ndoa kwa kufurahishana ama kuzalishana, jamii inalikubali na kulibariki, ndo maana kila siku mnachangia harusi ili watu wakajamiiane kwa heshima katika jamii. Tena hata kisheria mkifunga ndoa lazima mle mzigo ili kuihalalisha ndoa-consummate marriage, sasa uchafu na uzinzi unaanzia wapi?

Kujamiiana kwakweza kuwa kufanya mapenzi-kati ya wawili wapendanao, haijalishi ni ndoani ama nje ya ndoa, but hte feeling is real. Sasa hiyo ya uchafu wa tendo ni jicho lako wewe mtazamaji, wenzao aku kwa raha zao na hisia zao.

Fanyia kazi kwanza mtazami wako wa kujamiiana.

Kuhusiana na biashara yati ya Ke na Me, inatetegemea kilichowaweka kwanza karibu ni nini. Kama mlikuwa karibu sababu mmoja kavutiwa na mwenzie kingono, afu katikati mnataka kubadili uelekeo muwe kibiashara ni uongo mtupu, Mwisho wa siku mtakuwa mnaongelea ngono tu.

Ila kama mlikutana kwa jicho la kibiashara kuanzia siku ya kwanza, kunakuwa na psychological boundary, mkiamua kulaza ni zambi zenu wenyewe kama za Mh Zambi kula posho mara 2.
 
Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
36,024
1,500
Ujue faragha inaanzia kichwani? Ndo maana kuna watu full makiss barabarani au ngono zembe fukweni au makaburini, kule kuna faragha gani?

Au hujaona wanamme wanapiga mabao kwenye daladala? Yule naye ana faragha gani pale?

Mtizamo wangu, faragha ianzie kichwani, then kwingine kunafuata.

Mkishakutwa faragha inaleta utata kidogo,msikae faragha kaeni sehemu ya wazi.
 
Tamatheo

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,303
2,000
Nikikukuta faragha na mwanamke nitawaza hivyo hivyo kwani kamusi yangu imenipa maana ya faragha na sitoamini tofauti.
 
dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,348
2,000
Inakuwaje watu wenye akili zao wafikirie kila unapomkuta mwanamke na mwanamume faragha eti wanazungumzia mambo ya kuzaa tu,au eti ukiweka miadi na mwanamke mkutane sehemu fulani ni kwa ajili ya mambo ya kuzaa tu,kwani wanawake hawako kwenye mipango ya kiuchumi?hatuwezi kuzungumza na wanawake masuala ya biashara? masuala ya kuanzisha miradi? ushauri katika masuala ya maisha?.masuala ya uadilifu,masuala ya utu wema?.Yaani ukikutwa na mwanamke wapo wanaofikiria ni uzinzi tu,uchafu tu,.Watu tubadilike tuwape Wanawake ,mama zetu Heshima zao na wanaume tuwe na staha,tujiheshimu ,tutoe maboriti kwenye macho yetu, na tuzipe raha na ujasiri nafsi zetu.Aliye msafi na awe wa kwanza kurusha jiwe.

Haiwezekani manake kila anapokaa mwanamke na mwanaume basi katikati yao kuna shetani!
 
Qualifier

JF-Expert Member
Dec 14, 2012
1,251
1,500
Mtoa maada anaelewa maana ya neno FARAGHA? Faragha ni kukaa sehemu ya siri na kufanya mambo ya siri hata ikiwezekan kutumia viungo vya siri sasa hapo waweza kukaa na mke wa mtu faragha ukifumaniwa useme mlikuwa kwenye mipanga ya biashara nani atakuelewa?
 
dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,348
2,000
Unasahau kujamiana kunaweza kuwa 'tendo la ndoa-ndani ya ndoa kwa kufurahishana ama kuzalishana, jamii inalikubali na kulibariki, ndo maana kila siku mnachangia harusi ili watu wakajamiiane kwa heshima katika jamii. Tena hata kisheria mkifunga ndoa lazima mle mzigo ili kuihalalisha ndoa-consummate marriage, sasa uchafu na uzinzi unaanzia wapi?

I LIKE this
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom