johnsonmgaya
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 2,818
- 3,729
Habari za asubuhi wapendwa,
Poleni na mvua na majukumu ya leo
Natumai mpo salama kabisa,
Poleni kwa watakaosombwa na maji siku ya leo.
Naomba nilete mada mezani kama ifuatavyo:
Mimi ni muanglikana siwezi sema ni safi moja kwa moja maana siendi kanisani mara kwa mara ila naamini katika Anglican na namjua Mungu kiasi fulani, mke wangu yeye ni mlokole (nimekosa jina la dhehebu ila ni haya makanisa yenye majina majina)
Tumejikuta tupo katika ugomvi (japo si mkubwa) kuhusu dini zetu, baada tu ya kupata binti, kwa sasa huyo mtoto ana miaka 2 na miezi 4 hadi leo nisiwe muongo hatujashukuru wala kumbatiza huyo mtoto kutokana na mvutano uliopo tangu akiwa mchanga.
Mara ya kwanza alisema wao hawabatizi mtoto akiwa na umri mdogo (hajitambui)
Ila kanisani kwangu tunaruhusiwa tena ndo vizuri mtoto akimjua Mungu akiwa hivyo.
hapa kati nikapata ibilisi basi sijaenda tena kanisani kwa kipindi hicho chote labda siku za sikukuu tu. Maisha yakaendelea
Sasa juzi kati mama mtu kapata shoga mlokole (pure) mwenyewe anamuita au tuseme aliyeokoka, wamebebana wakaoneshana kanisa hilo la huyo bibie, mazoea yakaendelea wanatembeleana kila siku tatizo likaanzia hapa, yule anakuja saa moja saa mbili usiku kuondoka saa 4, mwanzo nikajua ni dharura kwa siku hiyo, lakini ile tabia ikaendelea kila siku akijisikia anakuja hadi mda huo, kiukweli kama binadamu mwingine hii hali ikawa inanikera sana maana umetoka kazini unatoka kuoga tu au upo bafuni unasikia hodi sebuleni ukizingatia muda huo kuna habari na vitu vingine.
Anyway hii si issue sana iliyonileta hapa leo, lakini ndo walokole mnavyoelekezwa jinsi ya kuwaokoa watu?
TATIZO LIPO HAPA:
Jana amekuja nyumbani (mda huo) kanikuta nipo zangu sebuleni, wakaanza kunong'onezana sijui kuhusu kubariki mtoto, (walikuwa washaambizana tangu Jumapili walivyokutana kanisani) hivyo hapo alikuwa anampa feedback ya nini kinahitajika, kwakuwa nilikuwa pale akaone anishirikishe na mimi (mambo ya kifedha) kuhusu vinavyohitajika.
Wanahitaji hela ya kadi ya ubarikio 3000/- tu, pia hela ya sadaka kulingana na thamani ya mtoto (hapa ndipo ubongo ulipocheza) anasema kama mwanao anathamani ya elfu mbili sawa toa japo Mungu anakuona kama anathamani ya mbuzi wawili toa Mungu anakuona, Hhhahahha nikajikuta namuangalia binti yangu nikacheka moyoni nikajisemea yale yale washaanzaa hawa watu, maana hakuna mtoto anayelinganishwa na fedha je hawa wanahitaji nini au shilingi ngapi?
So nilichomjibu mimi ni kitu kimoja, hili suala ni la kifamilia hivyo tunapaswa lijadiliwe majibu atakupa mwenzio kesho, kama unavyojua hii issue yenu ndo kwanza nasikia sasahivi japo nilishamwambia hili mda mrefu tu, yeye mwenyewe alisema mda bado so nahitaji niongee nae atakujibu.
Lakini yeye akawa kama analazimisha nikubaliane nalo hapo hapo, kajisomesha biblia hapo wee, mara kumpokea Yesu halihitaji majadiliano na mtu we ukiamua tu moyoni mwako fanya, au hauamini katika Yesu? Au ninavyokuja hapa nakukera maana haupo kabisa na sisi, nikacheka tena kama kawaida yangu, nikamjibu Aunt mbona kitu kidogo tu hiki unataka kulikuza? Umeleta jambo kama baba kichwa cha familia huwa sitoi majibu bila kuangalia effect zake so kuwa na amani kesho si mbali utapata majibu na pia shughuli umesema ni tarehe 29 leo ni tarehe 3 huoni kama kuna mda mrefu wa kujipanga? Then sisi pia tunafamilia mjukuu wao ndo huyo huyo lazima hili suala liwafikie wazazi wa pande zote mbili ili walibariki basi wakabeba hapo wakasindikizana.
Sasa hapa swali langu linauliza hivi:
JE KUNA MNANISHAURI NIFANYE UBATIZO NA UBARIKIO KANISANI KWANGU (ANGLICAN ) AU HUKO KANISANI KWAO?
Serious nahitaji hili lifanyike kama nilivyoelezea hapo juu ila siamini katima makanisa hayo ya ulokole huo ndo ukweli wangu.