Je! Nikweli msanii ni kioo cha jamii?

kitero

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
563
109
Tunaimani na tunaambiwa yakuwa msanii ni kioo cha jamii, je tunaelewa maaana ya huu msemo na nikweli wasanii wetu ni kioo cha jamii? Kioo huwa hakibadishi sura au uhalisia wa mtu/kitu,kioo huonyesha kilichopo mbele yake kiwe kizuri ama kibaya.kwa hiyo ni vizuri tukatafakari huu msemo kwamakini,hiki kioo tunacho kiita cha jamii kipo mbele ya vitu vingi sana visafi na vibaya.Tumewasikia wasanii wengi sana wa hapa na nje ya hapa.je bado huu mseme una maana/mvuto tena?
 
Labda tujiulize kwanza, ni nani aliyeanzisha huu msemo wa msanii ni kioo cha jamii,toka hapo nadhani tutaweza kuendelea..
 
Aah wapi. Sikubaliani kabisa na huo msemo. Ni msemo wa kijinga. Ni msemo unaohalalisha ukwepaji wa majukumu na uwajibikaji.
 
Si kweli kuwa msanii ni kioo cha jamii...maana ingekuwa ni kweli wasanii wengi wangekuwa washavunjika vunjika. Nyie si huwa mnaona kwenye show zao jinsi wanavyojirusha rusha jukwaani au wakati mwingine kurukiwa na mashabiki.
 
kama werevu, wajinga na wapumbavu ni jamii basi msanii ni kioo cha jamii
 
Back
Top Bottom