Je, Ni wakati wa matajiri kuongoza nchi?

yas-mic

JF-Expert Member
May 25, 2016
472
728
Habari ndugu zangu humu mjengoni,

Nilichokuwa napenda kusema ni kwamba "hivi tunakoelekea kama nchi tuna haja sasa ya kumchagua mtu tajiri kuongoza nchi kama wafanyavyo nchi kama za Marekani ili kuepusha huu ulimbukeni wa viongozi kutaka kutajirikia wakiwa madarakani" nimesema hivi kwasababu bado sijaona logic ya kujengwa kwa kiwanja cha ndege Chato ambacho expected life span yake ni miaka 5-10 kwasababu ndege inayotegemewa kutua ni moja tu huko.

Sidhani kama hii bajeti ya uwanja wa ndege ingekuwepo kama kiongozi angetoka kwenye Kanda zilizoendelea tangiapo.Je hiyo nayo ilikuwa ni moja ya ahadi za mh? Naombeni mniweke sawa hapo jamani mimi nahisi kama najichanganya hivi kwenye kumuelewa au kuelewa mambo anayoyafanya mh.uki compare na maneno yake aliyokuwa anayaongea kila leo ya kumkomboa mnyonge.
 
Back
Top Bottom