Mr. Tanganyika
Member
- Nov 13, 2010
- 91
- 7
Tumeshaongelea sana suala hili lakini sichoki kudai tena serikali ya Tanganyika au mfumo mbadala wa muungano. Ule wimbo wa kero za muungano uliokuwa unapigiwa kelele na wazenji sasa hausikiki tena. Yaonesha wameshapata keki yao......sisi je?
1. Mzanzibari akiwa rais wa Tanzania, anateua wakuu wa mikoa ya Tanganyika a.k.a tz bara. Kwani ukuu wa mkoa na wilaya bara ni jambo la muungano? Hakuna rais kutoka Tanganyika aliyeweza kuteua wakuu wa mikoa zenji....labda Nyerere napo kwa mbinde.
2. Ikitokea rais wa Tanzania kutoka zenji akateua waziri mkuu pia toka zenji, tumekwisha....kwa sababu makamu hana kitu.
3. Katika bunge, mijadala hujadiliwa bila kutofautishwa kuwa hili ni la muungano na wabunge kutoka zenji wanachangia tu mambo yasiyowahusu, tunaelekea wapi?
4. Kama serikali ya muungano inashughulikia mambo ya muungano, na serikali ya zenji inahusika na mambo ya zenji, ni serikali ipi inahusika na mambo ya Tanganyika?
5. Baraza la wawakilishi linateua miongoni mwao watu kuja kuwa wabunge Dom, hili haliniingii akilini.
6. Katika kila msaada tunayopata kutoka nje, Z'bar wanapewa percent fulani. Lakini sasa Zanzibar wanakwenda wenyewe ulaya kuomba pesa na wanapata. Sasa kama wizara ya mambo ya nje ni ya muungano vipi kunakuwa na segment ya misaada kwa Zenji pekee, au wameunda kinyemela idara ya mambo ya nje?
7. Lilipokuja suala la mafuta, wabunge wote wa Zanzibar waliungana kuwa wabinafsi bila kujali itikadi zao. Chetu chao. Chao chao.
Ni wakati sasa wa wabunge wa Tanganyika kuungana bila kujali itikadi na kutupatia uhuru wetu Tanganyika