Je, ni vyuo gani vinaongoza kwa kutoa wasomi walioiva vizuri Tanzania?

Mkuu nahisi bado hujanipata pointi yangu ilipo. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba tunasoma ili tuajiriwe BASI kijana anapokosa ajira kinachofuata ni kilio haijalishi amesomea wapi na fani ipi.

Tuamke leo hii hakuna ajira serikalini wala taasisi binafsi je, jamii yetu ina njia mbadala wa kujikwamua na kutatua changamoto kimaisha nje ajira?

Au ndio hivyo tumemezwa na wanaohimiza vijana wajiajiri wakati wao wakipewa huduma zote za kibinadamu kwa kodi zetu bure. Kwanini wanaohamasisha kujiajiri wasiache kazi zao na kujiari kama kweli kujiajiri ni dili?

Mkuu tunahitaji kujiuliza maswali magumu magumu na kukipata majawabu yake kama taifa/jamii basi tutatoka pale tulipo.

Huo ushabiki wa UDSM na UDOM mimi binafsi nauona ni utoto na ulimbukeni tu sababu hata waliopita huko waneshindwa kuisaidia jamii wamebaki kuvaa nusu uchi na kata k huku wakiijita eti ni WASOMI.
Mkuu umetupa mawe matupu

Naamini ipo siku Taifa litafaidika na mawazo yako hasa kwa kuwekwa katika nafasi inayokufaa ili kufanikisha hili.
 
Mkuu umetupa mawe matupu

Naamini ipo siku Taifa litafaidika na mawazo yako hasa kwa kuwekwa katika nafasi inayokufaa ili kufanikisha hili.
Asante kwa kuniombea mema mkuu naamini yote yanawezekana chini ya jua.
 
Hakuna chuo TZ kinachotoa wasomi walioiva. Atakayetaja chuo anijibie haya maswali mawili.

1. Ukiowaondolea wasomi wetu kujua kusoma na kuandika unahisi watabaki na nini cha kujivunia kuwa walikipata huko vyuoni?

2. Ukiwaondolea ajira walizonazo muda huu je, wana mbinu mbadala za kuendesha maisha nje ya ajira ambazo mbinu hizo wamezipata huko chuoni?

NB. Elimu yetu inahitaji marekebisho MAKUBWA SANA ili imukomboe Mtanzania kutoka pale alipo kifikra, kijamii, kiuchumi, nk
Naomba nikujibu kiufupi mkuu: ( From chuo cha kilimo (SUA))
01. Kikubwa nitajivunia swala kubwa la usimamizi wa mazao ya kilimo na mifugo katika nyanja mbili ikiwa ni, kilimo hai (organic farming) na kilimo cha kawaida (conventional farming).
02. Kupitia swala la usimamizi wa kilimo kwa ujumla naweza jishughulisha na kilimo nikiwa nje ya Chuo kiukamilifu kabisa.
Ahsante!
 
Wameiva, weka chumvi sasa
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
 
Watu wana div one ya point 4 ,wapo udom,mtu ana div 2 au div 3 yupo udsm, sasa kuna tofaut gan hapo,,na kuna mtu kasoma saut yupo nondo kuliko wa udsm
 
Udsm ndyo chuo kilichotoa watu wengi wanaojiita wasomi hapa Tanzania lakin hawana impact yoyte kwa jamii zaid ya ufisadi na kutokuwa creative, sasa cjui ubora wake upi hapo mkuu, umaskin ndyo kwanza ulizd bora hta sasa hv vyuo kma saut, udom tunaona kidgo madiliko kwenye jamii huko
 
Naomba nikujibu kiufupi mkuu: ( From chuo cha kilimo (SUA))
01. Kikubwa nitajivunia swala kubwa la usimamizi wa mazao ya kilimo na mifugo katika nyanja mbili ikiwa ni, kilimo hai (organic farming) na kilimo cha kawaida (conventional farming).
02. Kupitia swala la usimamizi wa kilimo kwa ujumla naweza jishughulisha na kilimo nikiwa nje ya Chuo kiukamilifu kabisa.
Ahsante!
Mkuu umenijibu kinadharia sana. Kilimo ni biashara hivyo kinahitaji mtaji, mvua/umwagiliaji, mbolea, vibarua, dawa, shamba la kulima, mbegu, usimamizi pamoja na ghala la kutunzia mazao yako.

Hivyo vyote hujasema utatumia njia gani kuvipata sababu naamini toka darasa la awali hadi kidato cha sita hukuwahi kuwa mkulima sababu muda wote ulikuwa darasani ukisoma. Huko SUA umeenda ukiwa na umri wako wa kutosha na kwa muda huo huwezi kunishawishi eti umeiva kushika wakati huku chini hukuwahi.

Mkuu kilimo ni levo nyingine kabisa ambayo vijana wengi hawataki kuisikia masikioni mwao ila utawasikia wanasema natafuta mtaji ili nifanye biashara mimi kulima hamna. Hawajui kuwa msemo usemao "ukitaka mali utaipata shambani".

Mkuu jipange upya uje na mchanganuo make majibu uliyonipa unanifanya niendelee kuthibitisha kuwa mfumo wetu wa elimu unawapotosha vijana. Wakiwa huko vyuoni wanajiona tayari wamemudu maisha ila wakifika mtaani wanakuta hali tofauti na wanaishia kujiua au kuwa mateja.
 
