Je, ni wakati muafaka sasa Serikali iweke utaratibu wa kuitembelea Familia ya Mwl Nyerere??

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,101
1,195
Wanabodi,
Watanzania wengi na raia wa nje ya nchi wanatamani sana kuitembelea familia ya Mwl Nyerere na wengine kuzuru kaburi lake pale Butiama.

Kutokana na watu kuwa huru juu ya hilo watu wengi wanakwenda sana kuijulia hali familia hiyo. Na wengi wao wanaona fahari kufika nyumbani kwake.

Kutokana na kitendo cha watu wengine wasio wema kutumia nafasi ya kuitembelea familia ya Nyerere kwa lengo la kutafuta "Umaarufu wa kisiasa" na wengine kutumia nafasi hiyo kupotosha jamii juu ya mambo mbalimbali, Je ni wakati muafaka sasa serikali iweke utaratibu wa kuitembelea familia ya Mwl Nyerere???

Ni sahihi watu kutumia nafasi ya kuitembelea familia ya Mwalimu na kupotosha umma??

Mandla.
 

tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,470
1,225
hilo swala ni la kifamilia na sio la kiserikali, serikali itamnyimaje mkwe wa nyerere kwenda kwa nyerere? mfano Leticia nyerere wa cdm.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,970
2,000
Hilo swala linahitaji viongozi wenye utashi wanaoweza kutambua hazina za Taifa kama famili ya Baba wa Taifa.
Ila kwa viongozi tulio nao wanaoweza kudhululumu hata kiwanja cha familia ya Mwalimu itachukua miaka miaka mingi kutambua hilo.
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Utawafahamu watu walioishiwa HOJA? Si ajabu huyu ni mshauri wa Kinana! Baada ya kumwekea mama Maria Nyerere utaratibu wa aina ya magazeti ya kusoma. Sasa mnataka pia kumuwekea utaratibu wa wageni wa kumtembelea. Sijui mkimaliza hilo mtamuwekea pia utaratibu wa kujisaidia chooni. Sasa atakuwa na tofauti gani na mfungwa aliyeko kwenye maximum prison?!
 

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Nadhani serikali ina mambo ya msingi inayotakiwa kufanya badala ya kufikiria kui-micro manage familia yoyote hapa nchini au nje ya nchi. Nadhani itabidi kwanza serikali ianze na haya hapa (ambayo naona ni ya muhimu zaidi kama Mwananchi)

1. Serikali inatakiwa kuja na majibu ya umaskini uliokithiri katika taifa ambalo ni la tatu kwa wingi wa rasilimali Africa, jambo ambalo imeshindwa vibaya, kulisimamia, huku Rais akisema hajui ni kwa nini!

2. Bado inatakiwa itoe majibu ya maana kuhusu kushuka kwa elimu, kiasi cha kufikia mhitimu wa kidato cha nne anafaulu mtihani wa kidato cha tano huku hajui hata kuandika jina lake,

3. Bado inatakiwa itoe maelezo ya kina kuhusu, umuhimu wa bajeti za serikali kuihusu tume ya maadili ya viongozi wa umma, kama viongozi walioza kitambo na wanazidi kuvunda kwa kila aina ya matendo maovu, ukiwemo ubakaji, wizi na uuaji,

4. Halafu itafute majibu ya ni kwa nini hakuna maendeleo ya nishati nchini, ambapo imefikia mahali makampuni binafsi hayaruhusiwi kuwekeza katika nishati mbadala, huku umeme ukiwa siyo wa uhakika iwe kuna mvua, ambapo watadai matope yamejaa mabwawani, au iwe kiangazi ambapo wataaema maji yamepungua!

Na bado kuna mengi ya serikali kufanya, badala ya kufikiria kuipangia wageni familia ya Mwalimu! Au wewe unaonaje?
 

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,372
2,000
Naona Mmempangia Nguo za Kuvaa hamjatosheka, Mumempangia Magazeti ya kusoma, Na sasa Mnataka Kumpangia hadi Marafiki na Majirani wa Kumtembelea na Kumjulia Hali. Je Mnataka Mama Afe? Si mu muue tu tujue moja?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom