Je ni wakati sasa kuwapa wawekezaji kusimamia rasilimali za Tanzania?

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,939
594
Kutokana na ukweli kwamba Serikali imeshindwa kusimamia rasilimali za nchi yaani natural resources na human resources na Takukuru imeshindwa kuzuia rushwa, TRA imefeli kwa kiasi kikubwa kukusanya mapato ya nchi, Serikali haina mpango wala wazo lakudhibiti wizi wa rasilimali. Serikali imeshindwa kusimamia kushuka kwa thamani ya Shilingi. Serikali imeshindwa kwa 100% kudhibiti pesa chafu na imeshindwa kudhibit wizi wa Pesa za uma.

Kwa upande wa human resources ni kwamba hali ya watanzania kuzurula barabarani kutwa mzima bila kazi maana yake ni kwamba serikali imeshindwa kusimamia rasilimali watu au imeshindwa kutumia effectively rasilimali watu. Watu wengi hawazalishi bali ni walaji wa kilichozalishwa na wachache. Sasa kama walaji ni wengi wakati wazalishaji ni wachache tusitegemee muujiza taifa kusonga mbele kiuchumi.

Sasa nawahoji:

Je ni wakati sasa wa kutangaza international Tender ili kupata mwekezaji wa nje kusimamia rasilimali?
Je tutafute mwekezaji wakukusanya kodi?
Je ni wakati sasa wakutafuta mwekezaji kuratibu uchumi wetu?

Mjadala upo mezani.
 
sasa hivi TRA imewajaza wazungu sehemu nyeti na maliasili pia sasa ni wazungu tu.
 
Back
Top Bottom