Udsm ndyo chuo kilichotoa watu wengi wanaojiita wasomi hapa Tanzania lakin hawana impact yoyte kwa jamii zaid ya ufisadi na kutokuwa creative, sasa cjui ubora wake upi hapo mkuu, umaskin ndyo kwanza ulizd bora hta sasa hv vyuo kma saut, udom tunaona kidgo madiliko kwenye jamii huko
Kweli, Udsm ni chuo kongwe hapa nchini,lakini impact ya wasomi walozalishwa ni sifuri, waangalie akina Palamangamba, Bashiru walipokuwa pale chuoni walionekana wanaharakati, walipotupiwa mfupa wamekuwa wachumia tumbo, Benki kuu inaongozwa na Profesa toka Udsm,bosi wa nyumba naye mhitimu hukohuko,lakini uchumi unamfia sasa hivi, Sifa ya chuo ni pamoja na wasomi wake kuwa na fikra za kuwatoa wananchi katika lindi la umasikini kwa kusaidia serikali kujinasua kiuchumi na kuwa wabunifu wa kiteknolojia itakayowekezwa kubadilisha maisha ya wananchi wa nchi hii.
 
Hakuna chuo TZ kinachotoa wasomi walioiva. Atakayetaja chuo anijibie haya maswali mawili.
1. Ukiowaondolea wasomi wetu kujua kusoma na kuandika unahisi watabaki na nini cha kujivunia kuwa walikipata huko vyuoni?
2. Ukiwaondolea ajira walizonazo muda huu je, wana mbinu mbadala za kuendesha maisha nje ya ajira ambazo mbinu hizo wamezipata huko chuoni?
NB. Elimu yetu inahitaji marekebisho MAKUBWA SANA ili imukomboe Mtanzania kutoka pale alipo kifikra, kijamii, kiuchumi, nk
. NATIONAL COLLEGE OF TOURISM ....BEST OF BEST IN TOURISM
 
Kwa sasa Chuo kikuu kinachotoa wahitimu Bora ni Open University of Tanzania. Chuo hiki kinaenda na mabadiliko ya Technology,kina platform moja ya kujifunzia online inaitwa "Moodle" ambayo nadhani hakuna Chuo chochote hapa Nchini kinayo! Pili Wanafunzi wa OUT wanasoma kwa mfumo " Kuku wa Kienyeji", wanajitafutia materials na hawasomi handouts " madesa" kama Vyuo vikuu vingine!
Na hivyo kwa Wanafunzi wa OUT ambao wako serious wako deep sana!
Tatu,nafasi ya degree za " chu.pi " hakuna kwani Instructors na Wanafunzi kukutana ni mara chache sana !
Hizi degree za chu*p* ziko nyingi mzee hahaha
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, karibuni tujadili bila upendeleo wala chuki yoyote. Mfano inajulikana wanafunzi wengi wanaosoma University of Dodoma ni wale ambao alama zao hazikutosha kusoma University of Dar es salaam n.k hivyo kujikuta wanaangukia kwenye kapu la Udom.

Vivo hivyo wanafunzi wengi wa SAUT ni wale ambao wamejikongoja kutoka shule za kata na wengine wale waliofaulu kwa kurudia mitihani( reseaters) na wale ambao wameunga unga kwa nguvu kuanzia certificate, diploma mpaka degrees.

Kuna wale wa vyuo kama Sebastian Kolowa, Meru University, St Joseph and the likes ambako wanaenda wale ambao lengo lao ni kusomeka ana degree bila kujali hiyo degree imetoka chuo gani.

NB: Karibu tuchangie kwa uhuru na bashasha
Chuo kikuu cha Dar es salaam, Chuo kikuu cha kilimo Sokoine , Chuo kikuu cha mzumbe na chuo kikuu cha Muhimbili. Hivi ni vyuo vikongwe zaidi katika historia ya nchi. Ila chamsingi siku hixi mtu Una degree bila kujuali Chuo. Ukiwa na degree inatosha . kwasababu kuna watu wamesoma vyuo vya kata halafu masters wanapata nafasi katika vyuo hapo juu. Ilimradi Una degree inatosha.
 
Nimefanya kazi kwa miaka 20 sasa ila nikiri wazi WAHITIMU KUTOKA MZUMBE UNIVERSITY hasa wale kutoka kada za UHASIBU, SHERIA NA UTAWALA wanakuwa smart sana.. UDSM pia wapo smart ila si sawa na wale wa mzumbe..
Kwenye kilimo wapi wapo smart na madaktari . Kila chuo kina umuhimu wake .
 
Uzuri ni relative. Mimi ningeenda open. Maana wanakubalika na waajiri!
 
Msomi kama msomi ni yule mwelewa , kuingia darasa haina maana ww ndo mwenye akili, tu ,bali kuna wenye akili hawajaingia darasani lkn akianza shughuli za kufahamu kitu huwa hashindwi kitu kuna dogo moja hajasomea computer lkn usomi wake ni online huyu ni kiboko mji mzima anatikisa excell kaisomea online leo hii anafinyanga sijapata kuona ..
 
Back
Top Bottom